SoC01 Njia sahihi za kulea watoto ili waje kuwa viongozi wema na wenye kutii sheria za nchi

SoC01 Njia sahihi za kulea watoto ili waje kuwa viongozi wema na wenye kutii sheria za nchi

Stories of Change - 2021 Competition

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Habari yako ndugu msomaji.

Katika mambo yanayolalamikiwa na jamii yetu hasa zama hizi basi ni kuwa na viongozi ambao hawana maadili na wala hawafuati sheria mbalimbali za nchi vile zinavyotaka.

Jambo hili sio tatizo dogo kama tunavyolifikiria,na wala sio mazao ya malezi ya mwaka mmoja au miwili iliyopita,bali ni matunda ya muda mrefu ya tabia alizokuzwa nazo.

Sisi kama taifa la watanzania tunalo jukumu la kuhakikisha kwanza tunapata watu wenye kutii sheria bila shuruti,wenye kutii sheria bila ya kutumia nguvu ili watii sheria hizo.

kwa masikitiko tumekuwa na watu ambao hawatii sheria bila ya shuruti.

Kuwa na watu wa aina hii ni hasara na hatari kwa taifa kwa sababu watasababisha kila sheria ambayo itatungwa ionekane haifai kwa sababu ya wao kutofuata sheria za nchi.

Kila sifa ya kiongozi inaanzia utotoni kama vile uadilifu,uungwana,utii,hekima n.k haya yote huanzia utotoni..

Kama tunavyofahamu ya kwamba samaki mkunje angali mbichi,je sisi kama taifa tumejiandaa vipi kuzalisha watoto ambao watakuja kuwa viongozi bora na watiifu hapo baadae ?

Haya ni mambo ya kufanya kwa mwanao au mtoto yeyote ambaye unayo nafasi ya kumlea kuhakikisha kwamba atakuwa mtiifu na kiongozi bora hapo baadae.

1. hakikisha wewe mzazi ama mlezi unakuwa mkweli kwa mtoto katika mambo ambayo hata ufanye vipi basi baadae atakuja kujua ukweli wa mambo hayo.

Mfano.
Huna haja ya kumuambia mtoto kwamba watoto wanaozaliwa wananunuliwa dukani wakati jambo hili atakuja kuujua ukweli hapo baadae.

Kama mtoto anaambiwa kwamba ule ni moto na anatahadharishwa tokea utotoni Basi na jambo hili aambiwe ukweli pia.

Kumdanganya sasa hivi ni kuwaandaa waongo wa baadae,ukimjenga katika ukweli basi atakuwa kiongozi mkweli baadae na ukweli ni sifa muhimu kwa kiongozi.

2. Mshirikishe katika mambo madogo ambayo ungeweza kuamua wewe mwenyewe bila yeye kwa lengo la kumkuza awe mtu wa kushauriana na watu asiwe mtu wa analotaka yeye ndio liwe.

Mfano. Muulize tu hivi mwanangu kununua nguo tatu za sikukuu na kununua mbili na pesa inayobaki tukuwekee akiba kipi bora ?

Lengo ni kumfanya awe mpenda majadiliano,na hawezi kuwa mtu wa aina hiyo mpaka awe amekulia katika hali hiyo.

Lengo : tunahitaji viongozi wapenda majadiliano.

3. anapokosea mrekebishe kwa hoja na usitumie nguvu.hii itamfanya ajifunze kwamba sio kila kosa mtu anatakiwa aadhibiwe bali kuna mambo ya kufahamishwa.

Mfano. Akirudi usiku nyumbani mfahamishe muambie madhara ya kurudi usiku nyumbani badala ya kumpiga.

Lengo : tunataka viongozi wachache wa kuadhibu na kutesa watu.

4. Akiwa ni mkaidi katika jambo ulilomuambia mara nyingi basi muonye kwa adhabu ambayo inaendana na hali yake.

Lengo : Hii itamfanya baadae akiwa kiongozi asimfunge mtu miaka 10 kwa kosa la kuiba kuku.

5. Hakikisha anapokuomba kitu na ahadi ulizomuahidi unamtekelezea.
Mfano. Ukimuahidi kumnunulia baiskeli munulie kweli na umuambie "mwanangu kama sikutekeleza ahadi utaumia" itamfanya aone kwamba kutotekeleza ahadi kunamuumiza aliyeahidiwa.

Lengo : itamfanya yeye awe ni mtu mtekeleza ahadi kwa raia wake

6. Tunga visheria vidogo vidogo hapo nyumbani na wewe uwe wa kwanza kuvifuata visheria hivyo bila kuvunja.

Mfano. Tunga sheria kila mtu chombo anacholia chakula basi anatakiwa akoshe,alafu wewe kuwa kinara wa kufuata sheria hii na umuelezee faida za sheria hiyo kama vile kupunguza mzigo wa vyombo vingi(na sheria nyinginezo)

Lwngo : itamfanya azowee kufuata sheria bila kulazimishwa na mtu hata kaiwa kiongozi.

7. Hakikisha unamuonya na kumrekebisha akiwa peke yake tu,usimkaripie kwenye watu wengi.

Wakati mkiwa peke yenu umuambie kwamba nakugombeza tukiwa wawili tu kwa sababu wangekuwa wengine ungejisikia vizuri ? Lazima atajibu hapana.

Basi hiyo ndio iwe taratibu kila akikosea muite pembeni usiseme kwamba hivyo wanatakiwa wafanyiwe watu wazima hapana,watoto wanahitaji kufanyiwa ili nao waje wafanye hivyo baadae.

Lengo : awe kiongozi anayeepuka kuwarekebisha wenzie kwenye hadhira na kuwafedhehesha.

8. Hakikisha unamuuliza mwanao akupe ufafanuzii juu ya jambo alilosema hata kama unajua maana yake.

Mfano. " baba leo tumemsoma chura shuleni" muulize chura ndio nani ?
Hakikisha anakufafanulia na akishindwa mfahamishe.

Lengo : itamfanya yeye asiwe mtu wa chuki pale atakapokutana na watu wenye kumhoji akiwa kiongozi hapo baadae.

9. Hakikisha unapokosea jambo useme kwamba umekosea mbele ya mwanao usione aibu.

Lengo : itamfanya aone kukosea ni jambo la kawaida na wala sio fedheha kusema umekosea na kuepuka misemo ya " mkubwa hakosei" na atakuwa wempesi kuomba radhi pale anapokosea katika uongozi wake.

10. hakikisha haumtukani tusi lolote lile hata mkiwa peke yenu.

Nikupe siri kwamba hakuna faida hata moja ya tusi unalomtukana mtoto,badala yake itamzidishia misamiati mibaya kichwani mwake.

Lengo : kuepusha viongozi wenye matusi na maneno ya kifedhuli katika jamii.

11. Akiongea na wewe msikilize kwa makini.hii itamfanya na yeye aige umakini huo pale anapoongea na wengine.

Lengo : awe kiongozi mwenye usikivu makini kwa wananchi wake.

12. Panga kununua kitu kisicho muhimu mbele yake kisha ghairisha upange kununua kitu cha muhimu hapo hapo mbele yake.

Mfano. Sema huku anasikia "nataka kununua biskuti ya alfu 5000" kisha ghairisha sema " lakini biskuti ya 5000 nitakula itaisha ila viatu nitavaa muda mrwfu.

Lengo : awe kiongozi anayeepuka matumizi yasiyo na faida na kufanya mambo ya msingi kwa raia wake.

13. Hakikisha unajishusha kwa watu ambao mumewazidi status ya maisha na onesha kuwaheshimu mbele yake.

Kama muna jirani hohehahe basi siku kadhaa mpe pesa aandae chakula huyo jirani kisha nyie na mtoto wenu muende kula kwao yule jirani na mumuambie mtoto wenu kwamba jirani kayualika chakula.

Lengo : itamfanya asiwadharau aliowazidi na wala kudharau wito wao.

14. Usimfundishe kuomba pesa ili baadae asijekuwa kiongozi mpenda pesa na rushwa akawa mvunja sheria namba moja.

Kamwe muepushe na tabia ya kuomba pesa tokea akiwa mdogo,na siku kaikuomba hakikisha ana hoja za msingi.

HITIMISHO
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ukiyafuata na kuyafanya katika maisha yako unapokuwa na mwanao basi kuna asilimia kubwa mtoto huyu akaja kuwa kiongozi bora kabisa.

Lengo ni kufanya mazuri yawe mengi kuliko mabaya na wala hatuwezi kufikia lengo la kuondoa mabaya yote.

Asanteni sana nakaribisha maoni.
 
Upvote 25
Umesema vyema, wazazi na walezi inatupasa kua kielelezo katika malezi ya watoto, ila kwa maisha ya bongo ni ngumu maana mpaka mwalimu shuleni anamdanganya mtoto, sijui tunatengeneza vizazi vya namna gani
 
Hata umleeje mtoto,kama atakutana na watu wenye roho mbaya sampuli zilizopo CCM
Lengo la uzi ni kuwalea watoto ili waje kuwa viongozi wazuri.
CCM,amiini amini nami nakuandikia,hawezi kutupatia tunachohitaji kama jamii.
-Katiba mpya,
Katika kulea mtoto hakuhitaji katiba mpya.

Leo huwezi kusema mwanao unashindwa kumlea vizuri ati kwa sababu katiba ni ya zamani sio mpya.

Katika ishu ya kulea mtoto wako katiba haina nafasi hasa ukiangalia na muktadhwa wa mada yangu.
Wanajamii waliofundwa vema
Hawa wanajamii waliofundwa vyema ndio wanaanzia huku utotoni na ndio maana nikaandika uzi huu.

Usitegemee katiba itakuletea wana jamii ambao wamefundwa vyema katu.

Bali katiba inahitaji ikute hao wana jamii waliokuwa vyema ili waitendee haki katiba hiyo.

Hivyo tuungane pamoja tulee watoto katika misingi tajwa hapo juu na mingineyo,kwa sababu mtoto huyu ndio jamii ya kesho
 
Umesema vyema, wazazi na walezi inatupasa khwa kieleleza katika malezi ya watoto, ila kwa maisha ya bongo ni ngumu maana mpaka mwalimu shuleni anamdanganya mtoto, sijui tunatengeneza vizazi vya namna gani
Akija kwako mzazi usimdanganye tena bali muambie ukwi wa mambo na umuambie kwa nini mwalimu anadanganya watu.

Umuambie kwamba mnadanganywa kwa sababu mwalimu hataki muharibikiwe n.k

Yaani mzazi asimkandie mwalimu kwwa mwanawe bali mzazi ampe udhuru mwalimu kwamba amewaambia kadhaa kwa nia nzuri tu.

Hapo mtoto anapambanukiwa na ulimwengu.

Nakumbuka wakati namfundisha mdogo wangu ishu ya janaba la zinaa.

Nikamuambia kwamba janaba la zinaa ukikoga linatoka,yeye akaniambia mbona kuna masheikh nawasikia wanasema janaba la zinaa hata ukoge vipi halitoki mpaka zipite siku 40.

Nikamuambia kwamba masheikh hao wametumia hikma ili mtu upate hofu usizini wala hawana lengo baya kusema hivyo, lakini wewe unasoma unatakiwa ujue kwa nini wanasema hivyo.

Yule kijana akatoka ameridhika na anawaheshimu wale masheikh kuliko ningemuambia masheikh waongo haooooooooo.

Hahahhaa
 
Lengo la uzi ni kuwalea watoto ili waje kuwa viongozi wazuri.

Katika kulea mtoto hakuhitaji katiba mpya.

Leo huwezi kusema mwanao unashindwa kumlea vizuri ati kwa sababu katiba ni ya zamani sio mpya.

Katika ishu ya kulea mtoto wako katiba haina nafasi hasa ukiangalia na muktadhwa wa mada yangu.

Hawa wanajamii waliofundwa vyema ndio wanaanzia huku utotoni na ndio maana nikaandika uzi huu.

Usitegemee katiba itakuletea wana jamii ambao wamefundwa vyema katu.

Bali katiba inahitaji ikute hao wana jamii waliokuwa vyema ili waitendee haki katiba hiyo.

Hivyo tuungane pamoja tulee watoto katika misingi tajwa hapo juu na mingineyo,kwa sababu mtoto huyu ndio jamii ya kesho
Kwa hiyo weye unamlea mtoto wako vizuri halafu unamuacha aende akaishi na uncivilized creatures na mazingira yaso rafiki?Ni vema kukawa na guided rules.Bila good rules mtoto wako uliyemtunza vema ataungana na jamii corrupted to savages!
 
Kwa hiyo weye unamlea mtoto wako vizuri halafu unamuacha aende akaishi na uncivilized creatures na mazingira yaso rafiki
Sasa utampeleka wapi wakati anaishi katika jamii hiyo.

Lengo la kumlea ni kusudi asiharibiwe na jamii ambayo inamzungika iliyoharibika.

Na ndio lengo la mtu kumfundisha mazuri,lengo aepuke mabaya.

Sasa mtoto wako sijui utampeleka wapi wakati yupo katika jamii ya watu wabaya.

Muache aishi hapo awaoneshe mema wengine wabadilike.
Ni vema kukawa na guided rules
Kulea mtoto hakuhitaji guide rules bali inahitaji maamuzi ya mlezi.
Bila good rules mtoto wako uliyemtunza vema ataungana na jamii corrupted to savages!
Hakuna sheria inayoruhusu rushwa.

Hakuna sheria inayoruhusu mauwaji.

Hivyo ukimlea mtoto kimisingi mizuri atafuata sheria na ataachana ma mambo mabaya wanayoyafanya wengine.

Kumbuka tunazungumzia malezi ya watoto namna gani wakilelewa watakuja kuwa viongozi bora
 
Sasa utampeleka wapi wakati anaishi katika jamii hiyo.

Lengo la kumlea ni kusudi asiharibiwe na jamii ambayo inamzungika iliyoharibika.

Na ndio lengo la mtu kumfundisha mazuri,lengo aepuke mabaya.

Sasa mtoto wako sijui utampeleka wapi wakati yupo katika jamii ya watu wabaya.

Muache aishi hapo awaoneshe mema wengine wabadilike.

Kulea mtoto hakuhitaji guide rules bali inahitaji maamuzi ya mlezi.

Hakuna sheria inayoruhusu rushwa.

Hakuna sheria inayoruhusu mauwaji.

Hivyo ukimlea mtoto kimisingi mizuri atafuata sheria na ataachana ma mambo mabaya wanayoyafanya wengine.

Kumbuka tunazungumzia malezi ya watoto namna gani wakilelewa watakuja kuwa viongozi bora
Sijajua kama umenielewa kabla ya Uhuru wa Tanganyika!Nina maanisha hivi;Pamoja na kumlea mtoto wako,umeandaaje au jamii inaandaaje mazingira rafiki au bora ya kudumisha ubora wa mwanao?Umehangaika kumlea kwa uzuri halafu unamuachia aende akaishi kwenye dunia iliyojaa wahuni na mazingira ya kihuni?Tafakari.
 
Umehangaika kumlea kwa uzuri halafu unamuachia aende akaishi kwenye dunia iliyojaa wahuni na mazingira ya kihuni?Tafakari.
Kwa hiyo kama mazingira ni ya kihuni maana yake tusilee watoto kistaarabu na kiungwana badala ya ke tuwaache wajiendee tu na tabia za ovyo wakue nazo ?
umeandaaje au jamii inaandaaje mazingira rafiki au bora ya kudumisha ubora wa mwanao?
Hiyo jamii ikiamua kulea kama ninavyolea mimi bila shaka tutapata kizazi bora.

Mazingira rafiki yanaletwa na jamii bora.

Hivyo solution sio jamii inamuandalia vipi mazingira mwanangu,hii sio solution

Kwa sababu mwanangu hatoishi milele,ataondoka alafu itabaki jamii ile ile kuendeleza ushenzi.

Solution ni kuibadilisha hiyo jamii nayo ili tupate solution ya kudumu.,na tunaibadilisha jamii kwa kubadilisha namna ya kuwalea watoto.

Jamii nayo ilee watoto kwa mfumo kama huu ndipo tutafikia katika maisha mazuri ya kiuongozi.
 
Kwa hiyo kama mazingira ni ya kihuni maana yake tusilee watoto kistaarabu na kiungwana badala ya ke tuwaache wajiendee tu na tabia za ovyo wakue nazo ?

Hiyo jamii ikiamua kulea kama ninavyolea mimi bila shaka tutapata kizazi bora.

Mazingira rafiki yanaletwa na jamii bora.

Hivyo solution sio jamii inamuandalia vipi mazingira mwanangu,hii sio solution

Kwa sababu mwanangu hatoishi milele,ataondoka alafu itabaki jamii ile ile kuendeleza ushenzi.

Solution ni kuibadilisha hiyo jamii nayo ili tupate solution ya kudumu.,na tunaibadilisha jamii kwa kubadilisha namna ya kuwalea watoto.

Jamii nayo ilee watoto kwa mfumo kama huu ndipo tutafikia katika maisha mazuri ya kiuongozi.
Kumbe majibu unayo?Kwa nini hautaki katiba mpya iliyo bora zaidi.
 
Kama niliyokupa.

Majibu yangu hayaendani na kutegemea katiba,majibu yangu yanaendana na kutegemea kuilea jamii kwanza.

Suala la katiba ni la kwako wewe sijalizungumzia kama inavyotaka uniaminishe mkuu😊
Holy moly!Unaileaje jamii tena watoto,halafu unawaachia kwenye dimbwi (maisha haya)lililojaa luba?Tunapaswa kuenenda kotekote.Umemlea mtoto wako vema halafu unampeleka shule ya bweni anageuka kuwa shoga(mwanaume) au msagaji(wa kike)?Ni sawa tu na kujilisha (siyo kula kwa kiasi na matazamio mema) ugali mkuuubwa tu bila mpango halafu utegemee kudra za wapita njia wasio wema.😝😝😝😝
 
halafu unawaachia kwenye dimbwi (maisha haya)lililojaa luba?
Una maanisha tusiwalee vizuri kwa sababu kuna dimbwi la luba ?
Tunapaswa kuenenda kotekote.
Kote kote wapi na wapi ?
Umemlea mtoto wako vema halafu unampeleka shule ya bweni anageuka kuwa shoga(mwanaume) au msagaji(wa kike)?
Na kwa jamii ya tanzania ushoga haukubaliki japokuwa watu wanafanya

Hata sheria zinakataa ushoga lakini katika jamii wapo.

Hivyo kilichobaki ni kurekebisha jamii na watoto wetu huu ushoga uondoke.
Katika kurekebisha huko sasa ni kila mtu aanze kumlea vizuri mwanawe.
 
Una maanisha tusiwalee vizuri kwa sababu kuna dimbwi la luba ?

Kote kote wapi na wapi ?

Na kwa jamii ya tanzania ushoga haukubaliki japokuwa watu wanafanya

Hata sheria zinakataa ushoga lakini katika jamii wapo.

Hivyo kilichobaki ni kurekebisha jamii na watoto wetu huu ushoga uondoke.
Katika kurekebisha huko sasa ni kila mtu aanze kumlea vizuri mwanawe.
Sitaki kukufundisha kujibu lakini huwezi jidai una maadili nyumbani kwako halafu watoto wakitoka kwako wawe "mahoka" kwa kuenenda watakayoyakuta kwenye jamii.
 
Sitaki kukufundisha kujibu lakini huwezi jidai una maadili nyumbani kwako halafu watoto wakitoka kwako wawe "mahoka" kwa kuenenda watakayoyakuta kwenye jamii.
Ndo nakuuliza hivi kwa kuwa jamii ni mbovu je na watoto nao tusiwalee vizuri nao tuwaache waharibike ili waongeze idadi ya wahuni mtaaani ?

Nijibu hapa kwanza.
 
Ni wazo zuri sana ila unadhani ni nani wakumfanya aje kuwa baba au mama, raisi (kiongozi) bora wakati wanaharibikiwa mikononi mwetu
 
Ndo nakuambia kwa kuwa jamii ni mbovu na watoto tusiwalee vizuri nao tuwaache waongeze idadi ya wahuni mtaaani ?

Nijibu hapa kwanza.
Fuatilia tangu mwanzo.Nimeeleza ukiwalea wanao vema bila kuisafisha jamii yote ili ienende kwenye misingi bora unajihangaisha tu.Nikakushauri,maana ulitaka pia tupate na viongozi wazuri kijamii,ni vema tukaandaa na misingi au miongozo ya kuwabana kivitendo wawe na maadili bora.
 
Back
Top Bottom