NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Kwa anayejua wanakokotoaje makato hasa kwa NMB-Mobile ukiangalia salio.Maana nilikuwa na salio la Tshs 350 kwenye simu,kuangalia tu salio kwa nmb-mobile mara moja nimebakiwa na Tsh 44.65 dah...Na kule akaunti sijui wanakata ngapi?...Pili: Kwa nini,mteja akitaka kujitoa Nmb -mobile wanagoma.?
Mbona kujitoa simple tu, we renew line uluojiungia nmb mobile
 
Sijui tatizo ni nini.

Maana huduma ninayoipata mimi wewe huipati na kinyume chake pia.

Sikujua kama kuna notificationa kwa njia SMS pindi utoapo Pesa kwenye Account
Sina hiyo notification mkuu,na ningependa kweli kuipata bila kuhangaika kuangalia salio.
 
Mkuu faida za NMB mobile ni nyingi ukilinganisha na hela wanazokata,mbona ni kidogo sana.Anyway kila mtu ana mtizamo wake.

Kweli faida zipo.

Unaweza kuokoa pesa endapo ukakutana na matapeli wanaoiba ATM card na kukimbilia kutoa pesa ATM zingine kwa kuhamishia pesa M-Pesa au mtandao uliojiungia NMB mobile.
 
Kweli faida zipo.

Unaweza kuokoa pesa endapo ukakutana na matapeli wanaoiba ATM card na kukimbilia kutoa pesa ATM zingine kwa kuhamishia pesa M-Pesa au mtandao uliojiungia NMB mobile.
Mkuu hivi mtu anaweza kutoka hela kwenye account yako akiwa na ATM card yako bila kuwa na password(namba ya siri),hebu nitonye,maana mimi nilidhani haiwezekani.
 
Yani haya mabenki yanamkamua mwananchi sana,ukitaka kutoa milioni ni lazima utoa mara tano,maana wameweka 5000 note tu na ukitoa mara tano unakatwa charges 5 times...Ni wizi Mkubwa.
 
Hili swali litakuwa ni gumu!! Mimi sijui hata wanakataga ngapi nikitoa hela kwenye ATM,yaani mi ni kuweka na kutoa tu,sijui nakatwa ngapi! Nilidhani ntapata mwanga hapa ila bado giza tu!
 
Yani haya mabenki yanamkamua mwananchi sana,ukitaka kutoa milioni ni lazima utoa mara tano,maana wameweka 5000 note tu na ukitoa mara tano unakatwa charges 5 times...Ni wizi Mkubwa.
Hii mpya mi najua kutoa milioni unatakiwa kutoa maratatu maana maximum kwa mkupuo ni lakini nne
 
Back
Top Bottom