Hongera mkuu, crew zinaumiza sana... Zoez nimeanza. Bahati mbaya uwanja umejaa maji. Sasa hiv nafanya light exercises push ups na pia baiskel ya mazoez.
ngoja niendelee kupiga debe. kina mambo mengi hiki kitabu.
Zifuatazo ni mbinu mbalimbali ambazo zinatumika kupunguza au kuacha kabisa unywaji wa pombe.
1. tafuta kinywaji mbadala wa pombe kama vile chai au kahawa.
2.tafuta vitu mbadala vya kufanya kwa wakati ambao unakuwa unakunywa pombe kama vile kusoma vitabu na kuangalia filamu
3.tumia pesa ambazo unaziokoa kutoka kwenye pombe kwa kujiburudisha kama vile kula vizuri au kununua vifaa vya nyumbani. Hii itakusaidia sana katika kuona umuhimu wa kuacha pombe.
4.jiwekee mkakati kabla ya kwenda kunywa kuhusu kiasi utakachoenda kunywa na pesa utakayotumia. Usibebe pesa zaidi ya uliyopanga kutumia.
5. tumia glasi ndogo wakati wa kunywa na tumia vinywaji vyenye nguvu ndogo. Utafiti unaonyesha watu hunywa zaidi wakitumia glasi kubwa kuliko wakitumia glasi ndogo.
6.kunywa maji kabla hujaanza kunywa pombe. na unavyokuwa unakunywa pombe hakikisha unakuwa na maji ya kunywa karibu na uyatumie mara kwa mara.
7.jaribu kuepuka vishawishi vya kunywa. Watu wengi huwa tunashawishika kunywa kwenye mazingira fulani au tukiwa na watu fulani. Unachotakiwa ni kugundua ni vishawishi vipi hukufanya unywe na uanze kuviepuka.
8.kuwa na msimamo. Watu wengi ambao hujaribu kuacha pombe hukutana na wakati mgumu wanapopata ofa toka kwa marafiki. Njia sahihi ni kukataa bila kusitasita. Kusitasita kunaweza kukufanya uteteleke katika msimamo wako. Ni vizuri ukatafuta sababu ya kukataa ofa mapema kabla hata ya kukutana na ofa. Mfano, unaweza ukasema sinywi au siongezi pombe nyingine kwa sababu nataka kupunguza uzito au sababu nyingine ambayo utakuwa umeitengeneza kama ulinzi wako.
9.epuka kunywa pombe ukiwa na kiu au njaa. Hii inapunguza kiasi cha pombe ambacho kitaingia kwenye damu hivyo utapunguza madhara yake. Pia inasaidia kupunguza kasi ya mtu kuwa mraibu/teja wa pombe.
10.hakikisha ndugu na marafiki wanajua kwamba umedhamiria kuacha pombe. hii itasaidia kupata msaada kutoka kwao pia hawatakuwa wanakushawishi sana unywe. Pia hili linaweza kukusaidia kupata marafiki wapya kwani changamoto mojawapo ya kuacha pombe ni kupoteza marafiki.
11. kama unakunywa kwa kutumia glasi hakikisha kinywaji kimeisha kabisa ndo uongeze tena. Hii itakusaidia kujua ni kiasi gani cha pombe ulichotumia.
Kuna watu ambao mbinu hizo hapo juu zimeshindwa kabisa kuwasaidia kuacha pombe. msaada pekee ambao hubaki kwa watu hao ni kutumia dawa. Mara nyingi watu hawa ni wale ambao wanakuwa wametawaliwa sana na pombe na hupata madhara mara waachapo. Matibabu ya watu hawa hufuata hatua tatu muhimu.