NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Nimepoteza kadi yangu, naomba utaratibu wa kupata nyingine
Unaenda kuripoti polisi kisha utapatiwa "loss report" , utaipeleka taarifa hiyo ya kupotelewa kadi benki kwa ajili ya kujaza fomu ya maombi ya kadi mpya
 
Idara ya Mikopo ya hii bank pale Bank house utendaji ni zero, NMB ebu tembeleeni Loan dept za benki nyingine mpate mfano,mmewaweka akina mama pale wanadonoa keyboards mteja mmoja wanahudumia dakika 45!

Na kuonyesha bado mpo kiujima katikati ya huduma hata Maboss wao wanawapigia simu na kuwaita ofisini na unaweza kuachwa kwenye meza hata 20 min ofisi yote imeenda kwa Boss!

Ukitaka kujua kwa nini Mashirika ya umma yalibinafsishwa tembelea hii department ,wale akina mama wapeni vitengo vingine hawaendani na kasi ya idadi ya wateja
 
Kuna tangazo lenu la Nmb Trade Financial, sasa mbona haliendani uhalisia,

Nilifika moja ya Branch zenu na Nina business account ya umri wa miaka6 kwa ajiri ya kuomba mkopo kama contractor lakini sikufanikiwa kupata niliambiwa mzunguko wa akaunti yangu ni mdogo mbele ya kuwa nina mikataba ya kazi za construction na supplier!

Hii Nmb trade financial inawalenga watu wa aina gani?
 
OK.Nimewapata ila nachukia midada inayovaa nusu uchi kama Malaya wa uwanja wa Fisi.Pls rekebisheni na hili ivi mnamvalia nano vinguo vifupi? Mnatuketa sana.
 
Hivi nyie mnaakili kweli?,hiii pesa mnanikopesha au ni yangu niliiweka ili mnihifadhie ?,inakuwaje nikija kuitoa kwa shida zangu binafsi mnataka kujua NATOA KWA AJILI YA MATUMIZI GANI?,aisee this is too much na mnavuka mipaka...........JIBU LA HII FOMU KWA JINSI NILIVYOIJAZA NI UJUNBE TOSHA KWENU,msinipangie wala kutaka kujua matumizi ya pesa zangu.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
NMB Magomeni huduma mbovu mno. Nilizungushwa zaidi ya wiki kufungua akaunti nikaamua kwenda NMB Ilala ikanichukua chini ya lisaa kupata akaunti. NMB Magomeni wachunguzwe na kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu kuanzia boss hadi yule wa chini kabisa.
 
Kwa watumishi wekeni mkopo wa miaka 20 hadi 30 kwa makato madogo zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…