NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Kuna kazi mlitangaza mwaka jana mwezi wa kumi ya Bank teller southern zone je mmeshaita watu kwenye usaili?
 
Kutoka http://dewjiblog.co.tz/wateja-wa-nmb-sasa-kutuma-pesa-benki-nyingine-kwa-kutumia-nmb-mobile/

NMB imezindua rasmi huduma ya kuhamisha ama kutuma fedha (NMB Mobile T.I.S.S), kutoka katika akaunti za benki hiyo, kwenda kwenye akaunti za benki nyingine, sambamba na kufanya manunuzi na malipo.

NMB.jpg

NMB Mobile T.I.S.S, ni huduma ya kwanza kutolewa na benki nchini Tanzania, ambayo imetajwa kuwa ni njia rahisi, salama na ya haraka katika mchakato wa kutuma ama kuhamisha fedha kutoka NMB kwenda benki nyingine.

Akizungumza katika hafla ya kuitambulisha huduma hiyo kwa wanahabari, Kaimu Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada, Stephen Adili Adili alisema NMB Mobile T.I.S.S ni mwarobaini wa wateja wao kutumia muda mrefu kwenye foleni za kuhamisha ama kutembea na fedha mkononi.

“Huduma hii inakuja kumaliza tatizo la wateja kutumia muda mwingi kwenye mchakato wa kuhamisha fedha. Muda ni mali na kwa kulitambua hilo, tumekuja na huduma hii ambayo inafanyika popote, hata ukiwa ufukweni unapunga upepo,” alisema Adili.

Aliongeza ya kwamba, NMB Mobile T.I.S.S haiishii tu katika kuhamisha fedha kutoka akaunti ya NMB kwenda benki nyingine, bali inaenda mbali na kupokea ama kutuma miamala ya mitandao ya simu za mkononi.

Huduma hiyo inayoweza kutumiwa na wateja wa NMB Mobile, inapatikana kwa mteja kubonyeza alama nyota, kisha namba 150, alama ya nyota, kisha namba 66 na mwisho alama ya reli na kufuata maelekezo (*150*66#)

Naye Geofrey Mwijage, ambaye ni Mkuu wa Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa NMB, alisema benki yake imejidhatiti vya kutosha katika kutanua huduma mongoni mwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

Alisema NMB Mobile T.I.S.S ni inaenda kuwa mshirika sahihi wa Watanzania, katika kuharakisha maendeleo yao na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kuelekea Tanzania ya Viwanda.
 
Wapendwa hii bank ni majanga tu, niliwahi kukopa tawi la newala, Afisa mikopo SWAI alikuwa anachexea Akaunti yangu atakavyo. Kwenda kwa manager anamtetea, kwenda makao makuu wakanijibu nashukughulikia ombi lako mpaka Leo. Hiyo ni Michezo ya maafisa mikopo ni miungu watu hiyo. Nafikiria kuhamia crdb.....
Llll
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Nmb mm sijawaelewa hasa hasa kwenye mikopo yenu pale mtu anapo top up..mfano mwaka jana nimetop up kwa makato ya elfi tisini kwa miaka mitano na deni langu lilikiwa ni sh 2020000....mkakata then nikapewa milioni moja tuu...kwel nliumia sana eti wakaniambia calculation za benk ni tofauti na hizi tunazocalculate...90000×60=5400000-2020000=3380000....ufafanuzi plz maana asilimia 18 ya hiyo hela ni kidogo sanaaa...
 
Naomba kuuliza nikibadili namba ya siri ya NMB mobile na kadi kwenye mashine itabadilika?
 
Ndugu wanajamvi...juzi kunamzee alikuja kuweka pesa NMB kahama branch. Inaonekana alikuwa na zaidi ya Million 20 kwa jinsi alivyokuwa anamlalamikia teller ambaye ni mwnadada.

Mie nilikuwa Nyuma ya mzee kwenye foleni ndo maana niliyasikia mazungumzo yao na malalamiko ya mzee husika. Suala lenyewe lilikuwa hivi, huyu mzee alifika akiwa na burungutu tofautitofauti akakabidhi yakiwa na label eg million 5, million 3 etc. Kilichotokea baada ya mzee kukabidhi pesa zile basi teller akawa anaweka kwenye ile mashine kila burungutu..chaajabu kufika mwisho akasema mashine yake inasoma million kadhaa pungufu ya million 1.5, Yule mzee akasema umezichanganya na hizo note zako nilikuona lakini dada akakataa , akijifanya kumuita meneja na kuangalia ile mashine ya noti, mwisho wakasema kuwa mzee kaleta pesa pungufu.

Mzee kabisha wee lakini hakupata msaada, basi akawa ndo ameibiwa hivyo basi akalazimika kujaza form nyingine ili aingiziwe pesa zile baki. Katika kufuatilia mkasa huu hapa kahama kunawatu wanasema ile branch ya nmb karibu na stendi ni wezi ukizubaa tu unaibiwa.

Kinachomuumiza huyo babu nikuwa pesa yenyewe ilikuwa ya mkopo wa nmb aliopewa motto wake huko morogoro akawa amenunua mpunga huko kahama. Swali je nikwanini wahudumu wa benki ya NMB kahama wanawaibia wateja? hawaoni haya matendo ndo yanafanya watu wasiokuwa na uzoefu na benki waogope kuweka pesa benki?? tujadili ninini kifanyike ili mzee alieibiwa asaidiwe kupata haki yake.
 
Inawezekana pia yule mzee alikosea kuhesabu. Kwa nini umwamini yule mzee na siyo mfanyakazi wa benk. Kwa hela nyingi kama hiyo, mfanyakazi hana namna ya kuibeba. Kumbuka kuna kamera inamwangalia.
 
Sasa mzee ameshajaza fomu nyingine na kuondoka asaidiweje wewe uliokuwa mubashara nyuma yake ukashindwa kumsaidia unakuja kutafuta msaada huku? Ur not serious dude
 
Kweli kabisa mkuu,siyo kahama tu nmb benk matawi yao wanahuo mchezo.hasa ukiwa na ela kuanzia million mbili
 
Hapo huwezi kuhitimisha kuwa mzee alikuwa na hela sahihi kama alivyokuwa anadai, usiamini mtu kwa kumuangalia tu juu juu.

Bank Teller ni vigumu sana (sisemi hawezi) kukuibia. So, ukweli anaujua babu na bank teller. Kwa kuwa alikubali kujaza fomu hapo hakuna msaada wowote.
 
Hapo huwezi kuhitimisha kuwa mzee alikuwa na hela sahihi kama alivyokuwa anadai, usiamini mtu kwa kumuangalia tu juu juu. Bank Teller ni vigumu sana (sisemi hawezi) kukuibia. So, ukweli anaujua babu na bank teller. Kwa kuwa alikubali kujaza fomu hapo hakuna msaada wowote.

Ndugu zangu landa nyie niwafanyakazi wa benki hivyo mnatetea.Nimeseama utafit wangu mtaani unaonyesha kunamchezo mchafu hapo nmb kahama karibu na stand ya mabasi,.

Kunamama Fulani alifanyiwa hivyo akaibiwa laki sta na ni mwalimu.. bahati nzuri akafahamu yule dada anapokaa basi dada akasema apewe mda aitafute fedha nakweli alimlipa nakumuomba radhi, hivyo tusipishe tu.

hawa wazee wakuuza umbaku vijijini hawana uelewa wa mabenki ila wanafanya trust sasa mabinti na mamenger uchwara wanataka hera ya sikuuu basi wanawaibia wateja hasa waliozubaa
 
Ndugu zangu landa nyie niwafanyakazi wa benki hivyo mnatetea.Nimeseama utafit wangu mtaani unaonyesha kunamchezo mchafu hapo nmb kahama karibu na stand ya mabasi,. Kunamama Fulani alifanyiwa hivyo akaibiwa laki sta na ni mwalimu.. bahati nzuri akafahamu yule dada anapokaa basi dada akasema apewe mda aitafute fedha nakweli alimlipa nakumuomba radhi, hivyo tusipishe tu. hawa wazee wakuuza umbaku vijijini hawana uelewa wa mabenki ila wanafanya trust sasa mabinti na mamenger uchwara wanataka hera ya sikuuu basi wanawaibia wateja hasa waliozubaa
Nilichokuwa namaanisha mie, ni vigumu ku'jump into conclusion kwa hilo tukio la babu, sitetei. Anyways, kama umefanya utafiti sawa. Lakini utafiti lazima uje na mapendekezo ya solution.
 
Nilichokuwa namaanisha mie, ni vigumu ku'jump into conclusion kwa hilo tukio la babu, sitetei. Anyways, kama umefanya utafiti sawa. Lakini utafiti lazima uje na mapendekezo ya solution.

anyway, kwa kuwa CCTV zilikuwepo,, je huyu mzee anaweza kuaidiawaje kusudi auone uongozi waweze kutrack cctv kwa mda husiaka ili waone yule dada kama alichukua burungutu akaliweka pembeni na hakuliweka kwenye machine ya kuhesabia.

Sisi vijana wa sasa lazima tukatae ufedhuri kwa wazee wetu na kwa benki..toeni ushauri wa nini kifanyike kuhakikisha haki inapatikana
 
Hiyoo branch hiyoo kuna dogo mmoja alinipiga elfu 20, nikiwa on transit to mwanza nienda kaunta kudroo 1.5m, nafika Hoteli mwanza kuhesabu nikakuta punguf ya 20 elfu. hiyo branch ni noma kweli kweli
 
anyway, kwa kuwa CCTV zilikuwepo,, je huyu mzee anaweza kuaidiawaje kusudi auone uongozi waweze kutrack cctv kwa mda husiaka ili waone yule dada kama alichukua burungutu akaliweka pembeni na hakuliweka kwenye machine ya kuhesabia. Sisi vijana wa sasa lazima tukatae ufedhuri kwa wazee wetu na kwa benki..toeni ushauri wa nini kifanyike kuhakikisha haki inapatikana
Mara nyingi unakuwa ni mchezo unaohusisha zaidi ya huyo teller. Kama ni kuangalia kamera hao hao waangaliaji huenda wako kwenye game!
 
Ndugu zangu landa nyie niwafanyakazi wa benki hivyo mnatetea.Nimeseama utafit wangu mtaani unaonyesha kunamchezo mchafu hapo nmb kahama karibu na stand ya mabasi,. Kunamama Fulani alifanyiwa hivyo akaibiwa laki sta na ni mwalimu.. bahati nzuri akafahamu yule dada anapokaa basi dada akasema apewe mda aitafute fedha nakweli alimlipa nakumuomba radhi, hivyo tusipishe tu. hawa wazee wakuuza umbaku vijijini hawana uelewa wa mabenki ila wanafanya trust sasa mabinti na mamenger uchwara wanataka hera ya sikuuu basi wanawaibia wateja hasa waliozubaa
Baadhi ya benki ni wezi kabisa na nadhani unachoandika na ulicho-observe kina ukweli. Hasa wakiona mtu amekaa kijiji-kijiji!
 
Back
Top Bottom