Njia rahisi ya kupata nafasi (cheo) ndani ya CCM au Serikalini kupitia siasa.

Joined
Oct 20, 2020
Posts
42
Reaction score
32
Kwa Tanzania kama unataka kuendesha maisha yako kupitia siasa unatakiwa uwe ndani ya CCM kwani ndio chama kilichoshika dola. Ukiwa ndani ya CCM ni rahisi kupata nafasi (cheo) ndani ya chama au Serikalini. Lakini tatizo CCM ina watu wengi sana kuliko nafasi za uongozi au vyeo vya kuwapa wanachama wake. Sasa kuna njia rahisi ya kupata nafasi (cheo) ndani ya CCM au Serikalini kupitia siasa. Ukitumia njia hii unakuwa na possibility ya asilimia kuanzia 85 hadi 100 kupata nafasi.

Njia yenyewe ni kuanzia au kupitia CHADEMA. Kama wewe ni kijana na ndoto yako ni kula maisha kupitia siasa basi usianzie moja kwa moja CCM kwa sababu utachelewa kuonekana kama nilivyosema awali CCM ina watu wengi. Kwa hiyo anzia kwenye chama cha upinzania chenye nguvu kama CHADEMA ukishapata umaarufu huko toka ingia CCM. Nakuhakikishia utapata nafasi kiulaini kabisa. Angalia mfano David Silinde, Patrobas Katambi, Mwita Waitara na wengineo.

Kama huamini hiki ninachokisema kama hujulikani wewe au mzazi wako nenda kaanzie CCM uone kama hujasugua benchi mpaka uzeeni. CCM kuna watu wapo tangu enzi na enzi mpaka sasa wanazeeka hawajawahi kupewa hata udiwani lakini karibu wote waliotoka vyama vya upinzani wamekula maisha.

NB: Siasa ni mchezo wa akili na timing, mfano mwingine utauona kwa Peter Msigwa, soon anaenda kupewa chaka maisha yanaendelea.
 
Ila Kuna jamaa mmoja mke wake nimiongoni mwa wale wabunge 19 waliotokea CHADEMA. Yule jamaa kwakweli anaonekana hana bahati.
Amekua chawa lakini hajafaidika bado
 
Kwa Tanzania kama unataka kuendesha maisha yako kupitia siasa unatakiwa uwe ndani ya CCM kwani ndio chama kilichoshika dola. Ukiwa ndani ya CCM ni rahisi kupata nafasi (cheo) ndani ya chama au Serikalini. Lakini tatizo CCM ina watu wengi sana kuliko nafasi za uongozi au vyeo vya kuwapa wanachama wake. Sasa kuna njia rahisi ya kupata nafasi (cheo) ndani ya CCM au Serikalini kupitia siasa. Ukitumia njia hii unakuwa na possibility ya asilimia kuanzia 85 hadi 100 kupata nafasi.

Njia yenyewe ni kuanzia au kupitia CHADEMA. Kama wewe ni kijana na ndoto yako ni kula maisha kupitia siasa basi usianzie moja kwa moja CCM kwa sababu utachelewa kuonekana kama nilivyosema awali CCM ina watu wengi. Kwa hiyo anzia kwenye chama cha upinzania chenye nguvu kama CHADEMA ukishapata umaarufu huko toka ingia CCM. Nakuhakikishia utapata nafasi kiulaini kabisa. Angalia mfano David Silinde, Patrobas Katambi, Mwita Waitara na wengineo.

Kama huamini hiki ninachokisema kama hujulikani wewe au mzazi wako nenda kaanzie CCM uone kama hujasugua benchi mpaka uzeeni. CCM kuna watu wapo tangu enzi na enzi mpaka sasa wanazeeka hawajawahi kupewa hata udiwani lakini karibu wote waliotoka vyama vya upinzani wamekula maisha.

NB: Siasa ni mchezo wa akili na timing, mfano mwingine utauona kwa Peter Msigwa, soon anaenda kupewa chaka maisha yanaendelea.
Ni kweli. Wengi wanaanzia upinzani lakini malengo ni kwenda ccm.

Asilimia kubwa ya wanasiasa uongo kwao ni kama dini kabisa!
 
Hii mbinu ya majambazi ya ccm ni ya kimkakati na imewekwa mahususi kama bait ya kuwanasa wenye njaa kama kina msigwa.
 
Back
Top Bottom