No body cares: Watu tupo bize mtandaoni, tume-lose touch na human connection

Kwenye heading waombe Mods wafanye editing. No Body isomeke Nobody
 
Mkuu binafsi ni kati ya watu ambao natamani watu wote duniani wangekuwa decent, yani kusiwe na uovu hata mmoja huwa naumizwa sana na maovu ya watu hata ambao hawanihusu, mwisho wa siku nikaona kama ninavyozidi kuumia ndivyo ninavyozidi kujipa stress

Kuna muda nakaa nafikiria hivi chanzo cha haya maovu yote ni nini na nini kifanyike ili dunia ibadilike kusiwe na maovu, lakini unakutana na watu ambao hawana mpango wala dalili ya kubadilika whether uwashauri, au ufanye mwenyewe haisaidii wao hayo ndio maisha waliyoyachagua

Unategemea mabadiliko gani kwenye dunia ambayo pesa na mali ndio kila kitu haijalishi umevipataje, mtu akitenda mema anaonekana mjinga na akitenda mabaya anaonekana mjanja unategemea mabadiliko gani kwenye dunia ambayo ngono ni kama chakula, watu wanazini tu hawajali kuhusu ndoa mtu akitunza bikira hadi ukubwani anaonekana mpumbavu
 

 
Mleta mada asante kwa mada hii, ni kama vile umenizungumzia mimi!
Uhalisia wangu si mtu wa kujichanganya na watu tokea udogo wangu, ni mtu mwenye udhaifu wa uoga na aibu na ukimya, tokea darasa la chekechea nimekuwa wakujitenga na wenzangu na kutengwa pia.
Nilianza kuwa na sim yenye internet kati ya 2010, ilipofika 2012 niliijua jf na kujinga kuwa mwanachama mtumiaji wa jf kila siku kwa kusoma kutoa maoni na kutoa mada.
Ila nimekuwa disappointment kwa vile naona niko karibu na watu walionizidi sana!
Elimu yangu ni ndogo, uchumi wangu ni mdogo!
Ninakuwa mpweke sana na mnyonge sana lakini siachi kuwa Jf kila leo.

Kama nisingekuwa mfutiliaji wa Jf kwa kiasi hiki labda nisingejiona mnyonge na asiye na thamani kiasi hiki, hakika internet na mitandao wa kijamii vina athiri sana.
 
Upo sahihi sana mkuu, mm mwenyew huwa na fadhaika sana kuona jinsi generation yetu inapoelekea... ni dhahiri kua hatuwezi badilisha chochote, ila kama m nilivyo sema "nobody cares" so ni personal change ndo inayohitajika. Hii ina manufaa japo yanaweza yasionekane collectively. Imefikia pahala I don’t care too inabidi kuacha kuangalia kinacho endelea na kufocus kwenye reality ambayo mm mwenyew nataka niwe. This world is heartless 💔

We can't change the world but we can make the world a better place.
 
Umezungumza vizuri hayo ulotaja si mageni na yamekuwepo miaka nenda rudi huenda yameshamiri sababu ya kukua kwa tech. n.k

Lakini ninachomaanisha kuna baadhi ya mambo hatuwezi kuyaishi tena nyakati hizi, mf. Socialization iliyokuwepo zamani.

Au watu kuwa bize mtandaoni unadhani ni kazi rahisi kuwafanya wasiwe bize mtandaoni na wawe bize na mambo mengine, wangapi wataweza kwa mazingira tuliyopo?
 
Pole sana, hii imetukumba wengi sana! Naweza kurelate na ww kuhusu kujitenga na kutengwa! Ina madhara mengi hasa psychological. Na tatizo la mitandao watu hawana sympathy hata kidogo na pia hawakujui hivyo hata ile kujali kua huyu ni mtu kama mm na anahisia kama mm inakua ngumu. Mm nahisi kwasabau ya kutengwa na kujiona wapweke imetusababisha wengi kuwa wahanga.

Jaribu kfatilia mada nzuri kama hizi hapa Jf achana na mada mbaya! Au hata ukifata hizo mada nenda kwa lengo la kujifurahisha. Usichukulie serious, hakuna anaejua unapitia nini hapa! Pia jaribu kuondoa mawazo mabaya kuhusu kutengwa ndo dunia ilivyo, watu hatujaliani kama zamaini.
 
Yessss sureee
 
We do care, but those we care about, dont even care about themselves..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…