NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Hawajibu maswali kwasababu wanajua wanachokifanya...! Yani ni wiziwizi tu,ukiacha visenti vyako ukija lazima ukute vimepungua..
 
NMB Tanzania ni kwanini mmeacha kutuma electronic bank statement za kila mwezi kwenye email.

Kuna uhusiano wowote na huu utaratibu mpya wa kukata tsh 5300 bila maelezo yoyote?
Hii nimehangaika nao sana. Ukiwafuatilia wanakutumia kwa mwezi mmoja au miwili halafu hawatumi tena. Mpaka ufuatilie. Sababu wanazotoa ni either hakuna network au hawaoni kama umeomba uwe unapatiwa e-statement kila mwezi. Ni sababu juu ya sababu. Badala ya kuweka hivi vitu viwe automated kutuma statement, wao bado wako manual
 
Hivi NMB kwa nini mkitangaza kazi za kuapply kwa kutumia system huwa mnachezea system na kumfanya muombaji asiweze kutuma Maombi ya kazi?,..nashauri msiwe mnatangaza ajira muwe mnachukuana kimya kimya.
 
NMB Mmegeuka Kuwa Wanyonyaji Msio na Huruma Kwa Watanzania

Hivi inaingia Akilini Kwa Kuchajiwa Tsh 7,800 kwa kuhamishq Tsh 100,000 kutoka Benki kwendq Airtel Money?

Narudia tena Mmekuwa Wanyonyaji Bila kuwa na Aibu

DON'T BE ANNOYED IF I DECIDED TO END SERVICES WITH YOUR BANK
 
NMB/VODA huu wizi mtaacha lini?. Napiga *150*66# ili nipate huduma ya bank mkononi. Naambiwa huduma hii kwa sasa haipatikani, lakini nakuta kiasi cha Tsh 50 mmekata kwenye simu yangu wakati sijapata huduma. Narudia tena *150*66#. Nafika hatua ya nne kuelekea huduma ninayohitaji, naambiwa 'huduma hii kwa sasa haipatikani'. Naangalia salio, mmekata Tsh 200 kutoka kwenye simu yangu. Huu ni wizi. Kulipia ni sawa, lakini ulipie ukiwa umepata huduma unayokusudia.
Hii ni aibu kwa kaliba yenu na mnaojitanabahisha kufuata sheria za nchi. Mnakera sana.
Naamini ipo siku mtakutana na mwizi mwenzenu, atawaburuza na mtalipa gharama kubwa, iwe ya pesa ama taswira ya kampuni.

Wakatabahu
INFOPAEDIA
 
Mbona ninyi hampunguzi riba kwenye mikopo...
 
Nataka kufungua account kesho alihamis.
Je nije na nini na nini ili kesho hio hio nifungue account?
 
Nmb mkononi app kwa android inashindikana kulogin baada ya kufanya updates kwenda android 13
 
#NMB msipo badirika kwa kushusha riba watumishi wengi watawakimbia na kuhamia #CRDB.. Nimeshuhudia kundi kubwa la watumishi wakijaza fomu za kuhamishia mishahara yao CRDB baada ya riba kupunguzwa hadi 13%.. NMB kwenye swala la TOP UP mmechemka yani unamkopo NMB unaenda kutop up unapigwa balaa wakati ukienda CRDB wanalinunua hilo deni la NMB na wanakupa ela nzuri...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…