Njia zipi unaweza kuzitumia kuondoa sonona?

Pole sana.
Wengi wamekuwa wanapitia hali hiyo.
Lakini cha kwanza ufahamu tu tatizo ni nini? Pia ujue kwamba kuliwaza sana tatizo sio njia ya kulishughulikia.
Tambua usuluhishi wa suala husika kama hakuna namna achana nalo usiliwaze kabisa. Aidha, kama ni ishu ameisababisha mwingine pengine wewe unasubiri akuombe msamaha, jiwahi wewe ndo usamehe na uendelee na majambo yako.
Maisha ni mafupi sana, na yote yanapita jitahidi usikae kizembe kabisa.
 
Pole

Tafuta mtu ni vyema kutafuta washauri bahati nzuri Tanzania tuko wengi mueleeze kuna ambao hufanya kwa malipo na kuna ambao ni bure

Tafauta mtu unayemuamini mueleze

Mueleze mtu usiyekufahamu ila umehisi unaweza funguka zaidi kwakwe sikia ushauri wake

Nenda mahali tulivu au beach kaseme yoote yanayokuumiza kisha achilia moyo

Fanya unavyovipenda zaidi

Muhimu jua amani yako iko ndani yako.

Kama unapenda kusoma vitabu. Naweza kupatia kadhaaa ukajijenga
 
Labda uelezeee tatizo au matatizo yanayokukabili tujue jinsi ya kukushauri accordingly.

Haiwezekani kukupatia general advise.

It should be specific and tailored.
 
1.Kujua chanzo cha tatizo/sonona inayokukabili
2. Aina ya sonona unayokabiliana nayo. Je, ni ya muda mfupi, muda wa kati? Au ni ya kudumu?
3. Kubaini kama chanzo cha sonona kinaweza kuepukika, kutatuliwa kwa njia za muda mfupi au muda mrefu au inahitajika kukubaliana na hali halisi ya sonona husika. Mfano kama chanzo ni kufiwa na mtu wa karibu sana inabidi kufanyike jitihada kwa muhusika kukubaliana na hali na kuyapokea mapenzi yaMungu.
3. Kuandaa mikakati ya kuondokana na sonona husika. Hapa unaweza kuweka ya muda mfupi, wa kati na mrefu.
4. Kuchukua hatua madhubuti dhidi ya sonona husika.
5. Kama hutaweza kutatua mwenyewe, kuwashirikisha watu unaowaamini inaweza ikawa njia ya kuelekea uponyaji. Mfano: Viongozi wa Kiroho, viongozi wa kimila, au watu wenye busarana utaalamu juu ya sonona inayokukabili
 
Pole sana ndugu,Mungu akusaidie
 
Unaishi wapi mkuu ?
Naweza kukusaidia..
Kama hutojali tuonane
 
Tatizo laweza kuleta madhara kwa 10% tu lakini madhara 90% hutegemea na mwitikio wa mtu juu ya tatizo hilo.

A problem can harm only 10% the 90% depend on how you react over it (situations/problem).
 
Let me be your friend, I can try somehow to comfort you.
But you have to put faith on
 
Nmeongea na simu kibao. Nnachopokea ni pole tu. Hamna hata anayesema uko wapi tuongee najieleza wee then pole yatapita basi
Like, how? unahitaji mtu wa kukufariji mpaka uwe naye karibu,mpate conversation za face to face
 
Safi.
 
Una madini sana kaka, Mimi Sonoma yangu ni tamisemi kunipanga kigoma aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…