Njia ya Kibiti kwenda kwenye laana ya Cabo Delgado

Vikundi vingi vya kigaidi/waasi hutumia silaha maarfu ak-47 hata hapo mozambique ni mwendo wa ak-47 kwa hiyo unataka kutuaminisha kua USA siku hizi na yeye n mzalishaji na msambazaji wa silaha hiyo?

Mbona nchi nyingi zinatengeneza hizo silaha kwa kupewa kibali na wengine hata hawajapata kibali wanajifanyia kwa wizi
 
Ukitaka kupoka utajiri wa sehemu Bila kulipa Kodi au gawio halisi Kwa wazawa waanzishie vurugu ya aina yoyote waache wakihangaika kupigana wewe unajichotea tuu, Hilo eneo la Kaskazin la Msumbiji Lina utajiri sana tena sana. Ko lazima liwe kama DRC tuu yaani hakuna kutulia watu wanajibebea tuu wanasepa zao Watawaletea magaidi wa kidini wa mchongo, mara vikundi vya kupigana uhuru ndani ya nchi huru kama M23 yaani taflani tuu. Na viongozi wetu hawanamaarifa Wala nguvu ya kututoa tulipo ndio changamoto zaidi. Ona Libya ilivopauka saa hivo waliwangilia na hoja ya demokrasia wameishia kuvuruga nchi na jamii Kwa ujumla na Mambo ndio hayaendi tena nchi ishagawanyika. Na uzuri Hawa wezi wa rasilimali za hili bara wanatujua nje ndani ndio maana wakija na mission Yao hawafeli tunaishia kuumiza wenyewe Kwa wenyewe wanatuangalia na vimisaada mbuzi kujifanya wanatutakia mema.
 
Nime uliza kuhusu Usa na sio masuala ya nchi nyingi je usa ana kibali cha kuzalisha hizo siraha na kuzisambaza?

Si lazima awe nacho kuna mafia nyingi kila mahali zinaweza kutengeneza bila kibali. hata wewe unaweza ukaitengeneza , ingia You tube wameonyesha vizuri sana , uwe na material tu na mashine za uchongaji .

Kule Pakistani na Afghanistani kila mahali wanazitengeneza wenyewe mitaani


View: https://www.youtube.com/watch?v=f58bfGlqceo
 
Pale Kibiti waliona nini ? Hebu dadavua mkuu
 
Yeah uko sahihi.
Ni aina ya watu wale wanaopoteza siku nzima kubishana habari za simba na yanga.
Hata Ulaya ugaidi na vita au mapigani yapo sema vita zao ziko strategic na huwa zina sababu maalumu za kushindana kiuchumi.
Wao hizi mambo walishazipita mkuu, vita hizi za vikundo vya kigaidi na vita za wenyewe kwa wenyewe washapigana sana.
Wakajua udhaifu wao, wakaurekebisha.
Sasa sisi daah hadi huruma aisee, tukechelewa kujitambua.
 
Wao hizi mambo walishazipita mkuu, vita hizi za vikundo vya kigaidi na vita za wenyewe kwa wenyewe washapigana sana.
Wakajua udhaifu wao, wakaurekebisha.
Sasa sisi daah hadi huruma aisee, tukechelewa kujitambua.
Yeah kwa sasa hawatumii vita za kutumia miguvu tena,wanaingia tu maabara kisha wanatuma kirusi kama cha covid basi kazi imeisha
 
Kaka huwezi kutibu tatizo lako kwa kunyoshea vidole watu.

Fanya hivi unataka kufanya tukio la ugaidi. Una vijana wawili Msabato na Muislamu, yupi ni rahisi kumpenyezea agenda yako akafanya kati ya hao wawili?

Siku mtayoanza kutumia muda wenu wa mahubiri kuwasihi vijana wasishawishike na haya makundi ya kigaidi iwe msikitini au kwenye mihadhara badala ya kuwasimanga Makafiri ndio itakua mwanzo wa mwisho wa kuhusishwa uislamu na ugaidi.

Niambie wewe mara ya mwisho lini umemsikia kiongozi wako wa dini iwe msikiti au madrasa anawaasa watoto na vijana kuhusu haya makundi?

Tatizo halitibiwi kwa kunyoshea watu vidole. Kanisa katoliki linakabiliwa na kashfa ya makasisi wake kulawiti watoto. Wanajitahidi kujisafisha kwa namna wanavyoweza lakini hatujawahi kusikia wakitajwa fulani ndio chanzo.

Mwisho unahisi ni kwanini ni rahisi kumshawishi muislamu kufanya Ugaidi kuliko Msabato, Mkatoliki, au hata wa Mwamposa?
 
Mna uhakika gani hao ni waislamu? Na wanamtumikia nani? Vazi ndio linawaaminisha wao ni waislamu?

Ndugu zetu wa palestina wanauawa kikatili, tena kwenye land yao na hatuwasikii mkisema makafiri ya kizayuni ni MAGAIDI, Nyie watu wa ajabu sanaa.
Kumbe una ndugu Palestine
 
Weka clip hapa tuone kama ni yeye, na waliomuuwa kama ni hamas!
Mzee ulikua mahabusu au? Pitia huu uzi utaziona hizo video.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…