Njombe ilinyofolewa kutoka Iringa leo ina watu wachache kuliko mikoa yote Tanzania Bara

Njombe ilinyofolewa kutoka Iringa leo ina watu wachache kuliko mikoa yote Tanzania Bara

kwa mujibu wa hilo jedwali kuna mikoa takriban 16 ina watu wengi kuliko visiwa vya Zanzibar
 
Naendelea kuchunguza hizi takwimu za sensa za mwaka 2022 na kuendelea kujiuliza sababu ya kugawanya mikoa na wilaya. Kwa watoto lazima mjua baadhi ya mikoa ilikuwa wilaya tu awali, mikoa hiyo ni pamoja na Songwe, Katavi, Geita na Njombe.

Leo nimeangalia mkoa wenye watu wachache nchini Tanzania, mikoa ya Zanzibar ina watu wachache. Lakini kwa kufananisha mikoa ya bara pekee, mkoa wa Njombe ni mkoa wenye watu wachache zaidi nchini.
View attachment 2816382

Je, ni kweli tunaanzisha wilaya na mikoa kwa ajili ya kupeana zawadi kwa nafasi za teuzi. Je ugawaji wa mikoa na wilaya unaongeza tija kwa maendelea ya sehemu husika?

Kwa kuzingatia gharama za uendeshaji mkoa, Je ni kweli tunazingatia kuona umuhimu wa kuwa na mikoa mingi. Kama tutahofu kuhusu ukubwa wa eneo kijiografia, hatuoni kuwa tunatoa umuhimu kwa nchi kugawwa ili kuwa na marais wawili kuunguza mzigo.

So manya questions.
Mikoa mingi ni ushahidi wa ufisadi wa kisiasa na ubinafsi wa watawala.

Nyuma ya kuanzishwa kwake ni wanasiasa wenye ushawishi wakiamini hilo lingesaidia kuharakisha maendeleo kwa wajomba zao huko vijijini kwao.

Pandora box ilifunguliwa na Sumaye alipoimega Arusha na kuanzisha mkoa wa kwao Manyara.

Muendelezo ukaja wakati wa JK/Magufuli:
1. Njombe...ex spika Anne Makinda
2. Simiyu...mzee Andrew Chenge
3. Geita...late president Magufuli
4. Katavi...ex PM Mizengo Pinda
5. Songwe........

Tusubiri tuone kama Majaliwa naye ataigawa Lindi au Bashe naye aivunje Tabora.

Kadhalika mgawanyo wa wilaya na majimbo mapya ya chaguzi...it's all about 'us'....it's our turn to eat! Yote ni ubinafsi na kutengeneza njia za kula jasho la mwananchi tu!

Maendeleo yatakuja kwa watu kufanya kazi kwa bidii na maarifa yao yote na kuacha wizi na ufisadi huko serikalini. Hata tuwe na mikoa 50 na wilaya 500...as long as kazi hazifanyiki na ufisadi umeenea ni kazi bure!
 
Nakumbuka nilihudhuria RCC moja Iringa mjini, RC anawauliza ma-DC mlianza safari lini? Vituo vya njiani mlilala wapi? Nikashangaa DC anatumia siku 2 kufika mkoani.

..huduma ambazo wananchi wanazifuata makai makuu ya mkoa haziwezi kupelekwa karibu na wananchi bila kugawa mkoa au wilaya?

..mimi nadhani ni busara zaidi kuboresha miundombinu na kuongeza matumizi ya tehama ktk kujaribu kuwafikia wananchi wengi zaidi.
 
Back
Top Bottom