We nae tutolee huu ujinga wako na mapovu Kila comment bwana.
Kila siku mnakuja na jambo hilo hilo la uislamu unachafuliwa. Kwa kitu kipi cha maana mlichonacho hadi dini yenu ichafuliwe?
Ni swala la kuamini (Imani )tu? Yani mtu akibadili dini na kuwa muislamu,hiyo itaniathiri vipi Mimi nisiye muislamu?
Mfano Mimi nimekaa Zanzibar ambako Kuna uislamu zaidi ya 90% ,hiyo Ina athari Gani kwangu nisiye muislamu? Mbona maisha yanaenda vile vile ?
Huu udwanzi wa kulalamika "uislamu unachafuliwa " mnatuchosha. Huo uislamu una nini cha maana hadi upigwe vita enyi wanafiki?
Ndugu kila community ina viongozi wao inaoqasikiliza na kuwaamini.
Lkn mwisho wa siku kwa kuangalia matukio hata asie na macho huona.
Bila ya kukuchosha soma waraka wa kiongozi wa waislam nchini alioutoa miezi michache iliyopita akiwatahadharisha serikali dhidi ya kikundi hiki cha waleta taharuki kwa nchi wakikingwa na baadhi ya watendaji wasio waaminifu. Ambao wapo na wanafanya maamuzi sawa na matamanio ya nafsi zao kwa mgongo na kwa jina la serikali ya JMT
Ni watumishi immoral, wavuta bangi waliojificha ktk vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Waraka
FITNA!
Propaganda mpya dhidi ya Waislamu.
Kundi laundwa kuzungumzia ugaidi
SERIKALI imetakiwa kuzingatia zaidi maslahi ya Taifa katika kuiendea na kuishughulikia dhana ya ugaidi nchini, kwani zimeanza kuibuka propaganda mpya za ugaidi na kunasibishwa na Waislamu.
Wito huo umetolewa na Sheikh Ponda Issa Ponda, akiongea na Gazeti la An nuur, kufuatia hivi karibuni kusambaa kwa makala katika mitandao ya kijamii iliyoandikwa na mwandishi aliyejitaja kwa jina la Lugete Mussa Lugete.
Mwandishi huyo pia ametangaza kuanzishwa Group maalum la kuandika makala zinazozungumzia ugaidi wa Waislamu, pamoja na yeye amewataja waandishi wengine katika group hilo kuwa ni Lugete Gulu Maester, Mpoki Buyah na Mwalimu Mayuni Joseph.
Tayari kazi ya uandishi imeanza na kwa mujibu wa makala hizo vyanzo vyao vya habari ni Intelijensia ya Serikali za Tanzania, Msumbiji, Marekani na vyombo vya Ulinzi na Usalama. Vyanzo vingine ni Dr. John K Kingu na Profesa Pedro C. Vicent.
Sheikh Ponda, alisema makala yake hiyo ameipa anuani ya Operesheni Mkuranga, Kibiti, Rufiji, Mkiru, na hatma ya ugaidi, ujambazi na upotoshaji wa Dini ya Kiislamu, Cabo Delgado Msumbiji.
Moja ya suala linalojitokeza katika makala hiyo ni Uislamu na ugaidi,
ingawa mwandishi anadai kuwa magaidi ndio wanao husisha Dini ya Uislamu na ugaidi lakini kwa hakika yeye (Mwandishi) ndiye anayehusisha Uislamu na Ugaidi.
Tunawashauri viongozi wazingatie zaidi maslahi ya Taifa katika suala hili la ugaidi, kwani sasa zimeanza kuibuka propaganda mpya za ugaidi zinazo wanasibisha Waislamu. Amesema Sheikh Ponda.
Alisema, katika hili anaikumbusha Serikali kwamba, Taifa la Tanzania limejengwa juu misingi mitatu ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama na mpango huo ni wa kitaalamu kwa ustawi wa Taifa na watu wake.
Sheikh Ponda ameeleza kuwa mwaka 2002, wakati wa mchakato wa Sheria ya Ugaidi, Wabunge walisema maneno mazito Bungeni, na kufafanua kuwa Tanzania hakuna ugaidi na Sheria hiyo ya Ugaidi inawalenga zaidi raia Waislamu.
Akasema, hivi sasa matokeo ya utekelezaji wa Sheria hiyo yanaonekana wazi kwani wanaokamatwa na kutuhumiwa kwa ugaidi wengi wao ni Masheikh na Waislamu wa kawaida.
Lakini la kusikitisha zaidi ni kwamba hata kesi zake mahakamani zinakwama kusikilizwa na Waislamu wakabaki wafungwa mahabusu wa muda mrefu.
Akizungumzia kuhusu makala hayo Sheikh Ponda, anasema ingawa mwandishi anadai kuwa magaidi ndio wanao husisha Dini ya Uislamu na ugaidi, lakini makala hiyo ipo wazi kuwa yeye ndiye anayehusisha Uislamu na ugaidi.
Akifafanua Sheikh Ponda, amesema Mwandishi wa Makala hiyo amewataja Waislamu wasomi wa Vyuo vya Kiislamu kama Magaidi huku Misikiti, Madrasa, Asasi kama vile vituo vya Yatima na Shule za Kiislamu amevitaja kuwa ni vituo vya Kigaidi.
Aidha amesema, katika makala yake hiyo ameyataja mataifa kadhaa aliyodai kuwa yanayoelekea kusambaratika kutokana na hicho alichokiita ni ugaidi.
Sheikh Ponda amemtanabahisha mwandishi huyo kuwa uandishi wake unatakiwa azingatie maamuzi yaliyotolewa na Mahakama kuhusu suala hili zito linalohusu uhai wa watu na mustakbali wa Taifa, badala ya kuja na huu uchambuzi bandia wa taarifa za Intelijensia.
XXXX
Maoni yangu
Kwa kuhitimisha kama kweli serikali ya inataka ikubalike kwa raia. Basi wamrejeshe mwandishi Azori huko aliko. Kwani ndie mwenye taarifa za kiuchunguzi za hakika za ugaidi wa mkwiru Kibiti.