Sasa mkuu kama wapinzani ndiyo watekaji mbona ni rahisi sana kuwapeleka mahakamani na kuuaminisha umma kwamba serikali yetu haihusiki na vitendo vya kigaidi kama hivi?
Kumbuka taswira ya nchi imechafuka kimataifa kuhusiana na vitendo vya utekaji, mauaji na ugaidi vinavyoendelea huku lawama zikielekezwa kwa serikali.
Yaani wafanye hivyo wapinzani halafu wasiumbuliwe hadharani? Tumia akili hiyo hiyo kidogo uliyojaaliwa mkuu kutafakari.
Wapinzani ndiyo miaka yote wanalilia uchunguzi huru hata ikibidi wa kimataifa lakini serikali haitaki. Hadi hapo hujagundua shida ipo wapi?