NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

hongera sana nmb, napenda kuwauliza kwa nini hisa zenu zimeshuka sana sasa hivi?
 
Kuna utapeli utapeli kwenye mikopo hasa kwa watu ambayo hawaelewi mambo ya mikopo.mfano kuna MTU alichukua mkopo mwezi wa kumi tarehe 20 cha ajabu akaanza kukatwa mkopo huo mwezi huohuo .maafisa wenu wa mikopo siwaamini
 
Yaani kama hili tawi lenu la Orkesumeti... yeuwii ni kichefuchefuuu. Muhdumu aliyekuwa mzuri ni Denis peke yake wengine wanaangalia wateja sura.

Asilimia kubwa ya wateja hawajasoma kingereza na kama kiswahili kuelewa mwingne anachelewa mtu kaja kutoa hela au kuweka ukute kakutana na Nabulu full kichefuchefuu...

wkt mwngine unaenda bank tailer hayupo unaambiwa subiri mara kaenda lunch mara cjui kaingia hapo balinga nk hakuna utaratibu wa kupokezana mkasaidiana kama ni mpo wachache?

Na huyu cjui nani ila mtaani ni kadada afadhali tu sasa hayupo maana alikuwa bingwa wa kutoa habari za kibank za wateja na si yeye tu na wengine mtu siri zako za bank znajulikana unash ngapi?umetoa ngapi?umekopa ngapi nk.

Wafanyakazi wa orkesumet wanadharau sana wateja na wanaviburi sijui wanaona kukalia hivyo viti hapo ndio baaasiii ajira yao kuuubwaa kama balozi wa nchi? hawajui ni mgawanyo wa ajira ambapo yeye kunihudumia ni wajibu wake na si nimbembeleze.
 
Orkesumet /monduli/Arusha jamani mikopo inatolewa kwa rushwa... ujamuahd afisa mkopo dau lake na kumruhusu alikate huko juu kwa juu ndugu yangu mkopo uupati Ng'ooo utasikilizia mkopo mdomoni. Otherwise uwe una bwana/hawara humo ktk wafanyakazi lasivyoo njia nyeupeee jiondokee.

CRDB wafanyakazi mameneja mpk mpewe rushwa ndio muwaidhnishie wenzeni mikopo.
 
Nmb why hamuweki tawi au angalau atm maeneo ya chanika na population hii kuchanganya wafanyakaz wa govt wako kibao huku tukitaka huduma eti hadi tuje gomz, angalieni wenzenu wa crdb na dcb wameshtuka kitambo wameshaweka matawi sjui hao watu wenu wa marketing hawalioni hili au ushaur wao unawekwa kapuni halafu mnakuja na ka slogan mlipo tupo pambaf
 
mkuu
Sijajua kama limeshajibiwa hili ila kwa vile customer care ni kumhudumia mteja individually naomba mjibu tu hata kama ninauliza mara ya 111100.

Je mna mpango wa huduma za pesa kwa mtandao? hii namaanisha kuwa kuwe na app kwenye simu za adroid na iOS ambayo mtu akiwa na data tu anaweza kuhamisha pesa, kuona statement ama kuangalia balance bila makato ya kijinga kabisa kama ya sasa. Sijui mnakuaje bank za Tz, eti huduma ya bank mpk niwe na vocha kwenye simu alafu *150*66#, hapo bado bank na nyie mnakata (eti gharama za kuangalia salio) huu ni wizi wa wazi wazi. Sasa kama natumia wi-fi au sipo Tanzania siwezi ona salio/statement/transfer monies.

Wenzetu walishapiga hatua hizo zamani sana, mpaka ukipoteza kadi unapewa nyingine free na haraka.
Je mna huo mpango ama lazima tuwafaidishe wenye mitandao ya simu na nyie?

rant rant rant rant
hiyo kitu wanayo, nilishawahi kuambiwa nijiunge nayo sema hofu zetu na vijisent visije potea. pia mfano mtandao wa tigo sio lazima uwe na salio.
 
NMB IMEKAA KIZAMAN MKOAN UKIFUNGUA ACCOUNT KUPATA ATM MPAKA MWEZ MZIMA UPIE
 
Hii huduma ya NMB mobile ni kero kubwa sana, ni kama wizi fulani hivi!! Hauna ufanisi na gharama mnazokata ni kubwa sana.

Ikitokea huduma haijakamilika, inakuwa ngumu kurudishiwa pesa zako, na kma ukirudishiwa hairudishwi yote, yaani kama nimetuma kiasi cha pesa na ikatokea ile pesa isifike kwa mhusika, inarudishwa kwenye akaunti kwa mbinde sana, mbaya zaidi hela inayokatwa kwaajili ya hiyo huduma hairudishwi wakati huduma haijakamilika, KWANINI?

Huu sio wizi? Mnakera kwa kweli na hii NMB Mobile yenu. Kama hamuwezi kuondoa hizi kero ni bora muifute..
 
Idara ya Mikopo tawi la Geita ni msumali au jipu jingine, linalotakiwa mlitumbue ndani kwa ndani kabla halijatumbuliwa na wengine.

Yupo mtu ( ) anahuska na mkopo kwa wafanyakazi wa serikali mvaa miwani, ukweli hajali mda na mahtaji ya wateja wake.

Istoshe anaelement za rushwa.

Utendaji kazi wake ni jipu, atahudumia mtu mmoja, utaskia internet imekata, wakati wenzake wanaendelea. Akitoka hakudi hata basi kujua kama hiyo net imekudi anaondoka masaa .

Tafadhali wekeni mambo vizuri
 
mkuu

hiyo kitu wanayo, nilishawahi kuambiwa nijiunge nayo sema hofu zetu na vijisent visije potea. pia mfano mtandao wa tigo sio lazima uwe na salio.
Hiyo tigo salio linakatwa kwenye pesa iliyopo kwenye akaunti yako. Hakuna cha bure
 
Hawa jamaa niwaizi kabisa,kwa maana ukibakiza change kidogo kwenye A/C yako,wanaimalizia na dhani ni uadilifu mbovu wa baadhi ya watumishi wake,mteja akiacha vijicenti vyake vinapotea gafla,hasa tunaetumia ATM mobile
 
Hii huduma ya NMB mobile ni kero kubwa sana, ni kama wizi fulani hivi!! Hauna ufanisi na gharama mnazokata ni kubwa sana. Ikitokea huduma haijakamilika, inakuwa ngumu kurudishiwa pesa zako, na kma ukirudishiwa hairudishwi yote, yaani kama nimetuma kiasi cha pesa na ikatokea ile pesa isifike kwa mhusika, inarudishwa kwenye akaunti kwa mbinde sana, mbaya zaidi hela inayokatwa kwaajili ya hiyo huduma hairudishwi wakati huduma haijakamilika, KWANINI? Huu sio wizi? Mnakera kwa kweli na hii NMB Mobile yenu. Kama hamuwezi kuondoa hizi kero ni bora muifute..
Nmb mobile sio huduma ya kisasa, nikiwa sipo Tz nitajuaje salio? Au mitandao yote tu inakubali?

Waweke app kama Jf app, una log in unaangalia salio, tuma pesa na chek statement bureee ili mrad uwe na data tuu
 
nmb salary account baada ya kusimamisha mishahara wangu. kila nilipoweka vihela vyangu akina mkavikata deni la mkopo. inamaana mishahara ukirejeshwa hamtaukata miez hiyo?
 
Mimi maoni yangu ni kua,ninaomba muweke branch au ATM Machine huku maeneo ya Mbezi mwisho(Kimara) ili huduma zitufikie kwa urahisi. Pale Kimara Korogwe kuna ATM lakini sidhani kama inafanya kazi.
 
Hiki ki ATM chenu cha hapa Posta ya Airport DSM ni kama pambo tu, mkiondoe. Hakuna siku nimeenda pale nikakuta kina hela
 
Back
Top Bottom