Mimi nitasimulia kisa kimoja tu, tena cha utotoni maana kiliniogopesha sana kwa umri ule wa miaka isiyofika hata kumi. Hiki ni kisa kati ya visa vingi vya nguvu za giza nilivyovishuhudia, na ninavyoendelea kuvishuhudia mpaka kesho. Mnivumilie na mnisamehe mdogo wenu maana nitaandika kurasa ndefu.
Picha linaanza pale marehemu mama(PKA mama yangu mzazi, na Mungu akurehemu kwa rehema zake) alipoolewa na baba yangu. Kwa miaka zaidi ya mitatu, mama hakuweza kukaa na ujauzito zaidi ya miezi mitatu, na badala yake mimba ziliharibika.
Mama aliisha kwa masimango, na kuonekana sawasawa na papai linalobeba corona badala ya vitamin! (Ni mchezo uliokuwa ukichezwa na majirani zetu, wenyej wa Kigoma, na Ukweleni hapo)....Lakini mama hakuchoka kuvumilia, na kumwomba Mungu.
Hatimaye mama akashika ujauzito wangu, haukutoka tena, na nikazaliwa pale MNH, na nikaitwa jina la "dawa ya Mungu", maisha yakaendelea kijijini kwetu Boko.
Katika makuzi yangu, utotoni wazazi wangu walikumbana na matukio na changamoto nyingi za kukatisha tamaa. Kuna wakati usiku mama alimka na akakuta sipo kitandani, ananitafuta kwa mda mrefu wakiwa na mzee, hatimaye wananikuta chini ya uvungu wa kitanda nalia, au wananikuta kwenye pembe ya nyumba, mama alikuwa akilia weee, hatimaye maisha yanaendelea. Ilifika mda nikiwa na umri wa mwaka na nusu, nililishwa nyama ya kisigino ya maiti, niliumwa sana kutikana na hili chupuchupu nilambe udongo, wazazi walipambana, Mungu akasaidia, nikatoka salama.
Balaa kwa macho yangu, lilikuwa hapa sasa. Nikiwa darasa la pili, miaka hiyo ya tisini nilitokewa na tukio la kwanza, mubashara ambalo lilinitisha sana maana hapa niliona kwa macho na akili zangu. Usiku nikiwa nimelala ghafla nywele nikahisi zinasisimuka, damu inaenda mbio, na mwili unachemka....ghafla nikashtuka na kuamka paaap! Uso kwa uso na mwanaume aliyeshika kitanda changu, miguuni mwangu nywele zake zinawaka moto mkubwa ila haziteketei, macho yake yanawaka moto kama mkaa wa moto, na mikucha mirefu.
Kulia kwangu, wanawake wanne wakiwa uchi kabisa, wamebeba vyungu kichwani vinawaka moto. Kushoto kwangu wanaume watatu wapo uchi nao wamebeba vyungu, nao vinawaka moto, na mtu mmoja wa kiume(jini) mrefu akikaribia kugusa paa, mweupe kwa rangi(mwarabu) amevaa miwani mweupe, kanzu ndefu, nyeupe mpaka chini, na alikuwa na ndefu ndefu kiasi.
Tukakaziana macho sana, nikawa nawageukia wote mithili nataka niamke niwarukie ila nahisi nazuiwa, nataka kupiga kelele sauti haitoki. Baada ya dakika kama 3 au 4, nikaanza kuuona ukuta kwenye pembe ya nyumba, mubashara unafunguka na wanaanza wanawake kutoka nje kinyumenyume, wakifuata wanaume, na yule jini anakuwa wa mwisho. Hatimaye ukuta unajifunga tena baap! Na hatimaye ndo sauti inatoka mamaaaaaaa........!!!
Mama na baba wanakuja, wananikuta nalia na nimeloa jasho mwili mzima. Hatimaye nawasimulia, mama analia sana, ananikumbatia, na anamlilia Mungu, ananichukua ananipeleka chumbani kwake kwenda kulala nao chumbani kwao. Mama akaniambia watoto ni malaika, huona majini na wachawi ila ukikua hutowaona. Ila haikuwa hivyo mimi mpaka kesho hawa washenzi hawakatishi anga zangu.
Asubuhi ikafika, nikajiandaa kwenda zangu shule, na mama akaniambia kwa sasa hali ilipofikia itabidi niwe nalala na mbwa chumbani kwangu, yaani mbwa anafungwa kwenye mguu wa kitanda changu. Hii ilinisaidia ila hawa washenzi walimuua mbwa wetu(PKA Jeck) ni mbwa aliyepambana sana na hawa washenzi, ila usiku mmoja alipiga kelele kushtuka damu zinamtoka puani na mdomoni ndo ukawa mwisho wake Jeck wangu.
Hili ni tukio mojawapo kati ya matukio mengi niliyokumbana, na ninayokumbana nayo. Ila kama ukilala unaamka tu flesh bila kuona haya mavitu, muombe Mungu akujalie hivyo hivyo. Haya mavitu yanatisha sana.
Asanteni, na poleni kwa kuwachosha!
Sent using
Jamii Forums mobile app