Habari
leo mchana mida ya saa sita na nusu mchana nimepokea message hii," IMETOA SH. 8,000 KWENYE A/C INAYOISHIA NA 00469 TAREHE 1-2-2017 12.27". nilichofanya nilichungulia wallet nayo nikakuta ipo salama isiwe nimebiwa kadi.
baada ya kukaa na kulinganisha message nyingine huwa wanaweka "KAMA HUTAMBUI MUAMALA HUU PIGA 0800 11 22 33".
Sasa nikatafuta ki peperushi cha NMB tariff guide 2016 na kukisoma kwa makini. kuna mahali pameandikwa ANNUAL CARD MAINTANCE chap*2 0.00, standard card 8,000, titanium 10,000 na world reward 100,000. kwenye MONTHLY MAINTANCE FEE ni 1,600 kwa personal, student, wisdom na current a/c.
hii imekaaje maana bado nina maswali mengi. nimepiga namba ile haijapokelewa mpaka napoandika uzi huu. na ukipiga mahesabu 1,600*12months plus 8,000 ni kama 22,700 kwa mwaka either u draw pesa au ufanye huduma yoyote ya kibenki.
embu fafanueni hiyo 8,000 ni ya nini
asante