Poleni kwa miangaiko ya wiki na pilika za hapa na pale!
Naombeni msaada tiba ya kumwachisha mtu kunywa pombe.
Hili tatizo la ulevi analo Baba mzazi ambapo akilewa tu , Mama anakosa amani kwa sababu anakuwa anapigwa tu, pasipo na sababu za msingi .
Lakini asipo kunywa pombe anakuwa ni mtu mwenye busara tu. Hivi karibuni amekuwa akilewa mfululizo kiasi ambacho vurugu nyumbani haziishi.
Kwa hyo kutokana na hili tatizo linapelekea Mama kukosa amani pale nyumbani, mpaka ndugu wa mama wamekuja juu kutaka kumwondoa dada yao pale nyumbani!
Nilishasikia tiba ya kumwachisha mtu pombe ni kumchanyia mkojo wake mwenyewe kwenye pombe!
Hili bado sijalifanyia kazi kwa kukosa ushuhuda thabiti kwa watu waliojaribu au kutibiwa!
Naomba mwenye kufahamu tiba yeyote ile au mwenye ushuhuda kwa hiyo tiba ya kumwekea mkojo wake kwenye pombe! Atakuwa amenipatia mwangaza mzuri!