Mpaka sasa nalishangaa taifa langu.
Mataifa yenye ujuzi wa watu, ujuzi wa technolojia na uwezo wa kiuchumi unowafanya wapige hatua kubwa sana katika sekta ya afya wanazuia wageni kuingia nchini mwao. Eti nchi kama Tanzania wanaendelea kusema tutaendelea kuwapima wageni?
Kwanini hamjifunzi kwa mgonjwa mliyemtangaza kuwa wa kwanza, aliingia akaingia mitaani ametokea mitaani kwenda hospitali bado tunajiona tutawapima wageni kubaini.
Hamuoni jinsi mnavyohangaika kutafuta amegusana na nani huko mitaani?
Hamjiulizi ni wangapi wanaweza kuingia nchini, pengine wakiwa hawajaanza kuonesha dalili.
Hivi mnatambua jinsi life style yetu jinsi ilivyo ni kama petroli ambazo zikishika korona hivi mnaweza kuidhibiti?
Hivi mnatambua ni athari gani kiuchumi tutapata kama taifa iwapo kutatokea mlipuko wa corona? inawezekana tunatumia "feki experts" wanatushauri tukifunga mipaka tutaathiri uchumi wetu bila kutambua kuwa kukilipuka corona nchi yetu mtailaani hakuna mtalii atakuja pengine kwa miaka mitano ijayo.
Sisi tunaona kuzuia wataalii kwa miezi michache tu ili janga la korona lipite na tujenge imani kwa watu, tunafikiri pengine mda huu wengine wamefunga ndiyo wa kupata lakini tutambue tunaweza kupatikana.
Tutazame mbali zaidi na tutambue wenzetu wakidhibiti ugonjwa ukadhibitiwa ukaisha na sisi kwetu tukaukaribisha ukazagaa, kwa wengine utaisha kwetu utabaki na wenzetu watatu-blacklist kwa kila kitu. Watu wetu watazuiwa na bidhaa zetu zutazuiwa na hapo ndipo tutajiuliza tulikataa kuzuia kutafuta nini na itatuchukua muda mrefu kuwashawishi warudi kwetu.
Njia pekee ya kuwa salama kiafya na kiuchumi ni kuchukua tahadhali sasa hasa kwa kufunga shughuli zote za utalii.
Wageni kutoka Ulaya, Marekani, China, Iran, S. Korea ni lazima tuwazuie sasa kwa bright future ya nchi yetu, ingawa wale tu ambao wanatizama kwenye viganja vya mikono yao tu hawawezi kukubali maana hawaoni mbali huko mbele tuendako.