Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Kuna mwanamke alikuwa anapigwa kila siku na mme wake, na kipigo haswa mpaka kwenda kujitibu majeraha hospital.Maji tena? Yanahusikaje?
Dr akawa kila wakati anamtibu na mama kila wakati alikuwa anamwambia sababu yote ni pombe.
Mara ya tatu Dr akamwambia sintakupa dawa yoyote ila ukifika nyumbani andaa maji yaweke karibu yako.
Mme wako akigonga mlango tu piga fundo moja la maji na usimeze yawe mdomoni tu
Na kila wakati fanya hivyo kwa wiki moja halafu uje kuniona
Baada ya wiki alikwenda kumuona Dr akiwa mzima wa afya na hajapigwa wiki nzima
Alipouliza kulikoni sijapigwa wiki nzima
Dr akamwambia una mdomo mrefu na MAJI ndio tiba yako
Hapo vipi umeelewa HEKMA ya Dr?