NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Mkuu hivi mtu anaweza kutoka hela kwenye account yako akiwa na ATM card yako bila kuwa na password(namba ya siri),hebu nitonye,maana mimi nilidhani haiwezekani.
Jamaa anaweza kuwa amekufuatilia muda mrefu akaisoma password, then akifanikiwa kuiba ATM CARD au simu ni kufanya muamala fasta. Na sio lazima awe mwizi anaweza kuwa hata mwanao aliyeasi au mume uliyemtishia kumuacha [emoji3]
 
Hili swali litakuwa ni gumu!! Mimi sijui hata wanakataga ngapi nikitoa hela kwenye ATM,yaani mi ni kuweka na kutoa tu,sijui nakatwa ngapi! Nilidhani ntapata mwanga hapa ila bado giza tu!
Ukitaka kujua gharama unaenda bank unaomba bank statement ya akaunti yako.
Kwa mfano unaweza omba ya mwezi wa kwanza, wanaprint na kukupatia. Itaonesha miamala yote iliyofanyika na gharama walizokukata.
 
Kwa anayejua wanakokotoaje makato hasa kwa NMB-Mobile ukiangalia salio.Maana nilikuwa na salio la Tshs 350 kwenye simu,kuangalia tu salio kwa nmb-mobile mara moja nimebakiwa na Tsh 44.65 dah...Na kule akaunti sijui wanakata ngapi?...Pili: Kwa nini,mteja akitaka kujitoa Nmb -mobile wanagoma.?
250 wanakata bila shaka ulikuwa unaangalia mshahara,bado mpaka mkulu aingie ofisini.j3
 
Mkuu hivi mtu anaweza kutoka hela kwenye account yako akiwa na ATM card yako bila kuwa na password(namba ya siri),hebu nitonye,maana mimi nilidhani haiwezekani.

Kuna mtindo wa kitapeli umeshamiri sana kwenye ATM machine, mtu anaweza kuja akajidai anataka kukusaidia ukiwa unataka kutoa hela, ukimuruhusu atakuchanganya kwa mbinu tofauti tofauti hadi utajikuta umeandika password yako ikaonekana kwenye secreen tofauti na kuonesha ****.

Hapo ataoina huku tayari kashabadili card yako na card fake amabzo wanazitumia kufanya huo mchezo, wewe ambaye hujui hicho kitu utachiwa machine inaanza kugoma na kukuleta habari ambazo ni tofauti, ukianza kukabiliana na machine yeye tapeli anasepa na kwenda kutoa pesa kwingine na card yako.

Mada ya kuzungumzia huu utapeli ishazungumziwa humu na kuambatanishwa video kabisa.

Kwa kifupi usiruhusu mtu yeyote akusaidie ukiwa ATM machine labda awe mlinzi tu.

Hao matapeli wanakuwa na card nyingi fake wanatembea nazo kufanya huo utapeli, akikuambia nikusaidie halafu akiishika kadi yako anabadili na kuweka card fake halafu anabonyeza akikuambia weka password ndio zitaonekana kama 1234 badala ya **** akiziona anazikariri halafu atabonyeza haraka ok, machine italeta taarifa zisizoeleweka kama nioivyosema hapo mwanzoni, muda huo yeye anaondoka maana kashamaliza kazi yake.

NB: Usiasidiwe na mtu yeyote kwenye ATM machine labda awe mazazi wako au ndugu zako pamoja na mlinzi tu.
 
260f314e7b4a96e22cfd432dab4bf456.jpg

pemgtoonet.com
Mwifwa
areafiftyone
King Kong III
Capt Tamar
Mponda 02
kiumbempole
 
Mkuu faida za NMB mobile ni nyingi ukilinganisha na hela wanazokata,mbona ni kidogo sana.Anyway kila mtu ana mtizamo wake.
Mimi naona faida ni kubwa. Kuna mtu huwa anatumia gharama sana kuifuata ATM ya NMB. Nimejaribu kumuelezea haelewi. [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji119]
 
Kwa anayejua wanakokotoaje makato hasa kwa NMB-Mobile ukiangalia salio.Maana nilikuwa na salio la Tshs 350 kwenye simu,kuangalia tu salio kwa nmb-mobile mara moja nimebakiwa na Tsh 44.65 dah...Na kule akaunti sijui wanakata ngapi?...Pili: Kwa nini,mteja akitaka kujitoa Nmb -mobile wanagoma.?
Hahaha unataka ujitoeje zaidi Tsh 44.65 waachie tu utakuwa umetoka hivyo, angalia salio hadi ziishe bank.
 
Kwani unaruhusiwa kuunga nmb mobile mitandao zaidi ya mmoja wa cm?
NMB mobile inaruhusu kutumia mtandao mmoja mkuu,ila unaweza kuhamisha hela kutoka Bank kwenda Vodacom,HaloPesa,TigoPesa,Airtel Money nk. kama sim yako imeunganishwa.
 
Back
Top Bottom