Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Mbona ni rahisi kuacha pombe? Mrudie Mungu naye atakata kabisa kiu ya pombe na utakuwa mtu mpya,kuwa mtu wa sala na maombi na utakuwa umejengeka KISAIKOLOJI na kuishinda tamaa ya pombe.
this is theory...kumrudia ndio kufanyaje....
 
Bro mi nakushauri kunywa pombe tu....lakini pia ukipata tu salary siku ya kwanza fanya investment.....surplus kanywee pombe....Pombe ni tamuu sana
 
Hongera mkuu, crew zinaumiza sana... Zoez nimeanza. Bahati mbaya uwanja umejaa maji. Sasa hiv nafanya light exercises push ups na pia baiskel ya mazoez.
 
bro mi nakukubali sana...manake wewe ukiongea tu....yaani unakuwa nywiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
mkuu siyo utumwa wa pesa ila kuna gharama zinatakiwa kurudi.
 
Well said mkuu, nime catch points za muhimu....
Unajua kila mtu ana set goals & objectives zake. Za long term & short term. Tatizo ni discipline ya kusimamia maamuzi ya yale tunayopanga. Mkuu hizo high income bar ndio na meet na crew zangu za tangu college.
Nakunywa sana 777,Mliman city, Catalunya, Top Gerage. Master club Mikocheni, Bondeni pale na Amsterdam. Lakin hapa ndio majanga zaidi. All in all naona kama na avoid responsibilities. I need to be busy and focused. Na imani nitakuwa Okay, are open to changes and I want to restore my past reputation.
 
Biblia inaonya kuhusu matokeo mabaya ya kunywa kileo kupita kiasi. Waefeso 5:18 inasema: “Pia, msiwe mkilewa divai, ambayo ina upotovu ndani yake.” Vilevile, Methali 23:20, 21 inahimiza hivi: “Usiwe kati ya watu wanaokunywa divai mno, kati ya watu wanaokula nyama kwa ulafi. Kwa maana mlevi na mlafi watakuwa maskini.” Na Isaya 5:11 inasema: “Ole wao wanaoamka asubuhi na mapema ili watafute tu kileo, wanaokawia mpaka giza la jioni sana hivi kwamba divai inawawasha!”
Rudi katika misingi yako ya Imani (kama ni Mkristo) upo ushindi mkubwa katika hilo....Mimi pia nimepitia sana hilo jaribu.
 
Siku hizi hata kwenye ATM hauendi. Unaingia Simbanking unahamisha kwenda mpesa au tigopesa then unatafuta kibanda cha karibu unarejea.
Mkuu nakuelewa sana. Tuko kwenye mashua moja.
mkuu vipi wewe hautaki kitabu.
 
Hongera mkuu, crew zinaumiza sana... Zoez nimeanza. Bahati mbaya uwanja umejaa maji. Sasa hiv nafanya light exercises push ups na pia baiskel ya mazoez.
ngoja niendelee kupiga debe. kina mambo mengi hiki kitabu.

Zifuatazo ni mbinu mbalimbali ambazo zinatumika kupunguza au kuacha kabisa unywaji wa pombe.

1. tafuta kinywaji mbadala wa pombe kama vile chai au kahawa.

2.tafuta vitu mbadala vya kufanya kwa wakati ambao unakuwa unakunywa pombe kama vile kusoma vitabu na kuangalia filamu

3.tumia pesa ambazo unaziokoa kutoka kwenye pombe kwa kujiburudisha kama vile kula vizuri au kununua vifaa vya nyumbani. Hii itakusaidia sana katika kuona umuhimu wa kuacha pombe.

4.jiwekee mkakati kabla ya kwenda kunywa kuhusu kiasi utakachoenda kunywa na pesa utakayotumia. Usibebe pesa zaidi ya uliyopanga kutumia.

5. tumia glasi ndogo wakati wa kunywa na tumia vinywaji vyenye nguvu ndogo. Utafiti unaonyesha watu hunywa zaidi wakitumia glasi kubwa kuliko wakitumia glasi ndogo.

6.kunywa maji kabla hujaanza kunywa pombe. na unavyokuwa unakunywa pombe hakikisha unakuwa na maji ya kunywa karibu na uyatumie mara kwa mara.

7.jaribu kuepuka vishawishi vya kunywa. Watu wengi huwa tunashawishika kunywa kwenye mazingira fulani au tukiwa na watu fulani. Unachotakiwa ni kugundua ni vishawishi vipi hukufanya unywe na uanze kuviepuka.

8.kuwa na msimamo. Watu wengi ambao hujaribu kuacha pombe hukutana na wakati mgumu wanapopata ofa toka kwa marafiki. Njia sahihi ni kukataa bila kusitasita. Kusitasita kunaweza kukufanya uteteleke katika msimamo wako. Ni vizuri ukatafuta sababu ya kukataa ofa mapema kabla hata ya kukutana na ofa. Mfano, unaweza ukasema sinywi au siongezi pombe nyingine kwa sababu nataka kupunguza uzito au sababu nyingine ambayo utakuwa umeitengeneza kama ulinzi wako.

9.epuka kunywa pombe ukiwa na kiu au njaa. Hii inapunguza kiasi cha pombe ambacho kitaingia kwenye damu hivyo utapunguza madhara yake. Pia inasaidia kupunguza kasi ya mtu kuwa mraibu/teja wa pombe.

10.hakikisha ndugu na marafiki wanajua kwamba umedhamiria kuacha pombe. hii itasaidia kupata msaada kutoka kwao pia hawatakuwa wanakushawishi sana unywe. Pia hili linaweza kukusaidia kupata marafiki wapya kwani changamoto mojawapo ya kuacha pombe ni kupoteza marafiki.

11. kama unakunywa kwa kutumia glasi hakikisha kinywaji kimeisha kabisa ndo uongeze tena. Hii itakusaidia kujua ni kiasi gani cha pombe ulichotumia.


Kuna watu ambao mbinu hizo hapo juu zimeshindwa kabisa kuwasaidia kuacha pombe. msaada pekee ambao hubaki kwa watu hao ni kutumia dawa. Mara nyingi watu hawa ni wale ambao wanakuwa wametawaliwa sana na pombe na hupata madhara mara waachapo. Matibabu ya watu hawa hufuata hatua tatu muhimu.
 
Aanze kwa kupunguza idadi ya chupa anazotumia polepole kama alikua anakunywa bia 5 basi apunguze 4 polepole mpaka 1 halafu siku ifuatayo anywe chai ya Tangawizi changanya, mdalasini na asali kikombe kimoja kila siku, siku nyingine anywe juice ya limao na afanye mazoezi mepesi jioni, aendelee na chai hiyo
 
Kama taifa linalokuwa Tanzania inahitaji kuongeza vita dhidi ya ulevi wa pombe ili kuharakisha maendeleo ambayo awamu ya tano inayotaka uchumi wa viwanda.Ikumbukwe mwezi huu raisi ametengua (ametumbua) Waziri Charles Kitwanga kwa tuhuma kuwa alipata kinywaji (alilewa) kabla ya kuingia bungeni na hatimaye kutojibu sahihi swali lililoulizwa bungeni.

Hiyo imeonekana bungeni lakini ni ishara tosha kuwa ulevi umekithiri Tanzania na unaadhiri utendaji wa wafanyakazi maofisioni.Bila ya kusahau familia nyingi zinaharibikiwa kutokana na ulevi na ndio kiini cha uzalishaji katika taifa yani familia ndio zitatengeneza taifa la viwanda kwa utendaji wao.

Kwa kuwa ulevi umeonekana ni ugonjwa kama magonjwa mengine basi serikali inabidi ichukue hatua za haraka ili kufanikisha taifa la viwanda kujengwa.Hii imekuwa aibu ya taifa ya ndani na nje ya nchi kwa skendo ya ulevi wa waziri wetu.

Kutokana na nia ya dhati ya serikali ya kuanzisha taifa la viwanda na uwajibikaji basi vita dhidi ya ulevi unaoonekana kuathiri uwajibikaji na utendaji wa wafanyakazi, serikali inashauriwa:
1: Kupitia upya na kurekebisha sheria zinazohusu vilevi/pombe ili kuipa nguvu zaidi serikali na kuibana jamii katika uwajibikaji.

2: Kuanzisha specifed helping centres for alcoholism only kwa wale walioathirika zaidi na ulevi.Ulevi ni ugonjwa kama magonjwa mengine ambapo inabidi muathirika apewe medical assistance pamoja na pschological treatment chini ya uangalizi ili kuacha kama ilivyo kwa watumiaji wa madawa kulevya kule sober house Bagamoyo.

Mfamo: Japani kuna kuna hospitali inayoitwa Kurihama Alcolism centre ambayo inatumika kuwapa msaada waathirika wa pombe na hivyo kusaidia taifa hilo kwa kiwango cha hali ya juu sana katika maendeleo.Naomba kwa hili tujifunze japani au USA.Na tumeona watu wengi maarufu wakipelekwa huko na kufanikiwa.Tanzania tuna pschologists wengi sana na madoctor wa akili.hivyo serikali ichukue jukumu hilo.

3: Kuziongeza na kuzipa nguvu NGOs ili kuelimisha umma kuhusu ulevi, serikali ishawishi wadau kuanzisha NGOs na kuzipa kipaumbele ili kutoa elimu katika jamii na hatimaye tupate jamii iliyo makini na mafanikio.

4: Kuanzisha Forums na debate (mijadala) ya kitaifa kuhusu ulevi na kuipa jamii uwanja wakutoa maoni yao juu ya jambo hili.

5: Kuendesha kampeni dhidi ya ulevi kwa kutumia vyombo vya habari kama magazeti,Tv na Redio.Kwa kuwashirikisha wadau wa habari tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana dhidi ya ulevi na kupunguza tatzo la uwajibikaji.

6: Kuongeza vyombo vya upimaji kilevi na sio tu kwa madereva pia hata ofisi kubwa za serikali kama bunge, askari pamoja na hospitali kubwa mfano: madoctor wengi wanalewa hasa wakati wa upasuaji (operation)

Sheria pekee haitoshi kudhibiti suala la ulevi bali ukombozi wa kifikra ndani ya jamii.kuna baadhi ya watumishi hawafanyi kazi bila kunywa pombe (kulewa) kwa hiyo hata wafukuzwe au kupewa maonyo wanashindwa kujizuia kwani ulevi ni ugonjwa na unawasumbua sana.
 
uko vzr mkuu
 
Ni sawa kila mtu anapenda hivyo, ila ujue pombe na sigara ndio vitu vinakuza sana uchumi wa nchi, kuanzia kodi, mauzo ya malighafi kama sukari, shayir, ngano, mahindi, tumbaku nk. Pia ajira nyingi sana zimetengezwa kwa ajili ya pombe kuanzia breweries kwenyewe, wauzaj wa jumla mawakala mpaka ma bar maid na tender. Kwa hiyo generally pombe na sigara (hukuisema but i assume) ina athar kubwa sana kichumi kuliko unavyoweza kufikiri na dunia hii wameshindwa kuzuia.
Amin nakwambia wakisema wazuie leo hii Tanzania hata ww mleta mada source yako ya kipato itashake kidogo.
 

Asante mkuu kwa kutambua hilo.Lengo ni kudhibiti utumiaji wa hovyo wa hivyo vilevi lakini kama kureflesh siku moja moja ambapo utakuwa haupo bize na kazi ni sawa.pia tunaweza kuwa na vyanzo vingine vya mapato nje ya pombe.
Pombe inaadhiri akili moja kwa moja tofauti na sigara.angalia
familia zimetelekezwa kwa sababu ya pombe, uwajibikaji umeshuka,utu wa mtu unapotea,heshima,kupoteza kazi, madoctor wanauwa watu kwenye upasuaji sababu ya ulevi watu hawapo makini na kazi zao kwa sababu ya pombe.
why pombe? kwani hatuna vyanzo vingine?
Faida kwa mzalishaji(brewaries) na sio kwa jamii( kwa afya ya jamii) japo wanalipa kodi na kuajiri. yani muuza majeneza mtaji wake ni vifo vya binadamu.na anafurahi na kukukaribisha tena na kesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…