Njia pekee ya kuzuia CORONA Tanzania Ni kuzuia watu kuingia na kutoka nchini

Njia pekee ya kuzuia CORONA Tanzania Ni kuzuia watu kuingia na kutoka nchini

Dalili za wazi kabisa ni kuwa Korona ipo Tanzania tayari. Ila serikali imeamua kuificha isijulikane kama ipo.
 
Tumesema na kushauri sana kuwa serikali izuie ndege kuingia humu nchini kama moja ya hatua za kudhibiti korona kuingia humu nchini.

Tukumbuke kama tu katika baadhi ya vituo vyetu vya afya,wamama wajawazito wanatumia chemli kujifungulia kutokana tu na umasikini na uhaba wa vitendea kazi, sasa tujiulize hali itakuwaje kwa hili gonjwa jipya?

Katika moja ya thread zangu nilitahadhirisha kwa kuzingatia mambo haya manne:

1. Umasikini wetu kama nchi
2. Ukubwa wa nchi yetu
3. Teknolojia duni tuliyonayo kama nchi
4. Elimu/ufahamu duni juu ya ugonjwa huu

Kama tunaendelea kuruhusu ndege kuingia nchini, serikali izuie ibada na mikusanyiko mingine yote isiyo ya lazima ikiwemo kudhibiti masoko.

Tupende, tusipende, haya mambo manne ndio yatakwenda kutufanya tuathirike vibaya na ugonjwa huu unless Mungu atasaidia ugonjwa huu utoweke bila kuleta majanga humu nchini.

Hata hivyo, kinachonishangaza ni kwanini mpaka muda hakuna tangazo la kusitisha uingiaji wa ndege humu nchini?

Kama mpaka muda huu hatujatoa tangazo, maana yake ni kuwa tunalazimika kuruhusu ndege kuingia nchini kwa siku kadhaa zijazo kwasababu huwezi toa tangazo leo na leo leo ukaanza kulifanyia kazi kwani itabidi utoe muda ili mashirika ya ndege yawezi ku-cancel safari zao.

Huu ni zaidi ya uzembe!!!
 
Mkuu bado tupo bize na kiki za kuomba kura uchaguzi wa 2020,bado tunashughulikia wahandisi na kutembelea daraja wenyewe.
 
Huo ugonjwa Ni Kama dunia imetupiwa adhabu, viongozi dunia nzima wamekuwa Kama mazezeta kiasi kwamba wamekuwa wagumu kuchukua maamzi sahihi kwa wakati sahihi Hadi pale gonjwa linapokuwa limetua rasmi ndo utaanza kuona wanahangaika kumbe wameshachelewa
 
[emoji51][emoji51][emoji51]
millardayo_B9q0bqzAr5p.jpeg
1584092525_1584092525-picsay.jpeg
 
Ule msemo wa maskini jeuri ndio maana huwa siuamini, ukishakuwa maskini huwezi kuwa na jeuri.

Hivi tupo tayari hata kuanzisha vituo vya kupima wagonjwa wa Corona kwenye viwanja vyetu vyote vya ndege nchini, na maeneo yote ya mipakani?

Je, tunavyo vifaa vya kutosha?

Au mpaka tupate msaada toka nje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mgojwa wa kwanza katushinda apemenya, na kwa kifupi wataalam wetu mipakani na viwanja vya ndege wanamtegemea mhusika mwenyewe ndo aseme wala sio vipimo vyao na kama vipimo vingekuwepo sampuli isingepelekwa Dar.
 
Huyo mgojwa wa kwanza katushinda apemenya, na kwa kifupi wataalam wetu mipakani na viwanja vya ndege wanamtegemea mhusika mwenyewe ndo aseme wala sio vipimo vyao na kama vipimo vingekuwepo sampuli isingepelekwa Dar.
Airport zote duniani wanachofanya ni temperature screening ndio maana wanalazimisha watu wakae siku 14 isolation kabla ya kuingia mtaani kwao , hivyo kupita airport sio ajabu.

Tatizo ni kwa nini serikali inapata kigugumizi kufunga mipaka, ni hadi ugonjwa usambae mitaani ndio mfunge mipaka? Kheri nusu shari kuliko shari kamili, serikali wafunge mipaka na kinachoruhusiwa kupita iwe bidhaa na Mtz tu, na huyo mtz ni lazima akae siku 14 isolation kabla ya kuingia mtaani.
 
Usiwe muongo sana . Hakuna vibatari tena mahospitalini
Solar zinatumika sana kila mahali
 
Nimeshtuka sana kusikia kwamba USA kuanzia jumamosi wanapiga marufuku safari zote za kutokea ulaya kuanzia jumamosi ijayo, lakini huku Tanzania hata waChina tunawaruhusu kama nyumbu wako kwenye migration, hii maana yake nini?
 
Wenye mamlaka ya kusitisha hilo wanaamini familia zao ziko salama na wanaweza kuishi miaka miwili na zaidi pasipo kujishughulisha na shughuli za kiuchumi hivyo wanaona wengine pia wao kama wao.
 
Mpaka sasa nalishangaa taifa langu.

Mataifa yenye ujuzi wa watu, ujuzi wa technolojia na uwezo wa kiuchumi unowafanya wapige hatua kubwa sana katika sekta ya afya wanazuia wageni kuingia nchini mwao. Eti nchi kama Tanzania wanaendelea kusema tutaendelea kuwapima wageni?

Kwanini hamjifunzi kwa mgonjwa mliyemtangaza kuwa wa kwanza, aliingia akaingia mitaani ametokea mitaani kwenda hospitali bado tunajiona tutawapima wageni kubaini.

Hamuoni jinsi mnavyohangaika kutafuta amegusana na nani huko mitaani?

Hamjiulizi ni wangapi wanaweza kuingia nchini, pengine wakiwa hawajaanza kuonesha dalili.

Hivi mnatambua jinsi life style yetu jinsi ilivyo ni kama petroli ambazo zikishika korona hivi mnaweza kuidhibiti?

Hivi mnatambua ni athari gani kiuchumi tutapata kama taifa iwapo kutatokea mlipuko wa corona? inawezekana tunatumia "feki experts" wanatushauri tukifunga mipaka tutaathiri uchumi wetu bila kutambua kuwa kukilipuka corona nchi yetu mtailaani hakuna mtalii atakuja pengine kwa miaka mitano ijayo.

Sisi tunaona kuzuia wataalii kwa miezi michache tu ili janga la korona lipite na tujenge imani kwa watu, tunafikiri pengine mda huu wengine wamefunga ndiyo wa kupata lakini tutambue tunaweza kupatikana.

Tutazame mbali zaidi na tutambue wenzetu wakidhibiti ugonjwa ukadhibitiwa ukaisha na sisi kwetu tukaukaribisha ukazagaa, kwa wengine utaisha kwetu utabaki na wenzetu watatu-blacklist kwa kila kitu. Watu wetu watazuiwa na bidhaa zetu zutazuiwa na hapo ndipo tutajiuliza tulikataa kuzuia kutafuta nini na itatuchukua muda mrefu kuwashawishi warudi kwetu.

Njia pekee ya kuwa salama kiafya na kiuchumi ni kuchukua tahadhali sasa hasa kwa kufunga shughuli zote za utalii.

Wageni kutoka Ulaya, Marekani, China, Iran, S. Korea ni lazima tuwazuie sasa kwa bright future ya nchi yetu, ingawa wale tu ambao wanatizama kwenye viganja vya mikono yao tu hawawezi kukubali maana hawaoni mbali huko mbele tuendako.
 
Back
Top Bottom