Kwanza nikukatishe tamaa kabisa. Kama huna refa wa serikalini ambaye atakuwa anakupa kazi jiandae kisaikilojia. Hukatizi.
Hata hivyo maadam unalilia wembe ngoja nikupe.
1. Brela unayo.
2. Pata TIN
3. Pata leseni ya kuuza fenicha
Google taneps, anza kujisajili. Utapata usajili huo. Hapo zitakuja tenda kubwa kubwa za fanicha ambazo masharti yake huyawezi. Maana huna mtaji, huna VAT.
Subiri kwenye email yako iko siku utaona GPSA wametoa tenda za kujisajili kuwa wasambazaji wa vitu mbalimbali. Hapa kila mkoa una tenda yake. Kama leseni yako ni ya Dodoma lazima uchague tenda ya fanicha ya Dodoma. Utajaza watakusajili. Hapo utapata tenda ndogondogo za mkoa huo tuuuuu. Ndio utaratibu wao. Hata kiti kimoja itakuja.
Hapo utasubiria machungu. Ukitenda ukifungua utakuta mko 50 mliopeleka tenda na wewe ni wa bei yako ni ya 40.
Pambana kijana.