Noti ya mia tano ya zamani inahitajika,iwe na nyati,nyoka,jengo pamoja na picha ya nyerere ikiwa kwa ndani,offer 120k(laki na ishirini).

Huo ni utapeli gani?

Ni weezy na utapeli tu ,haujawai kusikia jinsi watu wanavyotapeliwa kwa kutafuta hela za mjerumani ,mercury nyekundu na vijipesa kama hivyo vya TZ? Na hii ni moja ya style ya UTAPELI inaanza mtu anahitaji mia 5 ya noti(Kwa laki na 20) ,kisha anatokeza TAPELI mwenzake wanasema kuna mtu anazo yupo Morogoro anauza kwa elfu 50(Hapa unaona unapata cha juu elfu 70) kumbe huyo wa Moro ni Tapeli mwenzake 😀 😀 then unaingizwa mtu kati unapukutishwa mchana kweupe.
 
Huu ni utapeli, tafuteni kazi halali mfanye acheni kuumiza watu kima nyie

Mambo ya kizamani kabisa haya
Utapeli kivipi,mimi dalali nimepata boss namuunganisha na mwenye mali,pesa haina haramu mkuu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ogopa matapeli.... tatizo ni ujinga wa wabongo wenyewe ndio tatizo

Mimi niliwahi shuhudia mtu analipa 200k ukienda kupiga mluzi makaburini

Nakumbuka tulikua tunacheza Mpira kwenye uwanja wa kanisa la kikatoliki akaja mbaba mmoja smart akamtaka kijana mmoja ambae anaweza kufanya hivyo kwenye makaburi ya kanisa

Matapeli nao wamo ukikaa kizembe umeishaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…