NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1.
Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Kwanini mmeondoa huduma ya kununua vifurushi vya muda wa maongezi kwa simu?

Kwanini hamjawatangazia wateja kuwa huduma ya kununua muda wa maongezi kwa simu imeondolewa hivyo wateja watafute njia mbadala?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
NMB wananunua mikopo ya benk nyingine?
 
Napata tabu sana kuuliza bila kujibiwa. Haya nimeenda mwenyewe. Nimejibiwa mnanunua kwa faida mqaja JF mwenzangu
 
Mimi huwa nikitaka kutoa laki 5 na elfu sitini kwenye ATM huwa inakataa naambiwa kiasi kimezidi inabidi tena niwe natoa laki 2 mbili,hivi hapo si makato yanakuwa juu au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NMB Nina maoni/malalamiko.

Nimefanya biashara na mtu, nimempa bidhaa amenitumia pesa Pesa zaidi ya laki nne kwa Pesa Fasta (Simjui/hanijui). Baada ya kukamilisha deal nikaenda ATM niweze ku withdraw ile pesa. Naambiwa kiwango hakiwezi kutoka kwenye ATM.

Nikaingia ndani kuomba msaada, nikaambiwa hiyo helahaiwezikutoka, nisubiri mpaka siku 7 irudi kwa alietuma ili anitumie tena....

Hapa nimejifunza vitu vitatu.
1. Inaruhusu utapeli, what if yule mtu asipo tuma tena baada ya hela kurudi.
(Kama hela kutoka ni max 400,000 kwanini mruhusu itumwe zaidi ya hicho kiwango na mnajua inatakiwa kuitoa kwa round moja yote).
2. Aliedevelop hii service alifikiria pafupi sana , kwanini hii huduma sio flexible?
3. Wahudumu wenu wanatuhamasisha tutume pesa kwa njia nyingine, maana yake hii njia ya Pesa Fasta ni mbovu/incompetent.

Naomba msaada wakuitoa hii hela maana tuliefanya nae biashara hapatikani tena. Nahisi kutapeliwa.

Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kero yangu kubwa ni
nina miaka mitatu tangu niombe uwakala wa NMB , niliambiwa nifungue account mbili nikafungua lakini mpaka leo sijapata hiyo mashine mwanzo niliambiwa mashine zimeisha naomba kujua kuna tatizo gani asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau wa huduma za kifedha naomba ufafanuzi ikiwa Uendeshaji wa NMB Wakala Ifumbula, Wilayani Tanganyika ni Tawi la NMB au biashara binafsi.

Jengo linaonekana kama lilijengwa na Benki ya NMB, watohuduma wanafanya kazi muda wa kazi sawa na NMB lakini ofisi yao imeandikwa NMB wakala na makato yao ni ya viwango vya wakala! Kama NMB inaendesha tawi lake na kutoza wateja wake kama wakala itakuwa haiwatendei haki wateja wake wa NMB!
 
Nimejitolea kumsaidia mtoto mmoja yupo kwenye mazingira magumu ni yatima
nilikuja NMB kumfungulia bank account nimwekee fedha kidogo kidogo ili aweze kujisomesha akifika Sekondari

Kuna teller wa NMB ananiambia bila affidavit siwezi kumfungulia bank account cz mimi sio mzazi
sasa nawashangaa sana, account atakua anatoa hela mwenyewe affidavit yangu ya nini
i had plans ya kuwaomba ndugu na jamaa kumchangia kwenye hiyo account lakini mnakwamisha

ilitakiwa iwe rahisi kuweka hela, iwe ngumu kuzitoa, nyie mnafanya the opposite alaf mnalalamika makusanyo madogo
 
Hivi huko NMB, Huyo aliyekuwa amepangwa kujibu hoja/maswali kwenye hii page yenu amefariki? Sasa akifa haiwezekani kuajiri mwingine ajibu?

MODS fungeni hii page maana imekuwa kama dustbin watu wanatiririka shida zao na hakuna majibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom