NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Bora nyie mnaotokea hapa jukwaani kwa ajili ya kukidhi kiu ya maswali na ushauri kwa wateja wenu
Maana wenzenu NBC wako hoi kitandani na hawana hata habari juu ya yale yanayoandikwa kwenye mitandao juu ya benki yao
Hongereni sana kitengo cha mawasiliano kwa umma NMB kwa mrejesho huu mnautupatia, Hakika nyinyi ni wadau wa kweli katika maendeleo ya taifa hili
Natamani taasisi zote zikaiga mfano huu
HEKO NMB HEKO TANZANI

Nilisajili Account yangu ikiwa na vielelezo vyote per BOT requirements

Wame block account yangu bila maelezo ya kutosha. Nimepeleka details zangu upya, hii ni wiki ya pili hazijafanyiwa kazi.

Ukichukua pesa dirishani utabambikiwa noti za mia tano tano mpaka utakoma! Imagine nilipewa Tshs 500,000 katika note za 500!

NBC ipo ICU kweli!
 
Safi sana NMB,tumieni Jamii forum zaidi kuliko links mlizotoa ambazo watu wengine ambao hawataki kufahamika kutokana na mitandao yao ya ulaji kuweza kutudhuru.

Hapa singida hupati loam bila kupitia vishoka/wapiga debe ambao hutoza kuanzia laki mbili na kuendelea ili kupata mkopo wa nmb.Mkitaka fanyeni kuwapigia wateja wenu waliokopa kama 20(watumishi) muwa interview mpate picha ya ninacho waeleza
 
Hongera Nmb hii ndiyo Tanzania tunayo itaka Bado PPF
 
Nimeipenda sana hii najua ipo siku nitafungua NMB soon
 
Ndugu wana jamii forums,

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe Siri)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Hongereni kwa hatua na uamuzi mliouchukua. Mtawavumilia baadhi ya member wenye kutanguliza midomo michafu,yaweza kuwa sababu za wifi wa kibiashara na mengineyo.Ila kusema kweli kama mtakuwa wafuatiliaji wazuri mtafaidika na maoni ,malalamiko na ushauri toka kwa wengi wa member humu ambao yaweza kuwa nusu ni wateja wenu.

Naamini mara mpokeapo matusi na viroja toka kwa baadhi ya member wakorofi MODs watakuwa makini kuishughulikia mara moja.

Moja la msingi imarisheni na simamieni vizuri suala la Wafanyakazi kuwa na ID wawepo Ofisini,ili iwe rahisi kwa wateja kuwa tambua kwa majina na kurahisisha uwasilishaji wa malalamiko dhidi ya wahusika kwa huduma mbovu kuliko hadithi ya oh! yule mweupe sijui rangi gani nk.
 
Idara ya mikopo pamoja na managerment kujitutumua kudhibiti RUSHWa bado hamjafanikiwa kudhibiti urasmu huo dhidi ya wakopaji. NMB KITENGO CHA MIKOPO SHIDA IKO.
 
ni mfano wa kuigwa kwa taasisi nyingine,

1. upatikanaji wa mkopo umeanza kuwa mgumu kwenu kuna baadhi ya watumishi wenu kama maafisa mikopo bila ten percent upati mkopo utaishiwa kupangiwa tarehe tena kibaya zaidi wanashirikiana na ma branch manegar.

2.niliwahi fika pale mliman city nmb kuna mama mmoja mfupi hivi mweupe kama ana mguu mbovu mama anajua nini anafany it mean anawajibika ipasavyo kauli nzuri na mapokez ya ukwel ongera mama mweupe.

3 kuna siku kad yangu ilinasa mwananyamal hosp ilibid niifate post samora nmb kama mwezi wa sit au wa saba kuna dada alikuwa mjamzito yale majibu na dharau sitorudi tena pale kiukwel nilijisikia vibaya yuko pale mapokez inaonekana kama controllar pale reception
 
nmb mtwara baraka mwasandube jamani kaka yule mpeni ufanyakazi boraaa
maana anajituma hadi raha
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe “Siri”)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Great! Looks nice of you!
 
ni mfano wa kuigwa kwa taasisi nyingine,

1. upatikanaji wa mkopo umeanza kuwa mgumu kwenu kuna baadhi ya watumishi wenu kama maafisa mikopo bila ten percent upati mkopo utaishiwa kupangiwa tarehe tena kibaya zaidi wanashirikiana na ma branch manegar.

2.niliwahi fika pale mliman city nmb kuna mama mmoja mfupi hivi mweupe kama ana mguu mbovu mama anajua nini anafany it mean anawajibika ipasavyo kauli nzuri na mapokez ya ukwel ongera mama mweupe.

3 kuna siku kad yangu ilinasa mwananyamal hosp ilibid niifate post samora nmb kama mwezi wa sit au wa saba kuna dada alikuwa mjamzito yale majibu na dharau sitorudi tena pale kiukwel nilijisikia vibaya yuko pale mapokez inaonekana kama controllar pale reception

Tena sasa hivi wamesimamisha mikopo kwa baadhi ya taasisi. Kuna tatizo gani
 
NMB Tanzania hongera sana kwaa kuja jf!
_Hakuna bank yenye huduma nzuri za mikopo nzuri hapa Tanzania kama NMB nishakopa bank nyingi sijaona kama NMB!

__Tatizo moja tu rushwa rushwa idara ya mikopo..

mi niko mwanza nshakopa mara nyingi na hakuna wakati sijatoa rushwa tena afisa analazimisha kama tumefanya naye biashara
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe “Siri”)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

NMB mpo local sana tunaomba muingie kwenye mfumo wa VISA na MASTER card ili angalau ukiwa nje ya nchi uweze kuendelea kupata huduma.
 
NMB Tanzania hongera sana kwaa kuja jf!
_Hakuna bank yenye huduma nzuri za mikopo nzuri hapa Tanzania kama NMB nishakopa bank nyingi sijaona kama NMB!
__Tatizo moja tu rushwa rushwa idara ya mikopo..
mi niko mwanza nshakopa mara nyingi na hakuna wakati sijatoa rushwa tena afisa analazimisha kama tumefanya naye biashara
Ni vyema muwataje wahusika kukomesha haya yote
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom