Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Hilo tena halina mjadala.Unashangaa mikosi inatoka wapi kumbe ulilala na pepo usijue
Hivi viumbe (majini mahaba) vipo kwaajili ya kukusanya mbegu zetu za kiume kwa matumizi yao katika ulimwengu wa giza na kutuachia mikosi maishani. Tuwe watu wa Ibada na kumuweka Mungu karibu nasi, vinakosa namna ya kutuingilia.
 
Nikiwa na miaka 9 au 10 hivi nilikuwa naishi mkoa mmoja pembezoni mwa Tanzania. Siku moja nikiwa nacheza mpira barabarani na wenzangu mpira ulimgusa (sio kumpiga) bibi mmoja aliyekuwa anapita hapo barabarani.

Bibi aliinama na kuuokota ule mpira. Akaushika mkononi. Nikiwa sina hili wala lile nilimfuata yule bibi na kumtaka anipe ule mpira niendelee kuucheza na wenzangu. Bibi alikataa. Akauliza kwa ukali kwanini ule mpira umempiga. Nikajibu ni bahati mbaya lakin pia ni kwamba umemgusa tu hivyo haujamuumiza. Nilisema hayo maneno huku nikinyoosha mkono ili niuchukue mpira kutoka mkononi mwake.

Lakini bibi alikuwa kadhamiria kutonipa ule mpira. Akawa anataka labda nibembeleze lakin mim sikuona kosa tulilofanya hivyo sauti yangu na matendo yangu yakawa sio ya kubembeleza wala kuomba msamaha. Nikazidi kunyoosha mkono kuelekea ulipo mpira mkononi mwake na yeye akazidi kurudisha mpira nyuma ya mwili wake.

Alivyoona sielekei kutulia wala kubembeleza akautupia mpira kwenye majani yenye miiba miiba kando ya barabara. Nilikereka sana. Sijui hata kwanini. Nikamropokea maneno mabovu. Ilikuwa sio kawaida yangu lakin kwakweli nilisema maneno ambayo si mazuri kwa mbibi kama yule.

Nafikiri ni ujinga wa kitoto au vile nlikuwa na kiherehere cha kutaka kuendelea kucheza haraka na nilijua fika kuutoa ule mpira kwenye miiba ile kutanichukua muda mrefu maana inabidi niwe makini na niingie polepole sana ili nisichomwe.

Sasa baada ya kumtamkia neno mbofu yule bibi aliondoka bila kusema neno. Yaani aliurusha mpira majanini, mim nikamtamkia neno la ovyo wakat anaondoka na alisikia.

Nilichukua dakika chache kuutoa halaf nakumbuka hata dakika 2 hazikupita tangia nianze tena kucheza nikaanza kujisikia kuumwa. Dalili zote za kuumwa nilikuwa nazo. Nguvu sina. Kichwa kinauma, joto limepanda.

Nikawaambia wenzangu naondoka naumwa. Wakashangaa. Nikaenda kujilaza nyumban. Dingi akaenda kuitwa shamban. Akakuta nimelala mkekani, naumwa. Si kawaida mim kuumwa, zaman mpaka leo. Niko hivyo. Na nikiumwa sio wa kulala. Sasa kunikuta naumwa mpaka nimelala wakat lisaa limoja kabla nilikuwa njema kabisa alishangaa sana.

Akauliza naumwa nin nkajibu najskia tu kuumwa. Dingi aliuliza vitu vingi nilivyokula au kunywa lakn sikuwa nimekula wala kunywa chochote tofaut na vya pale maskani.

Katika kudadisi zaidi ndo ikaibuka stori ya bibi tuliyempiga na mpira. Dah, duh, loh. Dingi akafura. Haraka akatuma watu wawili wamfuate fasta sana bila kuchelewa.

Bibi akafika home. Dingi macho yakiwa yamemuiva akaanza kumkoromea bibi. Akatishia kumkata kata na mapanga. Akaanza kuongea mengi yanayosemwa juu ya bibi na kwamba yeye atammaliza na hata muda huo anataman aingie ndani achukue panga amkatekate. Dingi yangu alikuwa mkali sana lakin sikuwahi muona akiongea kwa ukali na kudhamiria kama siku ile. Dingi akasema nipone muda huo huo lasivyo atamfuata kwa mumewe akamuulie hapo. Bibi akafukuzwa aondoke haraka kabla hajafuata panga ndani.

Bibi aliongea kwa unyonge kuwa ni bahati mbaya nimeumwa ila nitapona tu. Akanyanyuka aondoke. Dingi macho mekunduuu, midomo inatetemeka kwa hasira

Ajabu sana. Ile bibi anapotea tu machoni petu yaani kafika mita 30 hivi kapitia kwenye mahindi na mihogo ya pale maskani hivyo hatumuoni mim nikaanza kuzungusha macho kutafuta mpira uko wapi. Nikauona. Nikanyanyuka. Nikauchukua huyooo mbio barabarani tena kucheza, nishapona hivyooo

Niko fiti kabisa na kwa muda huo bibi atakuwa hata 1 ya 10 ya safari ya kufika kwake hajaimaliza. Ndugu na jamaa wanakuja kuniangalia mgonjwa mim niko bize kwenye mpira nishapona. Nimepona ponaje? Niliumwa umwaje?

Mkwara wa dingi ulisaidia japo najua dingi yangu akili zake alikuwa anazijua mwenyew kumkata kata bibi alikuwa hatanii. Baadae ndo nilikuja kujua kuwa bibi alikuwa anaugua mpaka anakufa halaf anafufuka. Pia nilikuja kujua kuwa bibi alikuwa anaoza nusu ya mwili wake mpaka funza wanatoka lakin hafi. Kumbe Bibi alikuwa master wa uchawi pale kijijini

Hiki ndo kinanifanya nibabaike sana ninaposikia uchawi haupo na kwamba kama upo eti unawakumba wanaoamini tu. Sasa mimi mbona nilipigwa dafrao na bibi wakat nilikuwa sijui kama bibi ni master?

Kama haupo ilikuwaje mimi kuumwa baada ya kumkera yule bibi? Ikumbukwe sikuwa na background information yoyote juu ya uchawi wa yule bibi na nilikuwa simwogopi. Na yule bibi alikuwa na mjukuu wake wa kike nilikuwa nasoma nae darasa moja na siku ya tukio alikuwa ameongozana nae na alikuwa best yangu

Ijapokuwa kipindi kile sikutishika (sababu ya utoto?) lakin lile tukio ndo linanifanya mpaka leo niamin uchawi upo na ukijaa kwenye anga za wachawi wanaweza kukufanya kitu mbaya
 
Kuna zile bar unakuta zinajaza watu zina wahudumu warembo kweli wengine huwa ni majini hasa zile bar ambazo wamiliki wake wanamikataba ya kishetani kwa ajili ya mali
Kuna Bar iko mitaa flani hivi kule chuganian,ukimuelewa mhudumu fresh unampanga then anazuga zuga pale baadae anaingia chini ya meza(ni zile meza zenye cover za plastics ndefu) unashusha zipu kiaina yeye anaendelea kunyonya mkuyenge huku wewe unakunywa zako bia kama vile hakuna kinachoendelea,ukimalizana nae anatoka chini ya meza nduki anaendelea kuhudumia wateja kawaida kabisa.

Itakua wateja wa pale wamenyonywa sana na majini kule chini ya meza.
 
Inaitwaje hiyo bar mkuu? 😂
 

🙄🙄🙄🙄
 
Imenikumbusha .... nilikuwa natoa story na friends kuwa nikinywa Almond milk usiku napiga mabao hayafai....

Baada ya few days mmoja ya wana akanifuata... mkuu yale maziwa ya kupiga mabao yako wapi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Nilielezea tatizo... mwana kaona fulsa
Inaitwaje hiyo bar mkuu? [emoji23]
 
Mkuu Kama kweli wewe sio mchoyo wa fadhila Basi tupe angalau mtaa au Basi kiroho Safi tupe jina kabisa la hio baa niende na kikosi kazi Cha maombi kwenda kuwakemea na kuwafukuzia mbali hayo mapepo.
 
Hii story imenisisimua sana. Napenda sana story za re - incarnation. Hebu mkuu tafuta mambo hayo ya reincarnation hata YouTube afu fananisha na story yako.
 
[/QUOTE]
Wengi wanaohadithia mambo yao wanaihusisha tabora.hakika tabora ni kiboko kwa uchawi na kuwanga..true Bantu..
 
Wengi wanaohadithia mambo yao wanaihusisha tabora.hakika tabora ni kiboko kwa uchawi na kuwanga..true Bantu..
[/QUOTE]
Inawekana hivyo ila nachoamini mikoa mingi mpk miaka ya mwishoni mwa 90
inaamini sana ushirikil
Wengi wanaohadithia mambo yao wanaihusisha tabora.hakika tabora ni kiboko kwa uchawi na kuwanga..true Bantu..
[/QUOTE]
Mikoa mingi mpka mwishoni Mwa miaka ya 90 walikiwa wapo kwenye ushirikina wa kiwango cha juu sio Tabora tu ila utandawazi umepunguza sana haya mambo hasa vijijini
 

Pumbavu unaleta story za jeshini huku,hayo mambo ya kazini kwako unatuletea raia ili iweje?hujaiva wewe
 
Mkuu umenikumbusha hili neno Dafrao . Hivi maana yake Ni Nini hasa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…