Mkuu dhamira yako hasa ni nini?
Ushasema wewe huwezi kuweka feza zako huko na ukaeleweka sasa mbona kama unatengeneza chain ndefu ambayo haina maana yoyote?
Kwahiyo pia akitokea mtu akakushauri ukaweke Feza zako Bank katika Fixed Account, napo utataka uanze kujua ni manager gani alianzisha Fixed ACC, walikaaa kikao lini, wangapi wakakubali na wangapi wakakataa na walitumia vifungu gani vya katiba Yao?
Yani BOT kuweka mfumo wa kusaidia Wanachi katika uwekezekaji wa mitaji ni hadi Bunge likae,ujue kama lilianzia wizarani au kwa mtu binafsi umalizie na vifungu vya Sheria
Unauliza Mambo mengi ilimradi tu wewe uonekane wa tofauti sana, uonekane una Akili sana kuliko wanaoweka pesa zao, uonekane Mjanja sana, uonekane unajua sana sheria
Vile Unahoji kuhusu Bank kuu ya Tanzania as if ni Saccos/vikoba/Vikundi vya kina Mama mtaani kwenu, ushasema hutaki we acha wafanye wenye uhitaji usilete ujuaji mwingi ilhali hauna maana yoyote
Au uliwahi kuskia mtu katapeliwa huko kwenye UTT ili utujuze ilikuwaje mkuu?