Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Habarini za wakati huu wote humu
Mimi kila mwaka najiwekea malengo za kufanya jambo/mambo flani au kuacha vitu/tabia ambazo zinanirudisha nyuma kimaendeleo.

Mwaka unaoisha nilipanga sichepuki na nikaweka mikakati namna ya kupambana na hilo. Nashukuru Mungu nimeweza hilo.

Mwaka huu nahitaji kuacha pombe, japo nimepunguza kwa kiwango kikubwa. Maana mwanzoni sikuweza kulala bila kunywa ila kwa sasa naweza bila tatizo japo kuna watu imebidi nikosane nao ili nifikie hatua hiyo.

Ishu inayonitatiza ni kuwa nahisi nisipokuwa makini ntarudi kulekule kwa sababu hamu ya kunywa haijaisha ila najikaza sana.

Nachowaomba ni kujua, je hakuna dawa ya kumfanya mtu aione kama uchafu flani hivi ili nisiwe naitamani? Nilishawahi kusikia watu wanaongea kuwa ipo lakini sina ushahidi kama kweli ipo. Msaada tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilijaribu sana ila niliporudia ujinga huo nikajikuta naongeza mara 2 zaidi ya juzi. Niliwahi kuacha pombe for 2 yrs. Niliporudia nikawa chapombe.
Ila, tangu nikutane na huyu Mwanamume aitwaye Yesu Kristo Mnazareti. Akaniokoa, leo ni zaidi ya miaka 39 sijawahi, nasema tena; Sijawahi hata kuitamani tena. Maisha yamekuwa Swafiii kama ulaya.
Jaribu njia/dawa hiyo. Yesu Kristo Mnazareti. Matayo 11:28 Njooni kwangu ninyi nyote mnaosumbuka na kelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Kwisha
 
Mzee mimi niliwah kusikia dawa hiyo ipo Lakini sikumbuki wapi!!!! Tajitahid kesho kumuuliza jamaa yangu mmoja Weka namba yako ya simu na ulipo kesho takugongea uzi kukujulisha
Kila jambo lina mwanzo na mwisho maadamu umeonyesha nia ya kutaka kuacha nina imani utaacha ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona babu unatafuta sadaka hapo kanisani kwako ziongezeke!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu niliweka naziri hiyo nikashindwa kuacha pombe nikaweka tena ikifika December 23 nitaacha nashukuru nimeweza ila ndoto za ajabu aziniishi ila potelea mbali.ata pesa kwa siku chache zile za pombe nimeziona moto huhu mwaka mwakani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…