NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Hello Marashi,
Hii ni huduma ya kuchukua kiasi cha mshara wako kabla ya siku ya mshahara kuweza kujikimu na shughuli mbalimbali
Jiju swali unaloulizwa. Sizungumzii mikopo. Mimi ninazo hela NMB, sasa nilitaka kujua kama naweza kwenda kwa wakala kuwithdraw bila kadi. Nijibu swali hili achana na mambo ya salary advance me sitaki hayo mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NMB Tanzania nilibadilisha Namba ninayotumia kwenye NMB mobile kwenye ATM na kunirudishia msg kuwa nimefanikiwa kujiunga na Namba hiyo mpya. Hata hivyo nikijaribu kuingia kwa namba hiyo mpya inagoma. Assist pls.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Expire date ya atm card inapofika kwann msii update ileile tu bila kutengeneza nyingine?,na Kama kutengeneza labda kama imepotea au kuvunjuka?,majibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiju swali unaloulizwa. Sizungumzii mikopo. Mimi ninazo hela NMB, sasa nilitaka kujua kama naweza kwenda kwa wakala kuwithdraw bila kadi. Nijibu swali hili achana na mambo ya salary advance me sitaki hayo mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwezi kutoa hela kwa wakala bila kadi kwani huwa kuna mashine lazima kadi ifanyiwe swap na uingize password

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana ijumaa, nilitoa pesa kwenye acc yangu na kupeleka kwenye MPESA namba yangu, kwenye acc imetoka na kwenye MPESA haijafika. Napiga simu nikasubirishwa zaidi ya nusu saa. Sio mbaya ni kweli kuwa kwenye nahitaji ya Huduma yenu tu wengi.

Lakini nilipopata nafasi ya kuongea na customer care Frank, akanieleza kuwa jambo hilo ni mpaka j3 kwa kuwa jumamosi na jumapili kazi hakuna NMB.
Sasa kwa suala kama hilo na ndo mtu inategemea kutoa hicho alicho nacho kimsaidie mgonjwa wake, familia yake na mambo mengine.

MNA utaratibu gani wa kuweza kutatua jero kama hiyo? Na kwa njia hiyo mnaweza kushikilia Wateja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mteja wa NMB. Nilipoteza line ya simu ambayo nilikuwa nimejiunga na NMB Mobile. Kwa bahati mbaya hata namba ya simu nimeisahau.

Nimekwenda NMB Makambako na kujaza fomu zaidi ya mara nne mpaka sasa ili kurejeshewa huduma ya NMB Mobile lakini mpaka sasa imeshindikana kabisa.
Naomba msaada wa kurejesha huduma hiyo.
 
Toeni salary advance kama mtu ana dharura imsaidie mbona mlianza vizuri? Kama huduma imesitishwa pia mseme kwani kila ukiomba unaambiwa Masaa 48 ambayo nayo yanapitiliza. Tunahoji humu mpo kimya
 
Huwezi Amini juzi kati nimeenda Nmb Dodoma naulizia Washroom(Toilets) naambiwa choo kimeharibika niende nje kuna Baa kuna choo cha kulipia. Ajabu sana Bank kubwa makao makuu ya nchi hakuna choo cha wateja....

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo NMB Dodoma Brach..kuna afande mmoja yupo ndani Pale Yeye uwa Ni kufukuza Wateja Tu.Kauli zake Ni Mbaya.Kuna Siku Nafika Kufanya Transaction pale Nikawa Very Disappointed na Kauli zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.


Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:


Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.


4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom


Airtime top-up or Luku purchases, kuna gharama za kutumia huduma? (Service charges)
 
Huduma ya online banking ipo NMB au imeshakufa? kama ipo mbona wahudumu wenu hawaijui vizuri maana wanaulizana utadhani imeingia leo Tanzania.

Nilienda pale clock tower branch Arusha, nikajaza fomu miezi miwili naulizia tu wao wanadai itakuwa tayari kwa hiyo niingie tu online, nikabaki nashangaa... whaaaat?

Niingie online bila username wala password wala other security setup.... Nimeamua kuachana nao.
Ushauri : Acheni kukimbizana kuintroduce na kuiga vitu vipya kila kukicha ingawa vya zamani hamjaviweka vizuri, ni bora muwe na huduma chache lakini bora.
 
Nmb inachukua mda gan??card yang ilipotea Ktk mazingira tata,nikapiga cm ifungwe baadae nikaletewa na msamalia mwema ,nikaenda branch il ifunguliwe ,wakaifungua mda huohuo nikaenda kweny ATM ikamezwa nikaenda ndani wakaitoa nikaenda reception nikawambia mbona hamjaifungua nikarudi kwenye machine ikamezwa tena ,nikaondoka leo siku ya tatu sijaefata ,Wenda kesho nikaichukue ,,so swali langu baada ya mda gani nilipaswa niitumie ???
 
Hivi salary advance kukopa ni maramoja?.kwa mfano juzi nilikopa 13000,leo najaribu imegoma kabisa, why?
 
Back
Top Bottom