NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Tawi lenu la NMB Wami hapo Morogoro mjini ni janga.Huduma wanatoa kwa kujitakia.Mteja anakaa foleni masaa matatu,akifika kwa mhudumu anaambiwa mstari aliopo si sahihi arudi nyuma.Hakuna wa kuelekeza.

Pia kuna wahudumu wanafanya kazi kwa kujitakia, anahudumia mteja mmoja, halafu anaanza soga ilhali kuna wanaosubiri.

Pia,kwa sababu za kufahamiana tu kuna watu wanapitiliza bila kusimama foleni na kwenda kuhudumiwa.
 
Huu ukurasa wenu wa facebook mlifungua wa nini? Yaani mteja anauliza swali kwenye ukurasa wa facebook anajibiwa aulize tena kupitia whatsapp! Maajabu gani haya?

Kwa nini asijibiwe waziwazi kwani huduma hizi ni siri?

Hamtaki kutaja hadharani maana huwa mnatupandishia makato kimya kimya bila kututaarifu.

View attachment 1733177
View attachment 1733180
 
Sasa hapa umekuja kuwashtaki? Ungewafuata huko WhatsApp walikokuelekeza ungekuta ushatatuliwa shida yako.

Au tukutafutie mkalimani?
 
NBC ukienda ndani wameweka kwemye display makato ya hizo mambo kwa kiwango
 
Sasa hapa umekuja kuwashtaki? Ungewafuata huko WhatsApp walikokuelekeza ungekuta ushatatuliwa shida yako.

Au tukutafutie mkalimani?
Wala siyo mimi ila nlisoma tu comments zao.

Ila pia kumbka usipowasemea wenzako siku zamu yako ikifika pia hutopata wa kukusemea.
 
bado riba ya mikopo kwa watumishi wa umma ni kubwa sana.

Hii Bank ilipaswa haswa iwasaidie watumishi kwa kuwa mishahara yao inapitia hapo.
 
Naomba kujua vipi vigezo muhimu vya kufungua a/c
 
punguzeni Riba kwa watumishi wa Umma, bado Riba ni kubwa sana, pia wapeni mikopo ili wajikwamue kiuchumi.

ingieni mikataba na wafanya biashara wa magari ili wakopeshwe magari kupitia mishara yao kama ilivyo kwa wabunge.

jifunzeni kwa wengine.
 
Mankato tuu tatizo kwangu
 
Habari Nmb bank Tanzania ,

Naomba kujua kuhusu fixed account ..naomba ntolee mfano ,nikitaka kufungua fixed account nkaweka 5milions (5000,000) Baada ya mwaka itongezeka faida ya sh ngap

Nimeskia skia kuwa kuna rate kati ya 5% to 7.5% per year so nataka nipate jibu la uhakika kutoka kwenu

Asanteni
 
toeni mikopo ya magari kama ilivyo kwa wabunge, kwanini inashindilana kwa wengine
 
Habari za usiku
Hivi NMB mmetosheka na wateja sasa eeh
Ni miezi sita sasa nahangaika jinsi ya kurudisha NMB mobile account kila nikifika pale Mlimani City naambulia kuandika barua kisha nikiwapigia customer care wanasema haijawa uploaded.

Hii labda kwa sababu mimi sio mfangakazi wa serikali kwa maana umma.

So naomba mniruhusu nikatoe pesa yangu nihamie kwa wengine

Nakumbuka siku naenda pale Ilala kufungua account niligombaniwa nilijiskia faraja sana ila sasa hivi nikiwa na shida ya kurejesha mobile service inashindikana halafu sasa nilishaizoea.


Ahsante
 
Naomba kuuliza sisi watumiaji wa iPhone tutapata lini huduma ya NMB mobile app?
 
Tangu jana nafatilia mkopo branch yenu bank house nyaraka zote ninazo kama muaniriwa ila naambiwa hakuna network cjui inarud lini?
 
Mkuu huo mchakato unatakiwa kaufanyie kwenye ATM ya NMB kama utakuwa ulijiunga na huduma ya NMB mobile hauhitaji kujaza form unaenda ATM TU unachomeka kadi yako kisha
 
NMB nimeprocess mkopo hii wiki ya 4 bado sijawekewa na niliambiwa ni ndani ya saa masaa 48. Kwanini nyie sio wakweli?

Muda wote huu ningeshahamishia mshahara wangu CRDB na mkopo ungekuta nimeshapata. Nimechoka nataka nikaubatilishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…