Njoo uufahamu mji wa Ninawi alipotumwa nabii YONA

Jackwillpower

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2017
Posts
2,467
Reaction score
3,687

Ninawi ni wapi?

Ninawi ni mji uliokuwepo kaskazini mwa Taifa la Iraq kwasasa. Mji huu kwasasa haupo, ila mahali pale ulipokuwepo mpaka leo pako!. Na mji huu ndio uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru.

Ashuru ilikuwa ni nchi iliyokuwepo maeneo ya Iraq, Uturuki, na Syria..Mataifa haya matatu yamechangia sehemu ya nchi hiyo ya Ashuru, kama vile mataifa matatu (Kenya, Uganda na Tanzania), yalivyo na sehemu katika ziwa Victoria, kadhalika na Iraq, Uturuki na Syria ni sehemu ya Taifa hilo liliokuwa linaitwa Ashuru.

Lakini kwasasa duniani hakuna Taifa linaloitwa Ashuru. Kwani baada ya mataifa hayo matatu kuzaliwa hilo la Ashuru likafa.

Na Uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru, uliitwa NINAWI. Ninawi ndio mji Nabii Yona alioambiwa akahubiri Injili, lakini kinyume chake akakimbilia Tarshishi.

Tarshishi ni mji uliokuwepo nchi ijulikanayo kwasasa kama Lebanoni. Taifa la Lebanoni katika nyakati za kale ndio Taifa lililokuwa linaongoza kwa uzalishaji wa miti aina ya MIEREZI
Mji mkuu wa Taifa la Lebanoni, ndio ulikuwa Tarshishi. Mji huu wa Tarshishi ndio uliokuwa unaongoza kwa wafanya biashara, na ndio uliokuwa kitovu cha biashara ulimwenguni. Nabii Yona alikimbilia mji huu kwasababu ulikuwa na fursa nyingi

Mji wa Ninawi haukuwa mji wenye watu wengi sana lakini ulikuwa umeendelea sana. Kipindi Nabii Yona anatumwa kwenda kuhubiri huko, biblia inarekodi mji ule kuwa na watu 120,000 tu!.

Yona 4:10 “Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja;
11 na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?”
Ijapokuwa Mungu alikusudia kuuadhibu mji huu lakini wenyeji wake walitubu kwa mahubiri ya Yona. Na Bwana Yesu alikuja kutoa unabii kwa vizazi hivi vya siku za mwisho kuwa..

Mathayo 12:41 “Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; KWA SABABU WAO WALITUBU KWA MAHUBIRI YA YONA; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona”.
Na sisi tunapaswa tutubu kwa mahubiri ya Bwana Yesu, ili tusije kuangukia hukumu siku ya Mwisho.

Ninawi walikuwa wameitikia wito wa mahubiri ya Yona na wakageuka kutoka kwa njia zao mbaya kumtumikia Bwana Mungu Yehova. Lakini miaka 150 baadaye, Ninawi ikarudi kuabudu sanamu, vurugu na kiburi (Nahumu 3: 1-4). Kwa mara nyingine tena Mungu akatuma mmoja wa manabii wake Ninawi kuhubiri hukumu katika uharibifu wa mji na kuwaonya watubu. Cha kusikitisha, watu wa Ninawi hawakutilia maanani onyo za Nahumu na mji ukawekwa chini ya utawala wa Babeli.

Habari za kuangamizwa kwa mji wa Ninawi ni miongoni mwa nabii za kushangaza ambazo maelezo yake yanapatikana katika Biblia. Habari hizi zilitabiriwa na Nabii Nahumu mwaka 700 K.K. Katika utabiri wake alitabiri kuwa mji mkubwa huu, utaangamizwa kabisa na hautajengwa tena. Unabii huu ulitimizwa mwaka 606 K.K, wakati Wamedi walipouharibu na kuuteketeza. Sawasawa na maneno ya Nabii Nahumu, mji huu haujawahi kujengwa

1648165955664.png

1648165974084.png

kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) katika taarifa yake ya habari hivi karibuni lilitangaza kwamba namba ya wakristo imeshuka kutoka milioni 1 na laki tano mwaka 2003 mpaka 350,000 - 450,000, ambapo wengi wao waliobakia wanaishi vijijini kama kijiji cha Qaraqosh ambacho pia kinafahamika kwa jina lingine kama Baghidada, Bartella, -Hamdaniya pamoja na Tel Kef ambavyo vipo ndani ya Ninawi. mwishoni mwa mwaka juzi wakristo waliamliwa kuondoka katika mji wa Mosul, tamko lililotolewa na wanajeshi wa Sunni (moja ya majeshi makubwa ya kiislamu) na mpaka kufikia jumamosi iliyopita wakristo wengi waliamua kuhama mji huo na kukimbilia miji ya karibu inayokaliwa na wakristo, kwa mujibu wa ripoti kutoka vyombo vya habari vya kimataifa vinasema wakristo waliamua kuondoka Mosul wakiacha samani zao nyuma na kuondoka na nguo walizovaa tu na kukimbilia kijiji cha Al Qosh mji mkubwa wa wakristo ambao unadaiwa kabla majeshi hayo ya kiislamu kuchukua mji ulikuwa na wakristo wafikao 30,000 lakini toka june mwaka jana wakristo waliosalia waliamua kuukimbia mji.

(Popote ulipo maombi yako ni muhimu sana kwa ndugu zetu hawa).
 
Ninawi ni wapi?

Ninawi ni mji uliokuwepo kaskazini mwa Taifa la Iraq kwasasa. Mji huu kwasasa haupo, ila mahali pale ulipokuwepo mpaka leo pako!. Na mji huu ndio uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru.

Ashuru ilikuwa ni nchi iliyokuwepo maeneo ya Iraq, Uturuki, na Syria..Mataifa haya matatu yamechangia sehemu ya nchi hiyo ya Ashuru, kama vile mataifa matatu (Kenya, Uganda na Tanzania), yalivyo na sehemu katika ziwa Victoria, kadhalika na Iraq, Uturuki na Syria ni sehemu ya Taifa hilo liliokuwa linaitwa Ashuru.

Lakini kwasasa duniani hakuna Taifa linaloitwa Ashuru. Kwani baada ya mataifa hayo matatu kuzaliwa hilo la Ashuru likafa.

Na Uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru, uliitwa NINAWI. Ninawi ndio mji Nabii Yona alioambiwa akahubiri Injili, lakini kinyume chake akakimbilia Tarshishi.

Tarshishi ni mji uliokuwepo nchi ijulikanayo kwasasa kama Lebanoni. Taifa la Lebanoni katika nyakati za kale ndio Taifa lililokuwa linaongoza kwa uzalishaji wa miti aina ya MIEREZI
Mji mkuu wa Taifa la Lebanoni, ndio ulikuwa Tarshishi. Mji huu wa Tarshishi ndio uliokuwa unaongoza kwa wafanya biashara, na ndio uliokuwa kitovu cha biashara ulimwenguni. Nabii Yona alikimbilia mji huu kwasababu ulikuwa na fursa nyingi

Mji wa Ninawi haukuwa mji wenye watu wengi sana lakini ulikuwa umeendelea sana. Kipindi Nabii Yona anatumwa kwenda kuhubiri huko, biblia inarekodi mji ule kuwa na watu 120,000 tu!.

Ijapokuwa Mungu alikusudia kuuadhibu mji huu lakini wenyeji wake walitubu kwa mahubiri ya Yona. Na Bwana Yesu alikuja kutoa unabii kwa vizazi hivi vya siku za mwisho kuwa..

Na sisi tunapaswa tutubu kwa mahubiri ya Bwana Yesu, ili tusije kuangukia hukumu siku ya Mwisho.

Ninawi walikuwa wameitikia wito wa mahubiri ya Yona na wakageuka kutoka kwa njia zao mbaya kumtumikia Bwana Mungu Yehova. Lakini miaka 150 baadaye, Ninawi ikarudi kuabudu sanamu, vurugu na kiburi (Nahumu 3: 1-4). Kwa mara nyingine tena Mungu akatuma mmoja wa manabii wake Ninawi kuhubiri hukumu katika uharibifu wa mji na kuwaonya watubu. Cha kusikitisha, watu wa Ninawi hawakutilia maanani onyo za Nahumu na mji ukawekwa chini ya utawala wa Babeli.

Habari za kuangamizwa kwa mji wa Ninawi ni miongoni mwa nabii za kushangaza ambazo maelezo yake yanapatikana katika Biblia. Habari hizi zilitabiriwa na Nabii Nahumu mwaka 700 K.K. Katika utabiri wake alitabiri kuwa mji mkubwa huu, utaangamizwa kabisa na hautajengwa tena. Unabii huu ulitimizwa mwaka 606 K.K, wakati Wamedi walipouharibu na kuuteketeza. Sawasawa na maneno ya Nabii Nahumu, mji huu haujawahi kujengwa

View attachment 2164512
View attachment 2164513
kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) katika taarifa yake ya habari hivi karibuni lilitangaza kwamba namba ya wakristo imeshuka kutoka milioni 1 na laki tano mwaka 2003 mpaka 350,000 - 450,000, ambapo wengi wao waliobakia wanaishi vijijini kama kijiji cha Qaraqosh ambacho pia kinafahamika kwa jina lingine kama Baghidada, Bartella, -Hamdaniya pamoja na Tel Kef ambavyo vipo ndani ya Ninawi. mwishoni mwa mwaka juzi wakristo waliamliwa kuondoka katika mji wa Mosul, tamko lililotolewa na wanajeshi wa Sunni (moja ya majeshi makubwa ya kiislamu) na mpaka kufikia jumamosi iliyopita wakristo wengi waliamua kuhama mji huo na kukimbilia miji ya karibu inayokaliwa na wakristo, kwa mujibu wa ripoti kutoka vyombo vya habari vya kimataifa vinasema wakristo waliamua kuondoka Mosul wakiacha samani zao nyuma na kuondoka na nguo walizovaa tu na kukimbilia kijiji cha Al Qosh mji mkubwa wa wakristo ambao unadaiwa kabla majeshi hayo ya kiislamu kuchukua mji ulikuwa na wakristo wafikao 30,000 lakini toka june mwaka jana wakristo waliosalia waliamua kuukimbia mji.

(Popote ulipo maombi yako ni muhimu sana kwa ndugu zetu hawa).
Ninawi mji wa Ashuru (Siria kwa Sasa). Waashuru ndiyo waliteka na kuwachukuwa utumwa Isirael ya kasikazini ambayo makao makuu yalikuwa Samaria. Bablion (Iraqi kwa Sasa) ndiyo waliwapolomosha waashuru pia bablion ndiyo waliteka Isirael ya kusini (Yudea) ambayo makao makuu yalikuwa Yerusalem. Umedi na uajemi (Irani kwa Sasa) ndiyo walimpolomosha Mbabeloni. Kitabu Cha Ester Kama wimbo wa bahati bukuku unasimlia story ya mfalme na malkia. Baada ya hapa wagiriki walichukua ukanda wa mashariki ya Kati na Asia ndogo na badae waroma wakaja. Waroma ndiyo walifunga kazi mwaka 70 baada ya Yesu kuisambalatisa Yerusalem chini ya Mpompei. Lakini mwaka 79 waroma katika makao makuu yao huko Mpompei palipigwa na volcano na mji huo wote kufunikwa. Nikitazama Vita vya Urusi na Ukrein naiona sawa sawa na Vita ya Bablion na Isirael.
 
amen mkuu
 
Sidhani kama Tarshishi ilikuwa Lebanon. Miji ya kibiashara ya Lebanon ilikuwa Tiro(Tyre) na Sidon. Na mwingine uliitwa Tripoli.
 
Mi nahisi hata Kaole Bagamoyo itakuwepo ktk biblia kwa jina lingine sema tu fitna za Walatino.
 
Sidhani kama Tarshishi ilikuwa Lebanon. Miji ya kibiashara ya Lebanon ilikuwa Tiro(Tyre) na Sidon. Na mwingine uliitwa Tripoli.
Mji wa Tarshishi ni mji ambao ulikuwa mahali panapoitwa Tiro..ambapo kwa sasa ni nchi ya Lebanoni…Nchi ya Lebanoni ni nchi iliyopo kaskazini mwa Israeli, kama vile Kenya ilivyo kaskazini mwa Tanzania (Na mpaka leo hiyo nchi inaitwa hivyo hivyo Lebanoni haijabadilika, inakaliwa na Waarabu sasahivi, lakini haina tena utajiri/ushupavu uliokuwa nao wakati ule)..

Sasa wakati wa vipindi vya wafalme wa Israeli nchi hii ya Tiro (Lebanoni) ambao mji wake mkuu ni Tarshishi ndio ulikuwa ni mji wa kibiashara mkubwa kuliko miji mingine yote. Ulikuwa unasifika kwa kuwa na MERIKEBU NYINGI ZA KIBIASHARA kuliko miji mingine yote. Na ulikuwa ni mji wenye uzoefu wa ki-biashara

Biblia inasema katika kitabu cha Ezekieli…

Ezekieli 27:12 “Tarshishi alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa utajiri wa kila aina; kwa fedha, na chuma, na bati, na risasi, walifanya biashara, wapate vitu vyako vilivyouzwa”
Yeremia 10: 9 “Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi,….”.
Unaona? Vilevile Miti ya Mierezi ambayo ilitumika katika ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani, ilitoka huko Lebanoni, kulikuwa hakuna mahali pengine ambapo miti hiyo ilikuwa inapatikana, na njia ya usafirishaji iliyokuwa inatumika kusafirishia miti hiyo ni bahari (Njia ya Maji). Kwa ufupi sehemu kubwa ya malighafi za ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani zilitoka huko Tiro, ambao mji wake mkuu ni Tarshishi. Hata Dhahabu Sulemani alizozitumia kutengenezea vyombo vyake zilitoka huko Lebanoni..Sulemani alinunua dhahabu nyingi kutoka huko Lebanoni mpaka kufikia kiwango cha kuwa tajiri sana hata kuona kutumia madini ya fedha(silver) kutengenezea vito vyake ni kama kujishushia heshima..

1Wafalme 10: 21 “Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; hakuna vya fedha, fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani.
22 Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.
23 Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima.”
Huko Tarshishi walikuwepo pia manahodha waliobobea sana, na pia kulikuwa na watu wenye elimu ya ujenzi kubwa sana..baadhi ya wajenzi wa hekalu lile la mfalme Sulemani aliwatolea huko huko Lebanoni.

Hivyo ipo mistari mingi sana katika biblia inayoelezea ushupavu wa Tarshishi…ipo mingi sana unaweza kuipitia kwa muda wako upatapo nafasi…Kasome (Ezekieli 27: 25-27, Ezekieli 38:13, 1Wafalme 22: 48, ).

Sasa kwa kuielewa sifa ya Huu mji wa wa Tarshishi tunaweza kujua ni kwanini Yona alikimbilia huko…Na kwanini alipanda merikebu…Kumbuka kutoka Israeli mpaka Tarshishi(huko Lebanoni) kulikuwepo na njia ya nchi kavu nzuri tu..lakini yeye alikwenda kupanda merikebu. Ni sawa leo mtu atake kwenda Tanga..aache kupanda basi achague kutumia ferry/meli pale bandarini Dar es salaam aende Tanga. Ni lazima anayo sababu ya kufanya hivyo..

Na ni wazi kuwa sababu yenyewe si nyingine Zaidi ya biashara…Yona pengine alikuwa na mizigo yake anakwenda kufanya biashara.. Tarshishi haukuwa mji wa kitalii..ulikuwa ni mji wa kibiashara..hivyo alipoisikia sauti ya Mungu ikimwambia aende Ninawi kuhubiri yeye akaona njia pekee ya kuipotezea hiyo sauti ni kuzama kwenye biashara zake…wala hakuchagua kukimbilia miji mingine kama Misri, au Moabu ambayo angepata pumziko..yeye alikuwa na sababu ya kwenda Tarshishi.. Angalau apate riziki kidogo.
 
Mji wa Tarshishi ni mji ambao ulikuwa mahali panapoitwa Tiro..ambapo kwa sasa ni nchi ya Lebanoni…Nchi ya Lebanoni ni nchi iliyopo kaskazini mwa Israeli, kama vile Kenya ilivyo kaskazini mwa Tanzania (Na mpaka leo hiyo nchi inaitwa hivyo hivyo Lebanoni haijabadilika, inakaliwa na Waarabu sasahivi, lakini haina tena utajiri/ushupavu uliokuwa nao wakati ule)..

Sasa wakati wa vipindi vya wafalme wa Israeli nchi hii ya Tiro (Lebanoni) ambao mji wake mkuu ni Tarshishi ndio ulikuwa ni mji wa kibiashara mkubwa kuliko miji mingine yote. Ulikuwa unasifika kwa kuwa na MERIKEBU NYINGI ZA KIBIASHARA kuliko miji mingine yote. Na ulikuwa ni mji wenye uzoefu wa ki-biashara

Biblia inasema katika kitabu cha Ezekieli…

Unaona? Vilevile Miti ya Mierezi ambayo ilitumika katika ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani, ilitoka huko Lebanoni, kulikuwa hakuna mahali pengine ambapo miti hiyo ilikuwa inapatikana, na njia ya usafirishaji iliyokuwa inatumika kusafirishia miti hiyo ni bahari (Njia ya Maji). Kwa ufupi sehemu kubwa ya malighafi za ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani zilitoka huko Tiro, ambao mji wake mkuu ni Tarshishi. Hata Dhahabu Sulemani alizozitumia kutengenezea vyombo vyake zilitoka huko Lebanoni..Sulemani alinunua dhahabu nyingi kutoka huko Lebanoni mpaka kufikia kiwango cha kuwa tajiri sana hata kuona kutumia madini ya fedha(silver) kutengenezea vito vyake ni kama kujishushia heshima..

Huko Tarshishi walikuwepo pia manahodha waliobobea sana, na pia kulikuwa na watu wenye elimu ya ujenzi kubwa sana..baadhi ya wajenzi wa hekalu lile la mfalme Sulemani aliwatolea huko huko Lebanoni.

Hivyo ipo mistari mingi sana katika biblia inayoelezea ushupavu wa Tarshishi…ipo mingi sana unaweza kuipitia kwa muda wako upatapo nafasi…Kasome (Ezekieli 27: 25-27, Ezekieli 38:13, 1Wafalme 22: 48, ).

Sasa kwa kuielewa sifa ya Huu mji wa wa Tarshishi tunaweza kujua ni kwanini Yona alikimbilia huko…Na kwanini alipanda merikebu…Kumbuka kutoka Israeli mpaka Tarshishi(huko Lebanoni) kulikuwepo na njia ya nchi kavu nzuri tu..lakini yeye alikwenda kupanda merikebu. Ni sawa leo mtu atake kwenda Tanga..aache kupanda basi achague kutumia ferry/meli pale bandarini Dar es salaam aende Tanga. Ni lazima anayo sababu ya kufanya hivyo..

Na ni wazi kuwa sababu yenyewe si nyingine Zaidi ya biashara…Yona pengine alikuwa na mizigo yake anakwenda kufanya biashara.. Tarshishi haukuwa mji wa kitalii..ulikuwa ni mji wa kibiashara..hivyo alipoisikia sauti ya Mungu ikimwambia aende Ninawi kuhubiri yeye akaona njia pekee ya kuipotezea hiyo sauti ni kuzama kwenye biashara zake…wala hakuchagua kukimbilia miji mingine kama Misri, au Moabu ambayo angepata pumziko..yeye alikuwa na sababu ya kwenda Tarshishi.. Angalau apate riziki kidogo.
Maelezo yako mazuri, Lakini Tarshish haikuwa Lebanon. Ilikuwa ng'ambo ya Mediterania, haijulikani ni wapi hasa, lakini si Lebanon.
 
Sidhani kama Tarshishi ilikuwa Lebanon. Miji ya kibiashara ya Lebanon ilikuwa Tiro(Tyre) na Sidon. Na mwingine uliitwa Tripoli.
Tarshish ni eneo mbali ya fukwe ya Israel katika bahari ya Mediterranean, Tarshish haipo Lebanon, tusifananishe Tyre/ Tiro na Tarshish. Tarshish ni Jamii ya watu waliotoka katika kizazi cha Japhet mtoto wa Nabii Noah. Walikaa eneo la Magharibi mwa Ugiriki, Kusini ya Italy za leo hadi Kusini Magharibi mwa Ufaransa na Hispania. Kwa Tafsiri isio rasmi naweza sema, Tarshish ni MATAIFA YA MAGHARIBI YA LEO. Ingawa Tarshish alichanganya damu na Makabila 10 ya Israel yaliopotea ili kupata huo Umagharibi. Kumbuka Ezekiel 38, 39 na 40, inapozungumzia Tarshish (Europeans), na Simba Wake ambao ni USA, Australia, Canada, na New Zealand, siku za mwisho katika vita vya Gog, watakavyomsema Gogu (Russia, Iran, Turkey, Kush na wengine) wanapoenda kuivamia Israel. Biblia, Tarshish + Ten lost tribe of Israeli unapata EUROPEANS, alafu Tarshish YOUNG LIONS, ni USA, Canada na Australia, maana hizi 3 zimetoka kwa Tarshish. Soma Ezekiel utaelewa.
 
Back
Top Bottom