NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Mnaowaita maafisa mikopo wanapenda rushwa umeprocess kila kitu ila miez 6 hamna hela ,pesa zangu,mshahara wangu nikupe iweje sasa waoga hutoa within a week pesa hiyo sasa tutawapa za walee jamaa,fanyeni kaz za watu
 
Manispaa ya Sumbawanga kwa sasa ina idadi kubwa ya watu,kitendo cha kuwa na eneo moja la kutoa pesa si sahihi.Nina hakika huduma inavyotolewa na usumbufu wanaopata wafanyakazi kama kungekuwa na ridhaa ya kujiunga na benki yoyote hakuna mtumishi ambaye angekubali mshahara wake upitie NMB tawi la Sumbawanga.

Kwanini zisifunguliwe ATM mashine maeneo mengine kama wafanyavyo NBC?.
 
Kadi yangu ili expire mwaka jana mwezi wa kumi na toka kipindi hcho sijatumia akaunt yangu inaweza kuwa bado active au ndo ilishafungwa ?
 
Hello
Nimefungua chapchap account tangu 21 July 2015 kwenye tawi la Usa River Arusha, mpaka leo tarehe 27 July 2015 sijaweza kupata huduma yoyote kupitiaATM card niliyopewa, siwezi hata kutuma pesa kupitia NMB mobile isipokuwa kuangalia salio tu, siwezi kutuma pesa.

Nimefika customer care ya hapo nilipofungua kila mara naambiwa kuwa kuna tatizo la network. Halafu gharama za kupitia dirishani ni kubwa mno.
From Arusha.
 
NMB Mmenifedhehesha sana, mshahara umeingia kwenye account yangu ya NMB, mimetoa pesa kwa NMB Moile nakuziweka M-pesa, pesa bank kwenye account yangu zikatoka lakini hazikufika kwenye M-pesa, huu niusumbufu sasa familia yangu itaishije? kama huduma hii haipo nibora muitoe kwenye system kwani huu niusumbufu mkubwa, nimefedheheka sana na sijui pesa yangu kama itarudi kwenye account, na wala sijui itachukua muda gani!! NMB Mmeniumiza sana!
 
NMB Ndio Bank gani???
 
Nmb wahudum wenu wanalinga sana,wao tena ndio mabosi wetu badala ya sisi kuwa wafalme kwao kuanzia magbu na huduma mbovu kuliko damm hate these
 
Kuna mtu amekopa pesa NMB sasa akataka kwenda kulipa lile deni kwa sababu amepata pesa nyingi hivyo hataki tena madeni alipoenda katika ofisi za mkoa aliopo akaambiwa haiwezekani kufanya hivyo. Sasa naomba kujua kutoka kwenu je hili limekaaje?
 
mikopo yenu siku hizi ni ibabaishaji bila ten percent hupati loan.
 
Wafanyakaz bank wanajisahau sana..uu ujinga wao Tanzania tu huko dunian hakuna upuuz kama huu
 
Kuna mtu amekopa pesa NMB sasa akataka kwenda kulipa lile deni kwa sababu amepata pesa nyingi hivyo hataki tena madeni alipoenda katika ofisi za mkoa aliopo akaambiwa haiwezekani kufanya hivyo. Sasa naomba kujua kutoka kwenu je hili limekaaje?

Aende kwa MD wa Bank
 
NMB niliibiwa mishahara kwa two accounts kupitia ATM, nilifuatilia nikaishia kupewa statements zenye negative balance. Iliniuma sana nikafunga kabisaaa account. Sitamsahau yule customer care na manager wa branch walivyoninyanyasa.
 
Ehe !Tena afazali mmejileta wenyewe humu,
Yaani nyie sijui mkoje ?
Nimeomba kutenengeneza kadi miezi 2 na bado sujui nitaipata lini? Na MNA bahati INA hela vinginevyo ningewaachia muweke stoo
 
mimi binafis sijapata shidanao tena ukichukuatu hela kama umejiunga na simu bank inakuletea msg
 
Tatizo kubwa la NMB ni kuweka pesa. Unaweza kuwa na fedha zako ukasema kwamba utakwenda kuziweka benki lakini ukifika unakutaka na bonge la foleni. Unakata tamaa na kuondoka zako. Kesho vivyo hivyo hatimaye pesa inatumika katika matumizi ambayo hukukusudia.

Najua nitajibiwa kwamba niweke kupitia simu. Je hawa wazee wetu wanajua njia hiyo? Benki hizi zinazooonekana ni za kigeni hapa Dar, foleni ikizidi watu sita tu, meneja anakuwa mkali na kwenda kumuuliza kaunta kuna tatizo gani, nyie hamna mameneja?

Kwa nini zile Kaunta za NMB (ambazo utazikuta ni tano au sita) mbili tu ndiyo huwa zinafanya kazi? Kwa nini zile nyingine hazfanyi kazi je, mna uchache wa wafanyakazi?
 
Back
Top Bottom