Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Nmekuwa mnywaji sana siku hizi. Nataka niache bia kabisa yaaani. Mwenye tips anisaidie.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Unataka kuacha kwa sababu 'umekuwa mnywaji sana' au kwa sababu unataka kuacha?

Kuacha inaanza na wewe! Mbinu unazohitaji zitakuwa na maana pale UTAKAPOAMUA kuacha.

Njia rahisi hapo mkuu,tafuta jambo mbadala unalolipenda,na ulifanye muda huo huo unaokunywa pombe,kuwa na nia ya dhati ya kuacha pombe,anza taratibu,kama uko kwenye mtandao,jitoe taratibu...

Anza kwa ku avoid company especially wale wasiokuunga mkono afu uwe na kitu mbadala cha kufanya esp. ile mida uliyokua unaenda kupombeka

dawa kuu kuliko zote ya kuacha pombe ni KUACHA KUNYWA

Habari ya kwako Makanyagio, uliweza tafuta dawa ya mdogo wako kucha pombe, ulitumia maziwa ya nguruwe au njia gani??

Tafadhali tujuze ili na sisi wengine tujue.....
many thanks...

pombe ndio inalipa pato kubwa zaidi kwenye kodi mi nafikiri
badala ya kufikiria sana kuacha tungi fikiria zaidi kuongeza
kipato mbona watu tunapiga tungi deily na maendeleo yanakuja tu.
Mbadilishe kimtizamo aweke malengo mbele badala ya pombe kila
kitu kitakaa mkao kabisa

Unajua unataka kuacha. Si uache sasa...! Ukiona unashindwa ujue una tatizo lingine, linajionyesha kwenye mitungi...

Mkuu.@adakiss23 Dawa ya kuacha Pombe tafuta Mama anaye nyonyesha akutilie kwenye pombe yako maziwa yake kidogo tu utaacha kabisa kunywa Pombe fanya hivyo. Au hii dawa ingine ya kuacha kunywa Pombe tafuta mafuta ya Ubuyu uwe kila siku unakunywa hayo mafuta ya Ubuyu kijiko kimoja kwa muda wa mwezi mmoja utaacha kunywa Pombe ukipona unipe FeedBack

Hongera sana. Pombe ina hasara zaidi mwilini kuliko faida. Na unaweza kuacha, my nephew has more than 17 years toka aache jumla jumla.
Kwanza jiaminishe kwa nini ni muhimu kuacha pombe. Focus kwenye sababu za kiimani, kiafya na kisosholojia (pombe inaharibu mahusiano jamani, mnaokunywa more than three beers a day i am sorry kuwaamvia mnadhraulika kwa wake zenu. Painful truth, unless mmeoa pampula wenzenu mkifika home mnakoromeana tu).

Challenge kubwa utapata kwa walevi wenzio wa zamani. Ukijiaminisha una sababu za kitosha then utawakabili. Hata ukishindwa ukarudi nyuma its ok, amka uanze upya na utaweza. Haifanikiwi kwa siku moja tu, jipe muda. Kila la kheri

By adakiss23

Nmekuwa mnywaji sana siku hizi. Nataka niache bia kabisa yaaani. Mwenye tips anisaidie.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

umefulia au? toa sababu za kuacha ili upate msaada.
Huyu kafulia.Hamna lolote

:help::help::help::help::help::help:mshirikishe mungu katika hili utafanikiwa...:help::help::help::help::help::help::help::help::help:

nilisikia maziwa ya kitimoto unachanganya kwenye pombe unayokunywa unatapika inakuwa mwisho wa kunywa

Nashukuru sana kwa swali lako,Nami Nina shida kama yako NA natumai nitapata msaada kupitia hii forum.....tatizo kubwa mie sio kampani inanihamasisha kwani Mara nyingi nakunya nikiwa nyumbani,NA siku za karibuni nimekuwa nikipata shida Sana kupata usingizi kama sijanywa,mbaya zaidi nakunywa pombe Kali kwani bia siziwezi...msaada tafadhali.

Wewe unataka uache pombe, hii umei-post siku nyingi. Unachonishangaza ni kwamba pamoja na kupewa ushuri wa kutosha bado jana ulikunywa hadi kushindwa kujielewa na ukafikia hatua ya kumuomba mwanaJF yeyote aliye tayari kutoka na wewe afunguke....au si wewe? Au ushauri wote uliopewa na wadau wote hakuna hata mmoja uliokusaidia? Ukiamua kufanya jambo fanya acha kusita-sita.

Nmekuwa mnywaji sana siku hizi. Nataka niache bia kabisa yaaani. Mwenye tips anisaidie.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Wewe unataka uache pombe, hii umei-post siku nyingi. Unachonishangaza ni kwamba pamoja na kupewa ushuri wa kutosha bado jana ulikunywa hadi kushindwa kujielewa na ukafikia hatua ya kumuomba mwanaJF yeyote aliye tayari kutoka na wewe afunguke....au si wewe? Au ushauri wote uliopewa na wadau wote hakuna hata mmoja uliokusaidia? Ukiamua kufanya jambo fanya acha kusita-sita.

So?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Back
Top Bottom