Jackwillpower
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 2,467
- 3,687
Ninawi ni wapi?
Ninawi ni mji uliokuwepo kaskazini mwa Taifa la Iraq kwasasa. Mji huu kwasasa haupo, ila mahali pale ulipokuwepo mpaka leo pako!. Na mji huu ndio uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru.
Ashuru ilikuwa ni nchi iliyokuwepo maeneo ya Iraq, Uturuki, na Syria..Mataifa haya matatu yamechangia sehemu ya nchi hiyo ya Ashuru, kama vile mataifa matatu (Kenya, Uganda na Tanzania), yalivyo na sehemu katika ziwa Victoria, kadhalika na Iraq, Uturuki na Syria ni sehemu ya Taifa hilo liliokuwa linaitwa Ashuru.
Lakini kwasasa duniani hakuna Taifa linaloitwa Ashuru. Kwani baada ya mataifa hayo matatu kuzaliwa hilo la Ashuru likafa.
Na Uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru, uliitwa NINAWI. Ninawi ndio mji Nabii Yona alioambiwa akahubiri Injili, lakini kinyume chake akakimbilia Tarshishi.
Tarshishi ni mji uliokuwepo nchi ijulikanayo kwasasa kama Lebanoni. Taifa la Lebanoni katika nyakati za kale ndio Taifa lililokuwa linaongoza kwa uzalishaji wa miti aina ya MIEREZI
Mji mkuu wa Taifa la Lebanoni, ndio ulikuwa Tarshishi. Mji huu wa Tarshishi ndio uliokuwa unaongoza kwa wafanya biashara, na ndio uliokuwa kitovu cha biashara ulimwenguni. Nabii Yona alikimbilia mji huu kwasababu ulikuwa na fursa nyingi
Mji wa Ninawi haukuwa mji wenye watu wengi sana lakini ulikuwa umeendelea sana. Kipindi Nabii Yona anatumwa kwenda kuhubiri huko, biblia inarekodi mji ule kuwa na watu 120,000 tu!.
Ijapokuwa Mungu alikusudia kuuadhibu mji huu lakini wenyeji wake walitubu kwa mahubiri ya Yona. Na Bwana Yesu alikuja kutoa unabii kwa vizazi hivi vya siku za mwisho kuwa..Yona 4:10 “Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja;
11 na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?”
Na sisi tunapaswa tutubu kwa mahubiri ya Bwana Yesu, ili tusije kuangukia hukumu siku ya Mwisho.Mathayo 12:41 “Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; KWA SABABU WAO WALITUBU KWA MAHUBIRI YA YONA; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona”.
Ninawi walikuwa wameitikia wito wa mahubiri ya Yona na wakageuka kutoka kwa njia zao mbaya kumtumikia Bwana Mungu Yehova. Lakini miaka 150 baadaye, Ninawi ikarudi kuabudu sanamu, vurugu na kiburi (Nahumu 3: 1-4). Kwa mara nyingine tena Mungu akatuma mmoja wa manabii wake Ninawi kuhubiri hukumu katika uharibifu wa mji na kuwaonya watubu. Cha kusikitisha, watu wa Ninawi hawakutilia maanani onyo za Nahumu na mji ukawekwa chini ya utawala wa Babeli.
Habari za kuangamizwa kwa mji wa Ninawi ni miongoni mwa nabii za kushangaza ambazo maelezo yake yanapatikana katika Biblia. Habari hizi zilitabiriwa na Nabii Nahumu mwaka 700 K.K. Katika utabiri wake alitabiri kuwa mji mkubwa huu, utaangamizwa kabisa na hautajengwa tena. Unabii huu ulitimizwa mwaka 606 K.K, wakati Wamedi walipouharibu na kuuteketeza. Sawasawa na maneno ya Nabii Nahumu, mji huu haujawahi kujengwa
kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) katika taarifa yake ya habari hivi karibuni lilitangaza kwamba namba ya wakristo imeshuka kutoka milioni 1 na laki tano mwaka 2003 mpaka 350,000 - 450,000, ambapo wengi wao waliobakia wanaishi vijijini kama kijiji cha Qaraqosh ambacho pia kinafahamika kwa jina lingine kama Baghidada, Bartella, -Hamdaniya pamoja na Tel Kef ambavyo vipo ndani ya Ninawi. mwishoni mwa mwaka juzi wakristo waliamliwa kuondoka katika mji wa Mosul, tamko lililotolewa na wanajeshi wa Sunni (moja ya majeshi makubwa ya kiislamu) na mpaka kufikia jumamosi iliyopita wakristo wengi waliamua kuhama mji huo na kukimbilia miji ya karibu inayokaliwa na wakristo, kwa mujibu wa ripoti kutoka vyombo vya habari vya kimataifa vinasema wakristo waliamua kuondoka Mosul wakiacha samani zao nyuma na kuondoka na nguo walizovaa tu na kukimbilia kijiji cha Al Qosh mji mkubwa wa wakristo ambao unadaiwa kabla majeshi hayo ya kiislamu kuchukua mji ulikuwa na wakristo wafikao 30,000 lakini toka june mwaka jana wakristo waliosalia waliamua kuukimbia mji.
(Popote ulipo maombi yako ni muhimu sana kwa ndugu zetu hawa).