Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Pole sana, ni heri umeandika hapa ili ufahamu ukweli, hao watu ni matapeli tu, wanaotumia kivuli cha Mungu ili wawaangamize wengine..Jambo kama lako lilishanitokea na mimi zamani kidogo, lakini kabla ya hapo nilishawahi kuwasikia kwenye radio, lakini sikutilia maanani mpaka nilipokutana nao..

Mazingira yao ni hayo hayo, watakuja day one, wataondoka, kisha watarudi, mara ya pili au hata ya tatu, lakini safari hii wakiwa na vihirizi vyao walivyojiundia wenyewe, na ni lazima waje usiku..sasa wanachofanya ni kuvirusha, aidha nje,au ndani wakati wanapoingia au wanapojifanya wanafanya maombi wakati wewe umefumba macho, lakini kwa siri..Wakishamaliza, wanajifanya wameingia katika rohoni, kisha baadaye wanakwambia nimeona kitu, wanakuambia tuondoke twende..wanaelekea maeneo yale yale yaliyotupa hizo takataka zao, kisha wanajifanya wanatafuta tafuta..

Baadaye wanaona, ndio hapo wanakwambia walikuwa wanataka kukimbia wakaacha hirizi zao..sasa kama wewe ni yule wa kuombewa ombewa tu, bila kujitathimini Imani yako na Mungu wako ipo wapi, watakuzomba na maji haraka sana...

Mimi nilikuwa na watu wengine nao walikuwa wameshaogopa, kumbuka saa hiyo ni usiku wa saa 4 au 5 hivi..Lakini nilivyoona vile nikamweka chini siku subiri muda, nikamuhubiria, nikamwambia hapa umekutana na nuru, na ukijaribu kupambana na Nuru utakuwa kipofu..akaogopa, nikataka kumfukuza, watu wakasema tumwache tu asubiri asubuhi aondoke, ilipofika asubuhi aliondoka kwa aibu ya ajabu, mpaka leo hii sijui yule mtu alipotelea wapi, sijamwona tena..

Hivyo kwa ufupi jua hakuna uchawi wowote hapo,..Usiogope, ila na wewe pia, au mwingine yeyote anayesoma uzi huu, simama katika Imani yako. Mwamini Mungu. Soma Neno..Kwasababu hizi ni nyakati za mwisho. Manabii wengi wa uongo wapo duniani, na watawadanganya wengi..
 
[emoji33]Mh! Hata mi nahisi hawa mafala watakuwa walichukua yangu , waliponinyoa nywele usiku
Maana kuna mambo unaset fresh ikifikia wakat wa kuanza mabalaa yanatokea
Mchawi sio m2 mzur kabisa
 
Mwaka 2006 ilitokea binamu yangu akafariki, kipindi hicho tulikuwa tunaishi Bunju na bunju ilikuwa haijawa kama ilivyo sasa hivi yani kulikuwa hakujaendelea.

Kabla ya kufariki alianza kuugua akawa hana nguvu sasa alikuwa ana tabia akitoka kazini wakati anapanda ngazi kwenda chumba chake kwasababu nyumba ilikuwa ni ghorofa chumba chake kilikuwa floor ya juu, akipanda ngazi kama nne anachoka anakaa kwenye ngazi ana guna Mmmh.

Sasa wakati anafariki alikuwa kasafiri kaenda kuhuduhira harusi ya ndugu yake akiwa hhuko mkoa akazidiwa akakimbizwa bugando akafia Bugando. Tulipigiwa simu kuwa kafariki na mazishi yalikuwa hukohuko Mwanza hivyo tulipaswa kuondoka kesho yake kwenda huko. Sasa ajabu kesho yake kabla hatujaondoka, tulianza kumhisi akiwa humo ndani na muda mwingine unasikia akiita au akipanda ngazi na kuguna kama alivyokuwa anafanyaga.
Tukaenda kwenye mazishi tukazika na kurudi.

Hali ikaendelea hasa ile ya kusikia anapanda ngazi na kuguna. Ikawa tukienda kazini ndani anabaki dada wa kazi nyumba anaiogopa anaikimbia anaenda kukaa kwa majirani mpaka tukirudi.

Ikafika kipindi watu tukawa hatulali kila mtu anateseka kwa style yake. Nyumba ikawa siyo nyumba ile yani ikifika muda wa kurudi nyumbani kutoka kazini unatamani ulale huko huko.
Nakumbuka alikuja mchungaji flani akaiomba ile nyumba ndipo visanga vikaisha. Kwa sasa hiyo nyumba iligeuzwa shule.

Kuna mengi nimeyashuhudia ila dunia ina mambo nyie acheni.
 
...yaani umeniongelea mimi mkuu
...sasa sijui tufanyeje ?
[emoji33]Mh! Hata mi nahisi hawa mafala watakuwa walichukua yangu , waliponinyoa nywele usiku
Maana kuna mambo unaset fresh ikifikia wakat wa kuanza mabalaa yanatokea
Mchawi sio m2 mzur kabisa
 
...yaani umeniongelea mimi mkuu
...sasa sijui tufanyeje ?
Mkuu acha tu, mi ningefanikiwa kumtambua nabii WA kweli kwenye dunia ya sasa ningeenda huko akaniponye
Maana wengi ni matapeli
 
Nakumbuka kuna mwaka tulienda kufanya sampling mkoa fulani, kutoka mjini hadi huko kiijijini ni mbali mno na barabara zenyewe ziko hovyo.

Baada ya sampling tukaanza safari ya kurudi mjini, njiani kuna mzee mmoja akatuomba lift tukamwambia mzee gari imejaa akasema sawa,

Basi baada ya kama km 2 gari likaharibika tukachokonoa chokonoa yule mzee akatukuta na akatupita, gari lika faa tuakanza safari, tukampita yule mzee tena ila baadaye likaharibika tena, yule mzee akatupita tena.

Basi mchezo ukawa ule ule mwisho tukaona itakuwa huyu mzee ndo anatuchezea, tukaona ngoja tumpe lift tu, alivyotukuta tena tunachokonoa chokoa tukamwambia mzee, subiri turekebishe tukupe lift mzee akakubari.

Gari lilivyo faa halikuhabirika tena hadi tunafika mjini.
 
Duh ni hatari mkuu
 
Mmh...aliyemviza yupo karibu yenu kabisa..
 


Mzee alitisha sana huyo😄
 
Pol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…