Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Unakaa kwenye kona kwa nje au kwa ndani, na nikiwaona halafu nikasepa inakuwaje kabla hawajarudi?
Hahah nimegundua wewe Mwoga, usijaribu kama hauna moyo, mimi binafsi sikurudia na sitarudua mchezo huo

Nb: Unakaa kwenye kona nje ya nyumba.
 
Hahah nimegundua wewe Mwoga, usijaribu kama hauna moyo, mimi binafsi sikurudia na sitarudua mchezo huo

Nb: Unakaa kwenye kona nje ya nyumba.
Kumbe rahisi tu, 😃.Hakuna asiye nervous katika hali kama hizo kinachohitajika ni courage tu katikati ya hofu mkuu.Sasa mwenye nyumba baadae aliwa mind au mlichuniana tu😃😃.
Dah aisee hii mbinu simple sana then unamjua mbaya wako...
 
Mkuu hizo za kukubana usiku ni nyingi sana aisee, mara zote kukemea kwa jina la Yesu ndio hua kuniokoa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu isije ikawa tunatoka kijiji kimoja, hata kwetu ilitokea hiyo kitu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mbwa na mchawi ni vitu viwili tofauti. Hata wangu waliuliwa kikatili.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wewe tulia tu...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuja asubuhi akatutania nyie vijana ni (wajeshi sana) akimaanisha wakakamavu, baada ya wiki Tulipewa notice akidai anataka afanye ukarabati wa nyumba yake[emoji23]
 
Alikuja asubuhi akatutania nyie vijana ni (wajeshi sana) akimaanisha wakakamavu, baada ya wiki Tulipewa notice akidai anataka afanye ukarabati wa nyumba yake[emoji23]
😂😂😂 daah noma sana aisee,nimekaa hapa katika kona na stuli na jiwe naona bado,sijui wamenishtukia au sijakaa fresh,kuna mother ana shape wanasema ni mkali wa hizo mambo,akija kinyume nyume sirushi jiwe na enjoy tu
 
Nimejaribu kila njia ya kukutana na haya mambo lakini wapi
Nikisikia huyu bibi mchawi au huyu mzee ni mshirikina mimi kazi yangu ni kuwauliza tu hivi mnapata faida gani kuroga?

Yote hiyo natafuta huo wanga
Sina woga labda ndio sababu nao wananipuuza
Nikaona isiwe shida nikawa naenda kukaa makaburini manane ya usiku maana nikuambiwa ndio mda wa wawangaji kuwanga

Napo sikuambulia kitu zaidi ya mara mbili jamaa kunikimbia huku wanapiga yowe [emoji23][emoji23]
Yaani mpaka haunted house nimeingia sana zaidi ya baadhi ya vyumba kuwa baridi la kufa mtu lakini hakuna kitu cha kunifanya nikimbie
Kuna kizee Fulani waliniambia huwa kanapaa usiku
Nikakauliza naomba lift
Kakasema ya wapi tena nikakaambia kwenye ungo kalisonyaa mpaka kanapotea [emoji23][emoji23]


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mzee mwenzangu Titicomb
Sleep walking ipo na uchawi upo..! Kuna mambo mengi sana humu duniani, usibishane sana kwa kitu ambacho wenzio wamekishuhudia wewe hujashuhudia!!
Enwei, naamini uchawi upo ila sijawahi kukumbana nao uso kwa uso..!
 
Mzee mwenzangu Titicomb
Sleep walking ipo na uchawi upo..! Kuna mambo mengi sana humu duniani, usibishane sana kwa kitu ambacho wenzio wamekishuhudia wewe hujashuhudia!!
Enwei, naamini uchawi upo ila sijawahi kumbana nao uso kwa uso..!
katika vitu siamini in uchawi sijui majini labda mpaka nishuhudie



au mods mnasemaje???
 
Una bahati ulikuwa bado mtoro huyo mrefu alokuwa anakufata nyuma huwa mshenzi sana sema haui ila huwa anasumbua balaaa. Hapendi kukimbiwa. Ukimkimbia imekula kwako, we akija jifanye humuoni ikiwezekana kaa chini ama lala chini ili apite. Ila komesha yake vua nguo zote utembee uchi ama vaa kwa mtindo huu.

Anzia chupi igeuze nje ndani halafu ivae mbele nyuma fanya hivo kwa nguo zote soks na viatu kulia kushoto. Halafu tembea kawaida tu hatakiona. Ungekuwa mtu mzima ungekimbia ukastuoia akili zinarudi upo kijijiji cha 8. Ndo ungejiuliza umefikaje huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 

🤣🤣🤣 ah kudadeki. Hapa umetubeba , mkuu. Huo muda wa kuvua/kubadili nguo unapata wapi?
 

Lol mihadarati hii, mkuu.
 
Mkuu mimi nilikimbilia ndani shenzi likawq linazunguka nyumba likisonya balaa [emoji3][emoji3][emoji3] asee na lilinibamba nje huko nakojoa ile kuangalia pembeni naona kivuli kama cha mtu ila kirefu kinoma kugeuka nyuma kwanza nikakutana na sonyo kaliii. [emoji23] jikitu refu balaa. Nguzo ya umeme cha mtoto. Mkojo mwingine sijui ulitoka wapi maana nilikuwa nishamaliza kukojoa ndo narudisha dushe mahala pake. Basi nikaamua kutoka nduki hivyo hivyo mtu mzima nilijikojolea siku hiyo mpaka kitandani.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…