Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Mazoezi yanakata hamu ya pombe aisee. Mimi shahidi, kuna bia nymbani kwangu kwenye friji mwezi wala sina mpango nazo.
 
Pombe inatia hasara sana mkuu,mie nilikuwa natoka na laki moja na nikikutana na kampani yangu ndani ya masaa matatu kilo imeisha nilikuwa natembea na card mfukoni ilifikia mahala beer zikinoga nampa mtu kadi na password anaenda kuchukua pesa mie niko baa tunakula beer,kuna siku nilimuagiza Rafiki yangu akaenda akachota na yeye za kwake niliumia sana,kifupi tungi inahasara kubwa kuliko faida,nashukuru mungu alinisadia kupitia Rafiki yangu mmoja ambaye tulipokuwa tukitoka kazini ananigada na kunishawishi kwenda kucheza darts badala ya kwenda kwenye zile kampani za hatari mwisho wa siku nashukuru nilifanikiwa kuacha pombe.
Wewe ulikua mshamba ba limbukeni.unahaki ya kuacha pombe kabisa maana ungeendelea ipo siku wangekufanya vibaya.unalewaje adi unajisahau ivyo???
 
Mi niliacha kwa kujiuliza swali moja ambalo ni hili "je naweza kumpa matak.o yangu mwanaume mwenzangu ayachezee"nikajijibu big No hapo hapo ni conclude kama siwezi kuwa shoga basi sitaki tena Pombe.
Mkuu inamaana walikufanya vibaya ulevini??
 
Tulikuwa Airport tunasubiri ndege,kuna jamaa pembeni yetu alikuwa anavuta sana fegi(chain smoker),jamaa yangu akawa anakerwa sana na lile jambo la uvutaji,akamsogelea yule bwana na kuanza kumsihi sigara ni mbaya kwa afya pia kama asingekuwa mvutaji angeweza kumiliki ndege kama hiyo tunayotaka kupanda.
Kwa dharaau yule jamaa(mvutaji) huku anapuliza moshi juu akamjuza yule ndugu yangu kwamba ndege tuipandayo ni mali yake.(full stop)
 
Mkuu inamaana walikufanya vibaya ulevini??
Daa kama vile unataka kunipanikisha anyway jibu ni hapana nilimanisha msimamo wangu wa kugoma kuendelea kunywa pombe unafanana na msimamo wangu wa siku moja mimi kuwa shoga.
 
Tulikuwa Airport tunasubiri ndege,kuna jamaa pembeni yetu alikuwa anavuta sana fegi(chain smoker),jamaa yangu akawa anakerwa sana na lile jambo la uvutaji,akamsogelea yule bwana na kuanza kumsihi sigara ni mbaya kwa afya pia kama asingekuwa mvutaji angeweza kumiliki ndege kama hiyo tunayotaka kupanda.
Kwa dharaau yule jamaa(mvutaji) huku anapuliza moshi juu akamjuza yule ndugu yangu kwamba ndege tuipandayo ni mali yake.(full stop)

Kwa mtu aliyejitosheleza kimaisha akilewa sio Mbaya, Lakini sisi wenye viela vya mawaza vimshahara vya milioni mbili, tatu,nne... Kunywa pombe ni anasa.

Ndiyo nasema tena salary below 5 milion ni mshahara mdogo sana kukesha bar
 
Kuacha pombe si suala la uchumi, ni kuacha uteja (addiction). Si jambo rahisi, kama ilivyo kwa uteja wa ulevi wowote ule.
 
Ni Kazi kubwa sana Binadamu kubadili tabia,
Ulevi ni tabia ya mtu na Ulevi una hasara nyingi tukubali au Tukatae.

Mfano.
kama unakunywa Bia Tatu kila siku weekends unakunywa tano ina maana unakunywa Bia 25 kwa wiki, Na nyie wa maofisini mnaknywaga windhock na Heineken that means ni Tshs. 3000 kwa bia.

Kwea mwezi ni 100 Beers at minimum kwa mfano hii 300,000 kila mwezi ungekua unanunua hisa za CRDB leo ungekua na hisa ngapi?

Ni mambo mangapi umefanya kwaajili ya ulevi yakakusabishia hasara?

Ukiajiangalia kwenye kioo huoni adhari za pombe usoni mwako?

Ni dini ipi inarhusu ulevi?

Muda unaotumia kulewa ungekua unasoma vitabu leo IQ yako ingekuwa tofauti kabisa!!!

Ni mara ngapi pombe imekupeleka kwenye mchepuko.

Ni mara ngapi unatoka Mbezi unaenda kunywa Tabata? hiyo gharama ya usafiri unaipigiaga mahesabu.


Hatua ya kwanza kuacha kunywa ni kuyawaza hayo hapo juu na mengine, ukishachukua hatua sasa naacha au napumzika jiwekee malengo.

Anza mazoezi, jioni unapotoka kibaruani fanya jogging! uchoshe mwili, ukienda kuangalia mpira bar agiza chupa yako kubwa ya maji ya kilimanjaro, au coka na maji mdodo mdogo unazoea.

Hali ni ngumu wazee, tupunguze matumizi yasiyo ya lazima
Mwenye masikio na asikie.
 
Nauza viwanja Chanika majumba sita...homboza...hatua 20 kwa 20 ni 3.5milion..nichek kama unahitaji..0756761698
 
Mkuu eb tuweke waz kidogo au walishawai kukutest ukiwa umebwia vyupa nini[emoji23][emoji23]
 
Mkuu eb tuweke waz kidogo au walishawai kukutest ukiwa umebwia vyupa nini[emoji23][emoji23]

Sijawahi kuona mtu amelawitiwa kwasababu ya ulevi, kama binadamu unakunywa pombe kiasi cha kulawitiwa basi unahetaji kwenda kwenye rehabilitation centres,

Binafsi sidhani mtu mwenye uwezo wa kutumia keyboard anaweza kufika level hiyo, kwahiyo sioni haja ya kujadili wanaokunywa pombe mpaka wanaishia kulawitiwa.
 
nimeacha ulevi mwezi wa tano sasa nilisema 0ctober 2016 to 2017 ni mwaka wa mabadiliko katika maisha. na kweli nimeweza. Ulevi sio dili ni kuongeza umaskini tu wa kipato.
 
Wewe ulikua mshamba ba limbukeni.unahaki ya kuacha pombe kabisa maana ungeendelea ipo siku wangekufanya vibaya.unalewaje adi unajisahau ivyo???
sawa mimi nilikuwa mshamba kwa hiyo wewe ujanja wako wooote unawaza kufirwa tu basi,blood cameron.
 
Nimeamua kuachana na Pombe baada ya kusoma mistari hii miwili toka kwenye kitabu kitakatifu cha biblia katika somo lile la Harusi ya Kana ambayo Yesu, mama yake na wanafunzi wake walialikwa. Msitari wa 2 na ule wa 6 umenigusa sana rohoni.

1 Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.
2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.
3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.
4 Yesu akamwambia, Mwanamke, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.
5 Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni.
6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.
7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.
8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.


Mstari wa 4, Yesu hakupendezwa kabisa kauli aliyoambiwa na mama yake na ndiyo maana akatumia neno "Mwanamke" kuonyesha mamlaka yake makuu badala ya neno "mama".

Mstari wa 6, Kwa kuidharau akawaambia wale jamaa wakajaze mabarasi (matawadhio ya chooni)
Hapa ndipo pamenifanya niache pombe, maana ilidharauriwa sana, mimi ningekuwa hapo nisingeinywa aisee..!!

Hii mistari 2 imenifanya niachane na hii kitu kabisa, mtanisamehe sana watu wa Breweries.
 
jina la bwana Yesu litukuzwe...

furahaaaa mwenye mdhambi mmoja akitubu *2
na siku moja tutapaa kwenda nae mbinguni *2
kwilililililiiiii karibu katika utumishi wa bwana na hongera kumkataa shetani na dhambi zake zote..

biblia inasema mwana aliyepotea alivyorudi kwa baba baba alimkaribisha na kukumbatia amen ..
 
Amina, Mungu akusaidie uache na dhambi zingine kama unazo.
 
Nashukuru sana kwa kunifafanulia hiyo mistari, Mola akuzidishie na hongera sana maana umechagua fungu jema
 
Back
Top Bottom