1. Mkoa wa Njombe una watu wachache kuliko mikoa yote ya bara kwa mujibu wa sensa.
2. Mkoa wa Njombe ni wa pili baada ya Dar kwa utajiri kwa kigezo cha per capita income.
3. Mkoa wa Njombe unaongoza kwa idafi ya mabilionea nchini.
4. Mkoa wa Njombe, una eneo kubwa la kiutawala kuizidi mikoa mingi ya bara.
Je, kigezo cha kuwa mkoa, una uhakika ni idadi ya watu pekee yake?
Lakini ufahamu pia, sensa ni kwaajili ya kutoa picha tu ya jumla, lakini siyo halisia. Watu wengi siku ya sensa hawakuhesabiwa maeneo yao.
Tukitaka kupata idadi halisi ya watu toka eneo la kila mahali, labda tufanye sensa kama ilivyokuwa inafanyika enzi za Yosefu na Maria. Wao walisafiri mpaka eneo walikozaliwa, Betlehemu ili kwenda kuhesabiwa.
Idadi hiyo kubwa kabisa ya Dar, wala siyo wakazi wa Dar, bali wapo kwa shughuli za muda mfupi, wa kati au mrefu. Ni wachache ambao ni wakazi wa kudumu. Hata Mwalimu Nyerere aliishi Dar wajati wote akiwa Rais, lakini alipostaafu alirudi kwao, Butiama- Musoma.
NB: Mara nyingi wenye uchiumi mzuri husafiri na kutawanyika sana.