NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Mtu akifungua Account kwa utaratibu wenu huwezi kupata ATM card siku hiyo hiyo, ni kwa nini?

Kutokana na sababu hiyo, kama akiwa na shida ya fedha kabla hajapata ATM CARD analazinika kwenda kutolea fedha COUNTER.
Gharama ya kutolea fedha counter (TELLER WITHDRAWAL FEE) ni 3,400/= kwa muamala mmoja ambapo gharama ya kutoa fedha kwa ATM CARD ni 1,000/= kwa muamala mmoja.

Upatikanaji wa kadi hiyo mtu akipata mapema sana ni wiki mbili wanazosema lakini inawezekana muda mrefu zaidi ya mwezi. endapo kwa kipindi hicho mtu atakuwa na mahitaji ya fedha toka benk mara kadhaa, ataingia gharama kubwa za kutolea fedha COUNTER jambo ambalo linasababishwa na NMB yenyewe

USHAURI
1. Mteja ni mfalme anahitaji kubembelezwa
2. Kutokuwa na ATM CARD si kosa lake bali ni NMB kushindwa kumpa CADR papo hapo anapofungua Account
3. System ya NMB isome na kumtambua mteja mpya mpaka atakapopewa ATM CARD
4. System ya NMB kwa kumtambua mteja mpya imkate 1,000/= au chini ya hapo lwa kila muamala wa kutoa fedha mpata atakapopatiwa ATM CARD yake.
5. System ya NMB imtambue nteja aliyekwisha kupatiwa kadi kama myeja wa kawaida na endapo atachukulia fedha counter achajiwe hiyo 3,400/=
6. Kiwango cha 3,400/= kwa muamala ni kikubwa mmno bora kipunguzwe kuwa 2,000/=
 
kwanza nianze kwa kuwapongeza baadhi ya wafanyakazi wanatambua wajibu wao kwaba wapo pale kwaajili ya nini?lakini pia naomba nielekeze kero yangu idara ya mikopo branch ya mafinga watumliotuwekea pale sidhani kama wanafahamu wajibu wao mm nijuavyo mkopo ni biashara lakiniwao nadhani wanaona kama wanatoa msaada pale ofsin maana wamekuwa na majibu ya dharau na hawanahabari na mtejakwa leo naishia hapo
 
NMb ATM card zenu zile za blue mpya hazitoi hela kwanini mnaleta usumbufu kwa wateja ,rekebisheni hiyo foleni ndeefu ni shida
 
NMb ATM card zenu zile za blue mpya hazitoi hela kwanini mnaleta usumbufu kwa wateja ,rekebisheni hiyo foleni ndeefu ni shida
aise nimesikia hivyo, leo watu wanatoa tu pesa kwa NMB mobile. jingajinga sana NMB.
 
Tangu jana huduma za NMB kwa kutumia master card hazipo kabisa.

Tatizo ni nini?
Siamini kama NMB hawajui tatizo labda wameamua tu kupuuzia.
Wenye Visa card huduma ziko safi.

NMB tekelezeni wajibu wenu.
 
Tangu jana huduma za NMB kwa kutumia master card hazipo kabisa.
Tatizo ni nini?
Siamini kama NMB hawajui tatizo labda wameamua tu kupuuzia.
Wenye Visa card huduma ziko safi.

NMB tekelezeni wajibu wenu.
Yamenikita leo hii, maana nimejenga tabia huwa sitembei na hela mfukoni kwa kujifanya mjuaji kuwa ATM zipo nyingi, hapa nimekaa chini pembeni ya ATM najicheka[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah Leo nilikuwa NMB ku-Issue Nmb MasterCard , kwahyo nimeingia cha kike

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…