Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Mkuu ukiugua ugonjwa na daktari akakwambia ukinywa pombe glas 1 unakufa, naamini ungeacha kabisa.
Huo ni mchezo wa akili tu kichwani maana unashindana na nafsi yako ovu, ukiamua kuacha leo hii milele unaacha bila dawa ila ukichukulia hiyo hali ni kama ugonjwa kuacha dawa lazima utalala hapo milele na maendeleo utayaona kwa wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Revisit your own consciousness,evaluate yourself,dont deny what you are,look at what consequences you fall a victim into and re-evaluate them,MAKE a conscious DECISİON,determine and walk out free and safe-either with alcohol or without alcohol,Your choice is what you call DECISİON!!
-No medicine but YOU!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa unayo mwenyewe Hakuna Dawa kama maamuz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani huwa unashikiwa glas? Dawa ni kuamua tu kuacha na uende ukaombewe hilo pepo likutoke huku ukikaa mbali na maeneo ya bar


Sent using Jamii Forums mobile app
 
DAWA YA KUACHA POMBE NI YESU, YESU, YESU. MPOKEE YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO HAPO MAPEPO YOOOOTE YA ULEVI YATAONDOKA YENYEWE.
KAA MBALI NA MARAFIKI WALEVI HAPO NAYO ITAKUSAIDIA.
 
Nitakuja Inbox

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni mkristu mfungie kanisani, kama ni mwislamu mfungie msikitini na kama hayumo katika hizo dini mbili basi mwache alale kwenye kilabu cha pombe akizinduka amay be ataacha!
Yapo makanisa mengine pombe ziko humohumo.
 
Wakuu dawa ya kuacha pombe ipo. Wenye uhitaji mpo mikoa gani.
Ipo pia ya kuacha bangi na sigara
 
KUACHA POMBE

Watu wengi wamefanikiwa kuacha pombe kwa juhudi zao

wenyewe na wengine kupitia msaada wa wataalamu mbalimbali.

Kuna watu wanaojiunga ili kusaidiana katika kuacha pombe.

Moja ya kikundi maarufu ambacho kimeenea duniani kinaitwa

alcoholics anonymous (AA). Katika kikundi hiki watu

wanaotaka kuacha pombe hukutana na kubadilishana uzoefu na

mbinu za kuacha pombe. Kuacha pombe linaweza kuwa jambo

gumu hivyo inashauriwa kulifanya taratibu. Unaanza kwa

kupunguza kiasi unachokunywa taratibu mpaka unafikia kuacha

kabisa. Usikatishwe tamaa ukiona unarudi nyuma mara kwa

mara kwani ni jambo la kawaida katika kuacha tabia au zoea

lolote lile. Ukishindwa kuacha basi unaweza kupunguza kwani

unywaji kiasi huwa hauna madhara isipokuwa ukiwa mjamzito

au ukishauriwa na mtalaamu wa afya.

Zifuatazo ni mbinu mbalimbali ambazo zinatumika kupunguza

au kuacha kabisa unywaji wa pombe.

1. Tafuta kinywaji mbadala wa pombe kama vile chai au

kahawa.

44

2. Tafuta vitu mbadala vya kufanya kwa wakati ambao unakuwa

unakunywa pombe kama vile kusoma vitabu, kuangalia filamu,

kushiriki katika michezo au mazoezi.

3. Tumia pesa ambazo unaziokoa kutoka kwenye pombe kwa

kujiburudisha kama vile kula vizuri au kununua vifaa vya

nyumbani. Hii itakusaidia sana katika kuona umuhimu wa

kuacha pombe.

4. Jiwekee mkakati kabla ya kwenda kunywa kuhusu kiasi

utakachoenda kunywa na pesa utakayotumia. Usibebe pesa zaidi

ya uliyopanga kutumia.

5. Tumia glasi ndogo wakati wa kunywa na tumia vinywaji

vyenye nguvu ndogo. Utafiti unaonyesha watu hunywa zaidi

wakitumia glasi kubwa kuliko wakitumia glasi ndogo.

6. Kunywa maji kabla hujaanza kunywa pombe. Pia

unavyokuwa unakunywa pombe hakikisha unakuwa na maji ya

kunywa karibu na uyatumie mara kwa mara.

7. Jaribu kuepuka vishawishi vya kunywa. Watu wengi huwa

tunashawishika kunywa kwenye mazingira fulani au tukiwa na

watu fulani. Unachotakiwa ni kugundua ni vishawishi vipi

hukufanya unywe na uanze kuviepuka.

8. Kuwa na msimamo. Watu wengi ambao hujaribu kuacha

pombe hukutana na wakati mgumu wanapopata ofa toka kwa

marafiki. Njia sahihi ni kukataa bila kusitasita. Kusitasita

kunaweza kukufanya uteteleke katika msimamo wako.

45

Ni vizuri ukatafuta sababu ya kukataa ofa mapema kabla hata ya

kukutana na ofa. Mfano, unaweza ukasema sinywi au siongezi

pombe nyingine kwa sababu nataka kupunguza uzito au sababu

nyingine ambayo utakuwa umeitengeneza kama ulinzi wako.

9. Epuka kunywa pombe ukiwa na kiu au njaa. Hii inapunguza

kiasi cha pombe ambacho kitaingia kwenye damu hivyo

utapunguza madhara yake. Pia inasaidia kupunguza kasi ya mtu

kuwa mraibu/teja wa pombe.

10. Hakikisha ndugu na marafiki wanajua kwamba umedhamiria

kuacha pombe. Hii itasaidia kupata msaada kutoka kwao pia

hawatakuwa wanakushawishi sana unywe. Pia hili linaweza

kukusaidia kupata marafiki wapya kwani changamoto mojawapo

ya kuacha pombe ni kupoteza marafiki.

11. Kama unakunywa kwa kutumia glasi hakikisha kinywaji

kimeisha kabisa ndo uongeze tena. Hii itakusaidia kujua ni kiasi

gani cha pombe ulichotumia.

Kuna watu ambao mbinu hizo hapo juu zimeshindwa kabisa

kuwasaidia kuacha pombe. Msaada pekee ambao hubaki kwa

watu hao ni kutumia dawa. Mara nyingi watu hawa ni wale

ambao wanakuwa wametawaliwa sana na pombe na hupata

madhara mara waachapo. Matibabu ya watu hawa hufuata hatua

tatu muhimu.

1. Hatua ya kwanza ni kutibu madhara yatokanayo na kuacha

pombe. Tumeshaona baadhi ya dawa zitumikazo kutibu madhara

yatokanayo na kuacha pombe huko juu.

46

2. Hatua ya pili ni kumsaidia mtu huyu kutotumia pombe. Hatua

hii ndio mara nyingi hutumia dawa. Tutaona dawa hizo hivi

punde. Kumbuka kwamba dawa za kumsaidia mtu kutotumia

pombe ni tofauti na zile za kutibu madhara yatokanayo na

kuacha pombe.

3. Hatua ya tatu ni kumsaidia mtu huyu asirudie tena kunywa

pombe.

Kuna dawa nyingi ambazo hutumika kusaidia watu kuacha

pombe. Baadhi ya dawa hizo ni kama disulfiram, fluoxetine

ambayo kwa kawaida ni dawa ya sonona(depression). Dawa

zingine ni pamoja na ondasentron, acamprosate, setraline na

topiramate. Katika dawa zote disulfiram ndio imetokea kuwa

maarufu sana na ndio tutakayo izungumzia sana katika kitabu

hiki. Disulfiram ni dawa ambayo mtu akiitumia halafu akatumia

pombe hupata madhara ambayo yatamfanya asitumie/asitamani

pombe. Ni kama vile kula yamini. Mtu anayetumia dawa hii

huelezwa kwa undani madhara yatakayo mpata akitumia pombe.

Kwa kuogopa madhara mtu huyu hawezi kutumia pombe. Toka

mtu atumie dawa hii hatakiwi kutumia pombe hata kidogo ndani

ya siku kumi na nne (wiki mbili) vinginevyo atapata madhara.

Pombe hata inayopatikana kwenye vipodozi vya kupaka na

mouth washes (dawa za maji za kusafisha kinywa) inaweza

kusababisha madhara makubwa. Uzuri ni kwamba madhara haya

hayaui na huisha yenyewe japokuwa mtu anaweza hitaji

uangalizi wa mtaalamu wa afya kumpunguzia madhara

ayapatayo.

47

Madhara yanayoweza mpata mtu akitumia pombe na

disulfiram ni kama yafuatayo. Kuvimba uso, maumivu makali

ya kichwa, kupata tabu kupumua, kichefuchefu, kutapika sana,

kutoka jasho kwa wingi, kiu kali, maumivu ya kifua, moyo

kwenda mbio, kushindwa kuona vizuri na kuchanganyikiwa.

Watu wenye magonjwa ya moyo na magonjwa ya akili

hawapaswi kutumia disulfiram kwa sababu inaweza sababisha

madhara yanayoweza kuhatarisha maisha yao.

Pia tuliona mwanzoni kuwa watu waliotawaliwa sana na pombe

wakiacha ghafla wanaweza pata madhara yanayoweza

kuhatarisha maisha yao. Watu hawa wanapaswa kutumia dawa

hii kwa uangalifu wa karibu sana wa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…