Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Alcoholics Anonymous (A.A) ni ushirika wa wanaume na wanawake ambao wanashirikiana ujuzi, nguvu na matumaini kati yao ili waweze kutatua matatizo yao na kusaidia wengine kupona ulevi.

Sharti pekee la uanachama ni nia ya kuacha ulevi. Hakuna ada ya kuwa mwanachama wa A.A, tunajitegemea wenyewe kwa michango yetu wenyewe. A.A haifungamani na madhehebu yoyote ya dini, siasa, shirika au taasisi na haitaki kujiingiza katika mabishano yoyote. Kadhalika A.A haiungi mkono wala kupinga chama chochote.

Nia yetu ya msingi ni kukaa bila kulewa na kuwasaidia walevi wengine kufikia hali hiyo.

Kwa mawasiliano: +255 789 78 05 29
Huwa mnakutana wapi ili nije maana si unajua humu tunatumia majina tofauti!!!
 
Ni miaka zaidi ya kumi na tano kila nikijaribu nashindwa!!!
Great thinker what can i do so that never and never take in any alcoholic drink!!!!!

Lile zuri nilipendalo silitendi,Lile baya nisolipenda ndio natenda!!!!!!!!!!

Mwendee Yesu Kristo ukiwa na nia ya dhati kabisa ya kutubu dhambi zote na kumaanisha kuziacha,ikiwemo hiyo ya ulevi. Atakusamehe na kukupa uwezo wa kuzishinda kila zinapojaribu kukurudia. Soma Yohana 1:12....." Bali Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu,ndio wale waliaminio Jina lake"
 
Jiweke karibu na Mungu na uwe mtu wa Ibada utaacha tu.

Mkuu, Nuhu wa Biblia aligonga ile kitu hadi akazima, mwanawe akamchungulia. Halafu ndio alikuwa kipenzi wa Mungu, mwanaume pekee aliyebakishwa baada ya Gharika.
 
Amua kuacha.

dawa ya kuacha chocho ni kuamua kuacha
 
Chagua kati ya sigara na mademu maana pombe hutaki na duniani lazima uishi kwa kufanya kimojawapo
 
Wana JF,

Kwa yeyote anejua dawa au mbinu ya kumfanya mlevi kuacha pombe. Nina ndugu yangu yeye bila kilevi cha pombe siku haiendi kabisaa na hii imekuwa inarudisha maendekleo yake nyuma.

Wanaoijua tiba mnijuze niokoe maisha yake na familia yake.


Baadhi ya majibu kutoka kwa wadau



===============



kunywa maji lita 3 alafu kunywa maji yaliyochanganywa na magadi nusu lita baada ya hapo kunywa lita moja ya maji yaliyochanganywa na limao au ndimu. Fanya zoezi hili kwa mwezi mmoja lazima pombe utaacha. Proved to work successfully 100%
 
Mshauri azime simu kwa siku 3, ndani ya hizo siku 3 aletewe bia ndani tu, asitoke nje maana jua litaharibu dozi.
Siku ya 4 aende kazini, bosi wake akimuuliza kitu asijibu chochote ili mvuke wa bia usijetoka nje ukaharibu dozi. Bosi wake akimpa karatasi nyeupe yenye maandishi aichukue lakini akaisomee nyumbani. Hapo atakuwa amepata suluhisho la kuacha pombe.
 
Back
Top Bottom