SoC01 Njia sahihi za kulea watoto ili waje kuwa viongozi wema na wenye kutii sheria za nchi

Stories of Change - 2021 Competition

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Habari yako ndugu msomaji.

Katika mambo yanayolalamikiwa na jamii yetu hasa zama hizi basi ni kuwa na viongozi ambao hawana maadili na wala hawafuati sheria mbalimbali za nchi vile zinavyotaka.

Jambo hili sio tatizo dogo kama tunavyolifikiria,na wala sio mazao ya malezi ya mwaka mmoja au miwili iliyopita,bali ni matunda ya muda mrefu ya tabia alizokuzwa nazo.

Sisi kama taifa la watanzania tunalo jukumu la kuhakikisha kwanza tunapata watu wenye kutii sheria bila shuruti,wenye kutii sheria bila ya kutumia nguvu ili watii sheria hizo.

kwa masikitiko tumekuwa na watu ambao hawatii sheria bila ya shuruti.

Kuwa na watu wa aina hii ni hasara na hatari kwa taifa kwa sababu watasababisha kila sheria ambayo itatungwa ionekane haifai kwa sababu ya wao kutofuata sheria za nchi.

Kila sifa ya kiongozi inaanzia utotoni kama vile uadilifu,uungwana,utii,hekima n.k haya yote huanzia utotoni..

Kama tunavyofahamu ya kwamba samaki mkunje angali mbichi,je sisi kama taifa tumejiandaa vipi kuzalisha watoto ambao watakuja kuwa viongozi bora na watiifu hapo baadae ?

Haya ni mambo ya kufanya kwa mwanao au mtoto yeyote ambaye unayo nafasi ya kumlea kuhakikisha kwamba atakuwa mtiifu na kiongozi bora hapo baadae.

1. hakikisha wewe mzazi ama mlezi unakuwa mkweli kwa mtoto katika mambo ambayo hata ufanye vipi basi baadae atakuja kujua ukweli wa mambo hayo.

Mfano.
Huna haja ya kumuambia mtoto kwamba watoto wanaozaliwa wananunuliwa dukani wakati jambo hili atakuja kuujua ukweli hapo baadae.

Kama mtoto anaambiwa kwamba ule ni moto na anatahadharishwa tokea utotoni Basi na jambo hili aambiwe ukweli pia.

Kumdanganya sasa hivi ni kuwaandaa waongo wa baadae,ukimjenga katika ukweli basi atakuwa kiongozi mkweli baadae na ukweli ni sifa muhimu kwa kiongozi.

2. Mshirikishe katika mambo madogo ambayo ungeweza kuamua wewe mwenyewe bila yeye kwa lengo la kumkuza awe mtu wa kushauriana na watu asiwe mtu wa analotaka yeye ndio liwe.

Mfano. Muulize tu hivi mwanangu kununua nguo tatu za sikukuu na kununua mbili na pesa inayobaki tukuwekee akiba kipi bora ?

Lengo ni kumfanya awe mpenda majadiliano,na hawezi kuwa mtu wa aina hiyo mpaka awe amekulia katika hali hiyo.

Lengo : tunahitaji viongozi wapenda majadiliano.

3. anapokosea mrekebishe kwa hoja na usitumie nguvu.hii itamfanya ajifunze kwamba sio kila kosa mtu anatakiwa aadhibiwe bali kuna mambo ya kufahamishwa.

Mfano. Akirudi usiku nyumbani mfahamishe muambie madhara ya kurudi usiku nyumbani badala ya kumpiga.

Lengo : tunataka viongozi wachache wa kuadhibu na kutesa watu.

4. Akiwa ni mkaidi katika jambo ulilomuambia mara nyingi basi muonye kwa adhabu ambayo inaendana na hali yake.

Lengo : Hii itamfanya baadae akiwa kiongozi asimfunge mtu miaka 10 kwa kosa la kuiba kuku.

5. Hakikisha anapokuomba kitu na ahadi ulizomuahidi unamtekelezea.
Mfano. Ukimuahidi kumnunulia baiskeli munulie kweli na umuambie "mwanangu kama sikutekeleza ahadi utaumia" itamfanya aone kwamba kutotekeleza ahadi kunamuumiza aliyeahidiwa.

Lengo : itamfanya yeye awe ni mtu mtekeleza ahadi kwa raia wake

6. Tunga visheria vidogo vidogo hapo nyumbani na wewe uwe wa kwanza kuvifuata visheria hivyo bila kuvunja.

Mfano. Tunga sheria kila mtu chombo anacholia chakula basi anatakiwa akoshe,alafu wewe kuwa kinara wa kufuata sheria hii na umuelezee faida za sheria hiyo kama vile kupunguza mzigo wa vyombo vingi(na sheria nyinginezo)

Lwngo : itamfanya azowee kufuata sheria bila kulazimishwa na mtu hata kaiwa kiongozi.

7. Hakikisha unamuonya na kumrekebisha akiwa peke yake tu,usimkaripie kwenye watu wengi.

Wakati mkiwa peke yenu umuambie kwamba nakugombeza tukiwa wawili tu kwa sababu wangekuwa wengine ungejisikia vizuri ? Lazima atajibu hapana.

Basi hiyo ndio iwe taratibu kila akikosea muite pembeni usiseme kwamba hivyo wanatakiwa wafanyiwe watu wazima hapana,watoto wanahitaji kufanyiwa ili nao waje wafanye hivyo baadae.

Lengo : awe kiongozi anayeepuka kuwarekebisha wenzie kwenye hadhira na kuwafedhehesha.

8. Hakikisha unamuuliza mwanao akupe ufafanuzii juu ya jambo alilosema hata kama unajua maana yake.

Mfano. " baba leo tumemsoma chura shuleni" muulize chura ndio nani ?
Hakikisha anakufafanulia na akishindwa mfahamishe.

Lengo : itamfanya yeye asiwe mtu wa chuki pale atakapokutana na watu wenye kumhoji akiwa kiongozi hapo baadae.

9. Hakikisha unapokosea jambo useme kwamba umekosea mbele ya mwanao usione aibu.

Lengo : itamfanya aone kukosea ni jambo la kawaida na wala sio fedheha kusema umekosea na kuepuka misemo ya " mkubwa hakosei" na atakuwa wempesi kuomba radhi pale anapokosea katika uongozi wake.

10. hakikisha haumtukani tusi lolote lile hata mkiwa peke yenu.

Nikupe siri kwamba hakuna faida hata moja ya tusi unalomtukana mtoto,badala yake itamzidishia misamiati mibaya kichwani mwake.

Lengo : kuepusha viongozi wenye matusi na maneno ya kifedhuli katika jamii.

11. Akiongea na wewe msikilize kwa makini.hii itamfanya na yeye aige umakini huo pale anapoongea na wengine.

Lengo : awe kiongozi mwenye usikivu makini kwa wananchi wake.

12. Panga kununua kitu kisicho muhimu mbele yake kisha ghairisha upange kununua kitu cha muhimu hapo hapo mbele yake.

Mfano. Sema huku anasikia "nataka kununua biskuti ya alfu 5000" kisha ghairisha sema " lakini biskuti ya 5000 nitakula itaisha ila viatu nitavaa muda mrwfu.

Lengo : awe kiongozi anayeepuka matumizi yasiyo na faida na kufanya mambo ya msingi kwa raia wake.

13. Hakikisha unajishusha kwa watu ambao mumewazidi status ya maisha na onesha kuwaheshimu mbele yake.

Kama muna jirani hohehahe basi siku kadhaa mpe pesa aandae chakula huyo jirani kisha nyie na mtoto wenu muende kula kwao yule jirani na mumuambie mtoto wenu kwamba jirani kayualika chakula.

Lengo : itamfanya asiwadharau aliowazidi na wala kudharau wito wao.

14. Usimfundishe kuomba pesa ili baadae asijekuwa kiongozi mpenda pesa na rushwa akawa mvunja sheria namba moja.

Kamwe muepushe na tabia ya kuomba pesa tokea akiwa mdogo,na siku kaikuomba hakikisha ana hoja za msingi.

HITIMISHO
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ukiyafuata na kuyafanya katika maisha yako unapokuwa na mwanao basi kuna asilimia kubwa mtoto huyu akaja kuwa kiongozi bora kabisa.

Lengo ni kufanya mazuri yawe mengi kuliko mabaya na wala hatuwezi kufikia lengo la kuondoa mabaya yote.

Asanteni sana nakaribisha maoni.
 
Upvote 25
Nimeeleza ukiwalea wanao vema bila kuisafisha jamii yote ili ienende kwenye misingi bora unajihangaisha tu.
Kuisafisha jamii yote kila mzazi ana jukumu la kumlea mwanawe kama ambavyo mimi namlea hapo ndio tutaisafisha jamii.

vema tukaandaa na misingi au miongozo ya kuwabana kivitendo wawe na maadili bora.
Mfano katika ushoga tunaona tayari kuna misingi na miongozo inayokataza jambo hilo na kuwabana wahusika.

Lakini bado linaendelea jamii inazidi kuharibika.

Katika ushoga misingi iliyowekwa haijafanya kazi kwa sababu misingi inategemea watu waadifu.

Kama misingi ya kukemea ushoga imefi maana yake tuitengeneze jamii kwanza kwa kulea vizuri vijana wetu.

Rushwa imekemewa na misingi unayoisema lakini ndio imetamalaki,hivyo solution tutengeneze watoto watakaokuja kuwa wazuri hapo baadae ili waweze kuepuka rushwa.

Kwa munaasaba huo maana yake hoja unayosimamia inajigongagonga.
 
ni wazo zuri sana ila unazani ni nani wakumfanya aje kuwa baba au mama, raisi(kiongozi) bora wakati wanaharibikiwa mikononi mwetu
Mkuu samahani unaweza kufafanua swali lako zaidi maana sijalipata vizuri ?
 
Kuisafisha jamii yote kila mzazi ana jukumu la kumlea mwanawe kama ambavyo mimi namlea hapo ndio tutaisafisha jamii.

Mfano katika ushoga tunaona tayari kuna misingi na miongozo inayokataza jambo hilo na kuwabana wahusika.

Lakini bado linaendelea jamii inazidi kuharibika.

Katika ushoga misingi iliyowekwa haijafanya kazi kwa sababu misingi inategemea watu waadifu.

Kama misingi ya kukemea ushoga imefi maana yake tuitengeneze jamii kwanza kwa kulea vizuri vijana wetu.

Rushwa imekemewa na misingi unayoisema lakini ndio imetamalaki,hivyo solution tutengeneze watoto watakaokuja kuwa wazuri hapo baadae ili waweze kuepuka rushwa.

Kwa munaasaba huo maana yake hoja unayosimamia inajigongagonga.
Unajua kama kuna watoto wanaojilea wenyewe?
 
Mimi sijawagusia hao.

Nimegusia watoto wanaolelewa.

Hao wanaojilea unatakiwa uanzishe uzi sasa kuwazungumzia.

Mada yangu inasema "..kuwalea watoto.." na sio "kujilea watoto"

Siwezi kumaliza mambo yote kwwenye mada moja.
 
Mkuu ukiwaacha hao(na kukubali mabadiliko ya sheria muhimu nchini)hauna tofauti na anayesema kwamba yeye atakunywa mchuzi wa maharage tu ila maharage hali.Sababu:Akila maharage tumbo lake lamuunguruma na kumuuma.😝😝😝😝
 
Kutokuwagusia haina maana nimewaacha,hakuna sehemu nimesema nimewaacha.

Isipokuwa uzi wangu haujawalenga hao kwa sababu haikuwa mada yangu.

Hii ya watoto wanaojilea ni mada yako weye sikuianzisha mimi
 
Ili CCM iweze kuwatawala vizuri. Wakipandishiwa makato, sawa. Wakiibiwa kura, sawa tu...
 
Kukwepa hoja au kugoma kuwajumuisha kwenye mjadala haitosaidia.
 
Mkuu huwezi kunilazimisha nimtaje kila mtu kwenye mada ambayo nimeianzisha kwa mtazamo wangu.

Wewe anzisha mada wataje hao watu.😀.

Bila shaka hoja zako za juu zote nimezijibu sasa hivi unataka kuwatia watu ambao hawamo.

Unatakiwa ustiki kwenye mada kabla ya kuwatia unaowataka weye
 
Ili CCM iweze kuwatawala vizuri. Wakipandishiwa makato, sawa. Wakiibiwa kura, sawa tu...
Huyu mtoto tunayemlea akija kukua akawa na maadili mazuri hawezi kuiba kura wala kupandisha makato

Tuanze na watoto kuwalea
 
Habari yako ndugu msomaji.

Katika mambo yanayolalamikiwa na jamii yetu hasa zama hizi basi ni kuwa na viongozi ambao hawana maadili na wala hawafuati sheria mbalimbali za nchi vile zinavyotaka.

Jambo hili sio tatizo dogo kama tunavyolifikiria,na wala sio mazao ya malezi ya mwaka mmoja au miwili iliyopita,bali ni matunda ya muda mrefu ya tabia alizokuzwa nazo.

Sisi kama taifa la watanzania tunalo jukumu la kuhakikisha kwanza tunapata watu wenye kutii sheria bila shuruti,wenye kutii sheria bila ya kutumia nguvu ili watii sheria hizo.

kwa masikitiko tumekuwa na watu ambao hawatii sheria bila ya shuruti.

Kuwa na watu wa aina hii ni hasara na hatari kwa taifa kwa sababu watasababisha kila sheria ambayo itatungwa ionekane haifai kwa sababu ya wao kutofuata sheria za nchi.

Kila sifa ya kiongozi inaanzia utotoni kama vile uadilifu,uungwana,utii,hekima n.k haya yote huanzia utotoni..

Kama tunavyofahamu ya kwamba samaki mkunje angali mbichi,je sisi kama taifa tumejiandaa vipi kuzalisha watoto ambao watakuja kuwa viongozi bora na watiifu hapo baadae ?

Haya ni mambo ya kufanya kwa mwanao au mtoto yeyote ambaye unayo nafasi ya kumlea kuhakikisha kwamba atakuwa mtiifu na kiongozi bora hapo baadae.

1. hakikisha wewe mzazi ama mlezi unakuwa mkweli kwa mtoto katika mambo ambayo hata ufanye vipi basi baadae atakuja kujua ukweli wa mambo hayo.

Mfano.
Huna haja ya kumuambia mtoto kwamba watoto wanaozaliwa wananunuliwa dukani wakati jambo hili atakuja kuujua ukweli hapo baadae.

Kama mtoto anaambiwa kwamba ule ni moto na anatahadharishwa tokea utotoni Basi na jambo hili aambiwe ukweli pia.

Kumdanganya sasa hivi ni kuwaandaa waongo wa baadae,ukimjenga katika ukweli basi atakuwa kiongozi mkweli baadae na ukweli ni sifa muhimu kwa kiongozi.

2. Mshirikishe katika mambo madogo ambayo ungeweza kuamua wewe mwenyewe bila yeye kwa lengo la kumkuza awe mtu wa kushauriana na watu asiwe mtu wa analotaka yeye ndio liwe.

Mfano. Muulize tu hivi mwanangu kununua nguo tatu za sikukuu na kununua mbili na pesa inayobaki tukuwekee akiba kipi bora ?

Lengo ni kumfanya awe mpenda majadiliano,na hawezi kuwa mtu wa aina hiyo mpaka awe amekulia katika hali hiyo.

Lengo : tunahitaji viongozi wapenda majadiliano.

3. anapokosea mrekebishe kwa hoja na usitumie nguvu.hii itamfanya ajifunze kwamba sio kila kosa mtu anatakiwa aadhibiwe bali kuna mambo ya kufahamishwa.

Mfano. Akirudi usiku nyumbani mfahamishe muambie madhara ya kurudi usiku nyumbani badala ya kumpiga.

Lengo : tunataka viongozi wachache wa kuadhibu na kutesa watu.

4. Akiwa ni mkaidi katika jambo ulilomuambia mara nyingi basi muonye kwa adhabu ambayo inaendana na hali yake.

Lengo : Hii itamfanya baadae akiwa kiongozi asimfunge mtu miaka 10 kwa kosa la kuiba kuku.

5. Hakikisha anapokuomba kitu na ahadi ulizomuahidi unamtekelezea.
Mfano. Ukimuahidi kumnunulia baiskeli munulie kweli na umuambie "mwanangu kama sikutekeleza ahadi utaumia" itamfanya aone kwamba kutotekeleza ahadi kunamuumiza aliyeahidiwa.

Lengo : itamfanya yeye awe ni mtu mtekeleza ahadi kwa raia wake

6. Tunga visheria vidogo vidogo hapo nyumbani na wewe uwe wa kwanza kuvifuata visheria hivyo bila kuvunja.

Mfano. Tunga sheria kila mtu chombo anacholia chakula basi anatakiwa akoshe,alafu wewe kuwa kinara wa kufuata sheria hii na umuelezee faida za sheria hiyo kama vile kupunguza mzigo wa vyombo vingi(na sheria nyinginezo)

Lwngo : itamfanya azowee kufuata sheria bila kulazimishwa na mtu hata kaiwa kiongozi.

7. Hakikisha unamuonya na kumrekebisha akiwa peke yake tu,usimkaripie kwenye watu wengi.

Wakati mkiwa peke yenu umuambie kwamba nakugombeza tukiwa wawili tu kwa sababu wangekuwa wengine ungejisikia vizuri ? Lazima atajibu hapana.

Basi hiyo ndio iwe taratibu kila akikosea muite pembeni usiseme kwamba hivyo wanatakiwa wafanyiwe watu wazima hapana,watoto wanahitaji kufanyiwa ili nao waje wafanye hivyo baadae.

Lengo : awe kiongozi anayeepuka kuwarekebisha wenzie kwenye hadhira na kuwafedhehesha.

8. Hakikisha unamuuliza mwanao akupe ufafanuzii juu ya jambo alilosema hata kama unajua maana yake.

Mfano. " baba leo tumemsoma chura shuleni" muulize chura ndio nani ?
Hakikisha anakufafanulia na akishindwa mfahamishe.

Lengo : itamfanya yeye asiwe mtu wa chuki pale atakapokutana na watu wenye kumhoji akiwa kiongozi hapo baadae.

9. Hakikisha unapokosea jambo useme kwamba umekosea mbele ya mwanao usione aibu.

Lengo : itamfanya aone kukosea ni jambo la kawaida na wala sio fedheha kusema umekosea na kuepuka misemo ya " mkubwa hakosei" na atakuwa wempesi kuomba radhi pale anapokosea katika uongozi wake.

10. hakikisha haumtukani tusi lolote lile hata mkiwa peke yenu.

Nikupe siri kwamba hakuna faida hata moja ya tusi unalomtukana mtoto,badala yake itamzidishia misamiati mibaya kichwani mwake.

Lengo : kuepusha viongozi wenye matusi na maneno ya kifedhuli katika jamii.

11. Akiongea na wewe msikilize kwa makini.hii itamfanya na yeye aige umakini huo pale anapoongea na wengine.

Lengo : awe kiongozi mwenye usikivu makini kwa wananchi wake.

12. Panga kununua kitu kisicho muhimu mbele yake kisha ghairisha upange kununua kitu cha muhimu hapo hapo mbele yake.

Mfano. Sema huku anasikia "nataka kununua biskuti ya alfu 5000" kisha ghairisha sema " lakini biskuti ya 5000 nitakula itaisha ila viatu nitavaa muda mrwfu.

Lengo : awe kiongozi anayeepuka matumizi yasiyo na faida na kufanya mambo ya msingi kwa raia wake.

13. Hakikisha unajishusha kwa watu ambao mumewazidi status ya maisha na onesha kuwaheshimu mbele yake.

Kama muna jirani hohehahe basi siku kadhaa mpe pesa aandae chakula huyo jirani kisha nyie na mtoto wenu muende kula kwao yule jirani na mumuambie mtoto wenu kwamba jirani kayualika chakula.

Lengo : itamfanya asiwadharau aliowazidi na wala kudharau wito wao.

14. Usimfundishe kuomba pesa ili baadae asijekuwa kiongozi mpenda pesa na rushwa akawa mvunja sheria namba moja.

Kamwe muepushe na tabia ya kuomba pesa tokea akiwa mdogo,na siku kaikuomba hakikisha ana hoja za msingi.

HITIMISHO
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ukiyafuata na kuyafanya katika maisha yako unapokuwa na mwanao basi kuna asilimia kubwa mtoto huyu akaja kuwa kiongozi bora kabisa.

Lengo ni kufanya mazuri yawe mengi kuliko mabaya na wala hatuwezi kufikia lengo la kuondoa mabaya yote.

Asanteni sana nakaribisha maoni.

Habari yako ndugu msomaji.

Katika mambo yanayolalamikiwa na jamii yetu hasa zama hizi basi ni kuwa na viongozi ambao hawana maadili na wala hawafuati sheria mbalimbali za nchi vile zinavyotaka.

Jambo hili sio tatizo dogo kama tunavyolifikiria,na wala sio mazao ya malezi ya mwaka mmoja au miwili iliyopita,bali ni matunda ya muda mrefu ya tabia alizokuzwa nazo.

Sisi kama taifa la watanzania tunalo jukumu la kuhakikisha kwanza tunapata watu wenye kutii sheria bila shuruti,wenye kutii sheria bila ya kutumia nguvu ili watii sheria hizo.

kwa masikitiko tumekuwa na watu ambao hawatii sheria bila ya shuruti.

Kuwa na watu wa aina hii ni hasara na hatari kwa taifa kwa sababu watasababisha kila sheria ambayo itatungwa ionekane haifai kwa sababu ya wao kutofuata sheria za nchi.

Kila sifa ya kiongozi inaanzia utotoni kama vile uadilifu,uungwana,utii,hekima n.k haya yote huanzia utotoni..

Kama tunavyofahamu ya kwamba samaki mkunje angali mbichi,je sisi kama taifa tumejiandaa vipi kuzalisha watoto ambao watakuja kuwa viongozi bora na watiifu hapo baadae ?

Haya ni mambo ya kufanya kwa mwanao au mtoto yeyote ambaye unayo nafasi ya kumlea kuhakikisha kwamba atakuwa mtiifu na kiongozi bora hapo baadae.

1. hakikisha wewe mzazi ama mlezi unakuwa mkweli kwa mtoto katika mambo ambayo hata ufanye vipi basi baadae atakuja kujua ukweli wa mambo hayo.

Mfano.
Huna haja ya kumuambia mtoto kwamba watoto wanaozaliwa wananunuliwa dukani wakati jambo hili atakuja kuujua ukweli hapo baadae.

Kama mtoto anaambiwa kwamba ule ni moto na anatahadharishwa tokea utotoni Basi na jambo hili aambiwe ukweli pia.

Kumdanganya sasa hivi ni kuwaandaa waongo wa baadae,ukimjenga katika ukweli basi atakuwa kiongozi mkweli baadae na ukweli ni sifa muhimu kwa kiongozi.

2. Mshirikishe katika mambo madogo ambayo ungeweza kuamua wewe mwenyewe bila yeye kwa lengo la kumkuza awe mtu wa kushauriana na watu asiwe mtu wa analotaka yeye ndio liwe.

Mfano. Muulize tu hivi mwanangu kununua nguo tatu za sikukuu na kununua mbili na pesa inayobaki tukuwekee akiba kipi bora ?

Lengo ni kumfanya awe mpenda majadiliano,na hawezi kuwa mtu wa aina hiyo mpaka awe amekulia katika hali hiyo.

Lengo : tunahitaji viongozi wapenda majadiliano.

3. anapokosea mrekebishe kwa hoja na usitumie nguvu.hii itamfanya ajifunze kwamba sio kila kosa mtu anatakiwa aadhibiwe bali kuna mambo ya kufahamishwa.

Mfano. Akirudi usiku nyumbani mfahamishe muambie madhara ya kurudi usiku nyumbani badala ya kumpiga.

Lengo : tunataka viongozi wachache wa kuadhibu na kutesa watu.

4. Akiwa ni mkaidi katika jambo ulilomuambia mara nyingi basi muonye kwa adhabu ambayo inaendana na hali yake.

Lengo : Hii itamfanya baadae akiwa kiongozi asimfunge mtu miaka 10 kwa kosa la kuiba kuku.

5. Hakikisha anapokuomba kitu na ahadi ulizomuahidi unamtekelezea.
Mfano. Ukimuahidi kumnunulia baiskeli munulie kweli na umuambie "mwanangu kama sikutekeleza ahadi utaumia" itamfanya aone kwamba kutotekeleza ahadi kunamuumiza aliyeahidiwa.

Lengo : itamfanya yeye awe ni mtu mtekeleza ahadi kwa raia wake

6. Tunga visheria vidogo vidogo hapo nyumbani na wewe uwe wa kwanza kuvifuata visheria hivyo bila kuvunja.

Mfano. Tunga sheria kila mtu chombo anacholia chakula basi anatakiwa akoshe,alafu wewe kuwa kinara wa kufuata sheria hii na umuelezee faida za sheria hiyo kama vile kupunguza mzigo wa vyombo vingi(na sheria nyinginezo)

Lwngo : itamfanya azowee kufuata sheria bila kulazimishwa na mtu hata kaiwa kiongozi.

7. Hakikisha unamuonya na kumrekebisha akiwa peke yake tu,usimkaripie kwenye watu wengi.

Wakati mkiwa peke yenu umuambie kwamba nakugombeza tukiwa wawili tu kwa sababu wangekuwa wengine ungejisikia vizuri ? Lazima atajibu hapana.

Basi hiyo ndio iwe taratibu kila akikosea muite pembeni usiseme kwamba hivyo wanatakiwa wafanyiwe watu wazima hapana,watoto wanahitaji kufanyiwa ili nao waje wafanye hivyo baadae.

Lengo : awe kiongozi anayeepuka kuwarekebisha wenzie kwenye hadhira na kuwafedhehesha.

8. Hakikisha unamuuliza mwanao akupe ufafanuzii juu ya jambo alilosema hata kama unajua maana yake.

Mfano. " baba leo tumemsoma chura shuleni" muulize chura ndio nani ?
Hakikisha anakufafanulia na akishindwa mfahamishe.

Lengo : itamfanya yeye asiwe mtu wa chuki pale atakapokutana na watu wenye kumhoji akiwa kiongozi hapo baadae.

9. Hakikisha unapokosea jambo useme kwamba umekosea mbele ya mwanao usione aibu.

Lengo : itamfanya aone kukosea ni jambo la kawaida na wala sio fedheha kusema umekosea na kuepuka misemo ya " mkubwa hakosei" na atakuwa wempesi kuomba radhi pale anapokosea katika uongozi wake.

10. hakikisha haumtukani tusi lolote lile hata mkiwa peke yenu.

Nikupe siri kwamba hakuna faida hata moja ya tusi unalomtukana mtoto,badala yake itamzidishia misamiati mibaya kichwani mwake.

Lengo : kuepusha viongozi wenye matusi na maneno ya kifedhuli katika jamii.

11. Akiongea na wewe msikilize kwa makini.hii itamfanya na yeye aige umakini huo pale anapoongea na wengine.

Lengo : awe kiongozi mwenye usikivu makini kwa wananchi wake.

12. Panga kununua kitu kisicho muhimu mbele yake kisha ghairisha upange kununua kitu cha muhimu hapo hapo mbele yake.

Mfano. Sema huku anasikia "nataka kununua biskuti ya alfu 5000" kisha ghairisha sema " lakini biskuti ya 5000 nitakula itaisha ila viatu nitavaa muda mrwfu.

Lengo : awe kiongozi anayeepuka matumizi yasiyo na faida na kufanya mambo ya msingi kwa raia wake.

13. Hakikisha unajishusha kwa watu ambao mumewazidi status ya maisha na onesha kuwaheshimu mbele yake.

Kama muna jirani hohehahe basi siku kadhaa mpe pesa aandae chakula huyo jirani kisha nyie na mtoto wenu muende kula kwao yule jirani na mumuambie mtoto wenu kwamba jirani kayualika chakula.

Lengo : itamfanya asiwadharau aliowazidi na wala kudharau wito wao.

14. Usimfundishe kuomba pesa ili baadae asijekuwa kiongozi mpenda pesa na rushwa akawa mvunja sheria namba moja.

Kamwe muepushe na tabia ya kuomba pesa tokea akiwa mdogo,na siku kaikuomba hakikisha ana hoja za msingi.

HITIMISHO
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ukiyafuata na kuyafanya katika maisha yako unapokuwa na mwanao basi kuna asilimia kubwa mtoto huyu akaja kuwa kiongozi bora kabisa.

Lengo ni kufanya mazuri yawe mengi kuliko mabaya na wala hatuwezi kufikia lengo la kuondoa mabaya yote.

Asanteni sana nakaribisha maoni.
Good analysis lkn inahtaj mda san
 
Ni wazo zuri sana ila unadhani ni nani wakumfanya aje kuwa baba au mama, raisi (kiongozi) bora wakati wanaharibikiwa mikononi mwetu
Mkuu kwanza anayetakiwa awe baba bora ni yule ambaye anaishi vizuri na jamii.

Lazima kufanyike uchunguzi kuhakikisha huyu baba mtarajiwa anaweza kuishi na jamii vizuri ?

Kama anaweza kuishi na jamii vizuri bbasi bila shaka ataweza kuishi na mke ambae atakuwa mama watoto wakw hapo baadae.

Hali kadhalika kwa mwanamke pia anatakiwa awe hivyo hivyo.

Kama sijajibu unavyotaka naomba uweke vizuri swali lako mkuu
 
Back
Top Bottom