NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Nimepoteza kadi yangu, naomba utaratibu wa kupata nyingine
Unaenda kuripoti polisi kisha utapatiwa "loss report" , utaipeleka taarifa hiyo ya kupotelewa kadi benki kwa ajili ya kujaza fomu ya maombi ya kadi mpya
 
Idara ya Mikopo ya hii bank pale Bank house utendaji ni zero, NMB ebu tembeleeni Loan dept za benki nyingine mpate mfano,mmewaweka akina mama pale wanadonoa keyboards mteja mmoja wanahudumia dakika 45!

Na kuonyesha bado mpo kiujima katikati ya huduma hata Maboss wao wanawapigia simu na kuwaita ofisini na unaweza kuachwa kwenye meza hata 20 min ofisi yote imeenda kwa Boss!

Ukitaka kujua kwa nini Mashirika ya umma yalibinafsishwa tembelea hii department ,wale akina mama wapeni vitengo vingine hawaendani na kasi ya idadi ya wateja
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote,

NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.


Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Kuna tangazo lenu la Nmb Trade Financial, sasa mbona haliendani uhalisia,

Nilifika moja ya Branch zenu na Nina business account ya umri wa miaka6 kwa ajiri ya kuomba mkopo kama contractor lakini sikufanikiwa kupata niliambiwa mzunguko wa akaunti yangu ni mdogo mbele ya kuwa nina mikataba ya kazi za construction na supplier!

Hii Nmb trade financial inawalenga watu wa aina gani?
 
Bora nyie mnaotokea hapa jukwaani kwa ajili ya kukidhi kiu ya maswali na ushauri kwa wateja wenu
Maana wenzenu NBC wako hoi kitandani na hawana hata habari juu ya yale yanayoandikwa kwenye mitandao juu ya benki yao
Hongereni sana kitengo cha mawasiliano kwa umma NMB kwa mrejesho huu mnautupatia, Hakika nyinyi ni wadau wa kweli katika maendeleo ya taifa hili
Natamani taasisi zote zikaiga mfano huu
HEKO NMB HEKO TANZANI
OK.Nimewapata ila nachukia midada inayovaa nusu uchi kama Malaya wa uwanja wa Fisi.Pls rekebisheni na hili ivi mnamvalia nano vinguo vifupi? Mnatuketa sana.
 
Hivi nyie mnaakili kweli?,hiii pesa mnanikopesha au ni yangu niliiweka ili mnihifadhie ?,inakuwaje nikija kuitoa kwa shida zangu binafsi mnataka kujua NATOA KWA AJILI YA MATUMIZI GANI?,aisee this is too much na mnavuka mipaka...........JIBU LA HII FOMU KWA JINSI NILIVYOIJAZA NI UJUNBE TOSHA KWENU,msinipangie wala kutaka kujua matumizi ya pesa zangu.
IMG_20180125_133128_870.JPG
 
Hivi nyie mnaakili kweli?,hiii pesa mnanikopesha au ni yangu niliiweka ili mnihifadhie ?,inakuwaje nikija kuitoa kwa shida zangu binafsi mnataka kujua NATOA KWA AJILI YA MATUMIZI GANI?,aisee this is too much na mnavuka mipaka...........JIBU LA HII FOMU KWA JINSI NILIVYOIJAZA NI UJUNBE TOSHA KWENU,msinipangie wala kutaka kujua matumizi ya pesa zangu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
NMB Magomeni huduma mbovu mno. Nilizungushwa zaidi ya wiki kufungua akaunti nikaamua kwenda NMB Ilala ikanichukua chini ya lisaa kupata akaunti. NMB Magomeni wachunguzwe na kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu kuanzia boss hadi yule wa chini kabisa.
 
Kwa watumishi wekeni mkopo wa miaka 20 hadi 30 kwa makato madogo zaidi
 
Back
Top Bottom