Njoo uifahamu Taxi Mtandao BOLT/UBER

Uber ya gari na pikipiki ipi inabeba wateja sana?
Piki piki Ina kimbiza sana ila ni kama zinafatana TU...japo kihesabu mwenye gari akikomaa anaweza kulaza hesabu nzuri kwasababu bei ya gari IPO juu kidogo ki nauli...ni mara 2 ya nauli ya pikipiki au zaidi
 
Unaweza kunisaidia kufungua account
 
Xaw nmekupata kiongoz je kwa ufahamu wako ni steps zpi nikizifata ntapata leseni ya latra kwa wakati na itachukua mvda gani na nikishapata hyo leseni najiunga moja kwa moja au k una kingne cha ziada
 
mkuu vp gharama za kufata ili kupata leseni ya latra
Latra ni shilingi elfu 35 TU Kwa kibari Cha tax mtandao...huduma hii hata Kwa pikipiki inaitwa tax mtandao hivyo usije ukazani gharama hiyo ni Kwa tax gari...inaweza ikawa sawa sawa na tax gari...ukikata ile ndogo ya elfu 15 inakuwa ni kituo kimoja TU Yani unaruhisiwa kuwa na kijiwe kimoja...ila tax mtandao inaruhusiwa kupakia abiria sehemu yoyote abiria alipo ilimradi TU sehemu hiyo iwe inaruhusi pikipiki au gari kuingia...maana Kuna maeneo gari binafsi haziruhisiwi kuingia au pikipiki
 
Xaw nmekupata kiongoz je kwa ufahamu wako ni steps zpi nikizifata ntapata leseni ya latra kwa wakati na itachukua mvda gani na nikishapata hyo leseni najiunga moja kwa moja au k una kingne cha ziada
Latra unaweza kuitengeneza na kuilipia ndani ya nusu saa...na siku hiyo hiyo ukaenda kuchukua...unatakiwa utembelee tovuti Yao huko utafungua akaunti Kisha utapewa control number utalipia...then unaenda ofisi ya Latra na lisiti Kisha watakuprintia...ni rahisi sana.
 
hapo kwenye pikpik uhakika na huchukua muda gani mpaka kuipata.Tatizo la utapeli limekuwa shida sana kiasi kwamba hata kitu kiwe cha kweli tunaogopa.
Hakuna utapeli piga izo namba siwezi kuweka namba za mataperi...harafu Mimi ni verified user...siwezi kuweka data ambazo sijazifanyia utafiti ili mtu atapeliwe...ukiwa na hiyo pesa laki nne au tatu ukailipia ofisini Kwa siku hiyo hiyo unapewa pikipiki...hakuna utapeli...na hawatokubali ulipie endapo pikipiki zitakuwa zimeisha ..na Huwa wakimaliza pikipiki utasubiri Hadi kesho...zikiwepo ndio unalipia na kupewa chombo Yako...na PIKIPIKI zao ni mpya kabisa unatoka maganda mwenyewe
Hapo ni ofisini kwao baada ya kulipia mwenye hiyo pikipiki akakabidhiwa ... Muulize bodaboda yeyote kuhusu WATU CREDIT atakwambia habari zao.
 
madaraja ya pikipiki ni
A
A1
A2
A3

je nikiwa na A plain tu naweza kusajili kuendesha pikipiki zote hadi bajaji maana haya madalaja ya pikipiki diyaelewi wengne wanasema A plain ni kubwa kuliko zote wengne wanaema bajaji A plain hauendeshi mpka uwe na A3
 
A plain ni Kwa pikipiki yenyewe ndio inampa uwezo dereva kuendesha pikipiki kubwa Zaidi ya cc250... ila haikupi uwezo wa kuendesha pikipiki ya magurudumu matatu lakini hata hivyo Madaraja ya awali ya pikipiki na bajaji upatikanaji wake ni rahisi...tembelea ofisi za TRA au tovuti ya T.R.A portal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…