No body cares: Watu tupo bize mtandaoni, tume-lose touch na human connection

Ww unakula mabinti wa kazi nyumbani kwako inamaana hukupewa malezi mazuri jirani??
 
Mimi naona ifike pahala tukubaliane tu na hali halisi kwamba dunia imeshabadilika, kushindwa kukubali nako kunafanya mtu azidi kujiongezea stress tu, hakuna namna hapa ndipo dunia ilipofikia and there is nothing we can do about it
Kweli mkuu Dunia imebadilika na tuende nayo lakini je kwenye hizi technologies kama simu vijana wanazitumia kama wengine wanavyoweka vitu vya kujiendeleza kwa biashara ila vijana wetu kutwa mambo ya kijinga tu

Hata kwa kina Dada, kuna mapishi, mapambo, na vitu vingi sana vya kujifunza bure ila fursa wanachezea tu

Leo watu wamewekewa utajiri kwenye kiganja ila wana bet tu
Wengine wanaona simu ni kuchat tu
 
Yan hata misibani kila mtu busy na simu Mfiwa hafarijiwi tena kama zamani..... Atajijua mwenyeweeee

Huzuni kuuu
Na bado. Ubize huo umetupeleka hata kuwasahau wazee wetu (ambao hawakubahatika kutumia simu hizi za viganjani) kwamba wanahitaji uangalizi wa karibu, kuwatembelea na kuwasalimia, kuwasaidia kila inapowezekana, kuongea nao na kuwachangamsha ili watutemee mate a.k.a. Watubariki lakini badala yake tunawatelekeza kama ilivyo kwa wenzetu, na mwisho itakuwa ni kuwahamishia nyumba za wazee wakatunzwe huko na mtu atakayelipwa mshahara kitu ambacho ni sawa na kusema watajijua wenyeweeeeeee.
Tunakosa baraka za wazee waliotuleta hapa duniani na tunapata laana halafu tunaanza kulia-lia eti maisha ni magumu tunaomba misaada mitandaoni eti msaada tutani.
 
Ni kweli kabisa....
Zama zimebadilika Mkuu, saizi kila mtu yupo busy na simu yake, yan bora asile lakini aweke bundle aingie IG
 
YES exactly. Wapo wanaoridhika eti bora mtoto halafu kesho mtoto anaharibika na mzazi huyo huyo utamsikia "Oh! yan, Toto gani hili? ni afadhali hata nisingelizaa litoto hili."
Mtoto anaharibika kwa sababu mzazi/mlezi anazembea kimalezi tangu akiwa mdogo, baadae likishakuwa tatizo sio rahisi kurekebishika.
 
Facts💯💯
 
Kila kizazi na challenges zake. Imagine vizazi viwili mbele AI, automation, robotics na Neuralinks zimeshika kasi. Unafikiri watu wataishi maisha gani?

Dunia ndiko inakoelekea na hakuna kitu utafanya!
AI, automation na robotics zipo kuchallenge technological development sema watu wana mentality ya ovyo kuzihusu. Kuna watu wamezitumia vzuri na kuna wengine ambao hawako aware na nini wafanye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…