Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Naunga mkono kwa kiasi chake
mama angu bibi yake mzaa mama alikua mwanga mno Aliwatafuna watoto wa kwanza wa wajukuu zake wote wa kike na baadhi ya mama zangi wadogo hawajazaa mpaka leo.

Mama aliniambiaga kuwa chochote unachotaka kufanyiwa kishirikina lazima mchawi wa ukoo wenu akithibitishe. Kama hakithibitishi hufanyiwi kitu ( ni kama hukumu ya kunyongwa mpaka rais atie sahihi) akanipa mfano; Mkiwa ndani asubuhi mkiamka lazima nyumba muifungue wenyewe mtoke nje, mtu wa nje hawezi kufungua kuingia ndani. Kwahiyo hapo kwenye ukoo hapo nakubaliana huwenda ndio maana hatuoni mauza uza ila pia anakiukizaga mikoba ya bibi huyo kairithi nani [emoji3]
 
Share nasi mkuu baadhi ya mambo kama elimu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
malizia kwanza hii.
 
[/QUOTE]

We jamaa nikiangalia avatar yako naona kivuli, nikirudi kwenye muandiko wako najikuta nakuwazia "mambo ya ajabu ajabu". Mkuu huna mambo ya kiganga-ganga kweli??
 

We jamaa nikiangalia avatar yako naona kivuli, nikirudi kwenye muandiko wako najikuta nakuwazia "mambo ya ajabu ajabu". Mkuu huna mambo ya kiganga-ganga kweli??
[/QUOTE]
Hayo ni mawazo yako tu
 
We jamaa nikiangalia avatar yako naona kivuli, nikirudi kwenye muandiko wako najikuta nakuwazia "mambo ya ajabu ajabu". Mkuu huna mambo ya kiganga-ganga kweli??
Hayo ni mawazo yako tu
[/QUOTE]
Oya transpoter endelea kumwaga vitu.
 
Umenikumbusha two years ago nikiwa nimepanga maeneo flani hivi DSM ..nilikuwa naishi kwenye chumba na sebule maeneo hayo ..nikiwa na wapangaji wenzangu ila wengi walikuwa wanafunzi wa chuo...mama mwenye nyumba tulikuwa hatuishi nae ila alikuwa mtata mno na kwa taarifa za chinichini nilisikiaga alikuwa mfuasi mzuri wa mambo ya kishirikina...

nilikuwa naishi mwenyewe so muda mwingi nilikuwa nakuwa kazini ..mara nyingi home nakuwa jioni na muda wote nikiwa home mimi ni mtu wa kujifungia ndani na kuangalia movies ..

siku hiyo nimetoka job late hours nimechoka kinoma...nilifika home na kwenda kuoga nikarudi zangu nikawa nachat na michepuko yangu mwishowe kama kausingizi kakanipitia ghafla kuja sijui nini kilinistua usingizini mara papu nikaona mtu yupo kwa juu anaelea kwenye ungo ...najaribu kupiga kelele sauti haitoki ...kitu nilichoweza ni kuchukua simu yangu na kukirushia na kutimua nje mbio...

baada ya lile tukio nilihama ile nyumba ndani ya week mbili ...nilikopata pesa ya kodi wala sikumbuki niliitoa wapi..lakini tangu nimehama nile nyumba hususani ile apartment yangu mpaka leo imekosa mpangaji.

UCHAWI UPO NA NGUVU ZA GIZA ZIPO ..Jambo jema ni kumtemgemea Mungu tu.!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sio Yesu kweli?
 
Elezea ilikuaje
Mzee anasimulia Zamani za Kale, Kipindi katoka akumuoa Mama yangu alitoka Kupata Kilaji Kidogo kwenye Kasenta Ketu hako ( Mji wetu) around 1960s.

Sasa ile anarudi home, yaani Kufika Junction ambapo kupafikia Nyumbani ni Kama Mita 200, akakutana na huyo Jamaa Mrefu. Mshua alikuwa anakula Fegi, anakwambia Fegi Ikadondoka Palepale, ile Kukimbia, aisee anakuta Karibia Kunapambazuka ndiyo akili inamrejea yupo takribani 25Kms toka home. Ndiyo akaanza Kujikongoja Kureje home karibia Kumepambazuka tayari.
 
Ufyongo wote huu umeuona peke yako.
 
Na ww unakula fegi.?[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh pole mkuu vp walivyoawaachia hamkuwafata na mapanga asubuhi huku mkitema povu?
 
wakuu mie binafsi sijawahi kukutana na kisa kikubwa chakutisha kivile sema kunakimoja ambacho kilitokea ambacho kinanipa maswali mpaka iitwayo leo

ilikuwa ni kipindi flani wazee wangu wanapata huduma ya kiroho ka waumini wengine katika kanisa flani basi wakawa wanapata shuhuda mbalimbali toka kwa wenzao basi nao wakataka nao wapate baraka hizo za Mungu maana hakuna asiyezitaka ukizingatia nao walikuwa na shida zao. Basi wakaendelea kufanya taratibu zao ka kawaida ili wawezepata kibali chao cha kumshuhudia Mungu wao namie nikiwa ka mtu wa kando ka hayo mambo hayaniusu. Wakaendelea kupata maombi na kuhudhuria ibada basi siku moja kiongozi wao wa kiroho akawaahidi kufika nyumbani kwaajili ya kufanya maombi na kuombea nyumba na familia kwa ujumla

Day one alifika mida ya usiku ka mida ya saa mbili, ikiwa mama ndo alikuwepo akanialika namie kuweza kupata baraka na mengine ya kiroho, mchungaji akafanya maombo kiasi pamoja na wasaidizi wake baada ya muda akasema nitakuja sikunyingine kwaajili ya maombi tena. basi akaondoka. na mzazi akaondoka siku iliyofuatia mie ndo nikaachwa kwaajili ya kumpokea kiongozi huyo wa kiroho siku atakayokuja.

Siku iliyofuatia baada ya siku kadhaa ilikuwa ngumu kumpata kiongozi huyo wa kirohoo maana alikuwa anahudumia watu wengi na alikuwa busy na majukumu mengine ya Kanisa, nikafanya jitihada za kuwasiliana nae mara kwa mara basi akaniahidi one day atafika.

Hiyosiku aloyofika akafika salama maana alikuwa anatokea mbali kiasi na alifika mida ya usiku maana alitoka kutoa huduma sehemu nyingine basi akafanya maombi nikiwa nae na baadhi ya watu wengine baada ya hapo akaanza kumwaga maji ya baraka nyumba nzima na vyote vilivyokuwepo nyumbani hasa magari na nyumba zote na vyumba vyote, baada ya hapo akarudi tena akafanya maombi kiasi then akaniambia twende nje.

Tukazunguka kwenye eneo la nje akaanza kutafuta tafuta akaniambia ka naona kitu, nikamjibu sioni akatafuta tena na tena kwakutumia mwanga wa simu basi akaanza kusema 'lilikuwa linataka kukimbia tena na leo' basi akakiona kumbe ilikuwa kibuyu na kichupa vimefungwa pamoja na vinashanga na kitu ka irizi nyeusi na nyekundu, nilistaajabu sana. akanijuza kuwa ilikuwa inataka kukimbia na ndo maana siku ya kwanza alishindwa kuikamata. na hizo zana za kishirikina zilikuwepo sehemu nyeupe ambayo ni rahisi kuviona ila akaniambia vilikuwa ndani ya banda lililokuwepo karibu ila kwakuwa alimwaga maji yaliyobarikiwa kikashindwa kukimbia kikaishia hapo nje na akanijuza kwa macho ya kawaida huwezi ona

Mpaka leo najiuliza sana hivi ule ushirikina ulitoka wapi na uliwekwa pale nyumbani toka lini na unawezaje kukimbia pindi nguvu ya Mungu ijitokezapoooo? Mpaka leo lile tukio huwa nalikumbuka sana na vile kibuyu kilivyousisimua moyo wangu.
 
Huna Nyota inayowaka! hii yako imezima kabisa! tunachotaka wachawi ni mwili wenye bahati njema za kuzaliwa! tuna uwezo wa kuwajua! tunajua Ma-Rais, Wafanya biashara! Viongozink , wengine hazitoki wengine zinatoka kabisa!

Ndo pale unaona mtoto hapendi shule, wakati alianza vizuri, Ugonjwa, kufukuzwa kazi, ulevi nk, Mzazi akilegea tu zina chukuliwa mapema utotoni.
 
Kaeni na minyota yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…