Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Unataka kweli kuacha?? Peke yako huwezi ni lazima upate nguvu kutoka nje. Yaani nguvu za Mungu. Hebu fungua hiyo picha uliyoweka halafu isome kwa muda kidogo. Wadhani huyo mwanamke anakunywa kwa kupenda?
Kuna nguvu inamsukuma kuzinywa. Hata ustaarab wake kesha nyang'anywa na hiyo pombe. Si chupa zote ni zake?? Kwanini asiziweke chini akanywa taratiibu?
Mpe Yesu maisha yako, ndiye dawa
 
Dawa ya kuacha kufurisika kwako hata mia usipate.ndiyo utaacha kama bado zinaingiya kuacha hapo ngumu kata maji tuuu.
 
Too much of anything is harmful.

From my experience: Everything IN LIFE should be done in moderation.

Mimi ni mpenzi wa beer (mara nyingi Heineken). Lakini baada ya mda niliamua kupunguza. Si kwamba sinywi au nilipata mhadhara yoyote. NO. Nikiwa na marafiki napiga monde vizuri tuu. Lakini naweza kumaliza hata wiki sijaenda bar. Au naweza kwenda bar nikanywa bia mbili au tatu nikarudi zangu nyumbani. Ni maamuzi tuu. Kikubwa ni kujielewa.

Again ushauri kwa mleta mada. Si lazima uache Pombe. Lakini unaweza kunywa in moderation na ukawa powa tuu.

Ni kama sigara. Nina Rafiki yangu anavuta sigara for more than thirty years now. Lakini mpaka umuone anavuta ....ni shughuli. Na anaweza akamaliza hata mwezi hajavuta. Ni swala la ku-control mind zetu. Maana hata juice, soda, nk ukinywa in large quantity lazima vitakudhuru tuu.
Ahsante "pacha" wangu Masanja tulijiunga JF siku moja yaani 1/8/2007
 
Unataka kweli kuacha?? Peke yako huwezi ni lazima upate nguvu kutoka nje. Yaani nguvu za Mungu. Hebu fungua hiyo picha uliyoweka halafu isome kwa muda kidogo. Wadhani huyo mwanamke anakunywa kwa kupenda?
Kuna nguvu inamsukuma kuzinywa. Hata ustaarab wake kesha nyang'anywa na hiyo pombe. Si chupa zote ni zake?? Kwanini asiziweke chini akanywa taratiibu?
Mpe Yesu maisha yako, ndiye dawa
Amen.
 
Mkuu umepata hiyo dawa. Nilipo hapa kuna mtalaam anatoa hii dawa ambayo ukiinusa tu utapa kichefu chefu cha ajabu kila unapohisi harufu ya pombe yoyote. Kichefuchefu hiki kinapelekea kutapika kusikokwisha mpaka kuachia ngazi. Wengi wameshaachia ngazi na hawakurudia tena pombe. Tuwasiliane.
0756361909 tuwasiliane
 
Neema ya Mungu itatosha kukufungua kutoka NIRA ya ulevi. Kimbilia kwa Mungu Tuuuuuuuu
 
eaea09928a4878b262cd1e79ea3e9065.jpg

je unataka kuacha pombe lakini unashindwa? basi angalia jinsi ya kupata msaada. siku hizi kuna dawa zimeingia kwenye soko la dawa ambazo zinaweza kukusaidia kuacha pombe, dawa hizi hazikuachishi pombe lakini zinaleta hali ambayo utajikuta hupendi kunywa pombe yaani ukinywa huoni raha tena.

matibabu haya yanatakiwa yaende na njia zingine za kucha pombe kama ushauri, kuamua moyoni kuacha, kuomba msaada kwa marafiki, kukaa mbali na wanywaji, kuepuka kukutana bar na rafiki zako na kadhalika.
zifuatazo ni dawa husika za kuacha pombe

[emoji117] disulfiram; hii ni dawa ya kwanza kabisa iliyogunduliwa ya kuwafanywa watu kuacha pombe, inafanya kazi kwa kuzuia mwili kuondoa pombe mwilini baada ya kunywa na matokeo yake mtu huweza kukaa na hang over kwa muda wa mpaka wiki mbili.

Mtu hujisikia kichwa kuuma, kutapika, kuishiwa nguvu, kuchanganyikiwa, kutokwa jasho sana, kupumua kwa shida, na kushindwa kuona vizuri kila anapokunywa. mtumiaji hutapaika sana kama mtu aliyekunywa sumu kila akigusa pombe. hali hii humfanya mtu aiogope pombe kabisa.
fcbdb52c1e5e08cf572a12cedca670ab.jpg

[emoji117]naltrexone; hii ni dawa ambayo inafanya kazi kwenye ubongo, kitaalamu kuna sehemu ya ubongo ambayo hupata raha mtu anavyoendelea kunywa pombe...dawa hii huzuia sehemu hiyo ya raha na kumfanya mtu asione raha yeyote kunywa pombe.

Watu wengi hunywa pombe sababu kuna raha wanaipata wakati wanakunywa pombe hivyo wakiikosa raha hii hulazimika kuacha. dawa hii haina madhara ya kutapika kama ile ya mwanzo, dawa hii huchomwa kama sindano kwa mnywaji kila baada ya muda fulani mpaka atakapoacha kabisa.
a39400b7a103a1ad20bff01828819fc6.jpg

[emoji117] acamprosate; mtu ambaye amezoea pombe hawezi kuacha ghafla kwani anakua ameshaizoea mwilini kitaalamu kama addiction hivyo akiacha ghafla hupata matatizo ambayo yanaitwa kitaalamu kama withdraw syndrome ambayo mtu huapata dalili za wasiwasi, kutetemeka,kukosa usingizi, na kutokwa na jasho, sasa dawa hii humsaidia huyu mtumiaji arudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya kuacha pombe bila kupata hayo madhara niliyotaja.
080adf8f068e6551d90f66e7d4c3747d.jpg

mwisho; dawa hizi hupewa kwa watu tu ambao wako tayari kuacha pombe na mgonjwa asiwekewe kwenye pombe yake au kunyweshwa bila mwenyewe kujua kwani hiatamsaidia. kabla ya kuanza dozi ni vizuri daktari aliyekaribu na mgonjwa afahamu ili kama madahara ya dawa yakiwa makubwa aweze kumsaidia muhusika.
Wakati unaleta hii mada umewafikiria wafanyakaz wa Kampuni za bia na familia zao? Umewafikiria wamiliki wa bar na grocery na familia zao? Umewafikiria mabaamedi na familia zao? Umeufikiria uchumi wa nchi yetu? Umewafikiria wakulima wa ngano? Umewafikiria madereva wa malori ya pombe na ngano? Uwe na huruma kijana...unadhani tukiacha pombe hao watu wataishije?
 
Hii dawa ya pili nimeikubali...ngoja nkadungwe sindano, Savannah bye bye
 
Back
Top Bottom