Now mil 50 UTT, napambana ifike mil 65 mwaka huu

Nenda kwenye ofisi zao, utapata elimu nzuri sana na utawaelewa.
 
Got you. Mimi UTT niko Liquid fund, nilikuwaga pia na Bond. Ila Bond 10days kusubiria pesa vikanishinda, nikazitoa zote nikabaki na Liquid.
Inasaidia, kuna uhitaji mwingine wa pesa unakuwaga sio wa lazima sana, ila km pesa iko bank kuifikia ni chap sanaa.
Ila UTT kuna kauvivu flani kuifata ‘ kanasaidia
 
Asante sana. Ni kampuni ya serikali. Bunge lilihusishwa wakati wa uanzishwaji au ni wizara tu au ni nani hasa? Kwa vifungu gani vya sheria? Board of directors na watendaji wake wakuu wanachaguliwa/kuteuliwa na nani?
 
Asante sana. Ni kampuni ya serikali. Bunge lilihusishwa wakati wa uanzishwaji au ni wizara tu au ni nani hasa? Kwa vifungu gani vya sheria? Board of directors na watendaji wake wakuu wanachaguliwa/kuteuliwa na nani?
Mkuu dhamira yako hasa ni nini?

Ushasema wewe huwezi kuweka feza zako huko na ukaeleweka sasa mbona kama unatengeneza chain ndefu ambayo haina maana yoyote?

Kwahiyo pia akitokea mtu akakushauri ukaweke Feza zako Bank katika Fixed Account, napo utataka uanze kujua ni manager gani alianzisha Fixed ACC, walikaaa kikao lini, wangapi wakakubali na wangapi wakakataa na walitumia vifungu gani vya katiba Yao?

Yani BOT kuweka mfumo wa kusaidia Wanachi katika uwekezekaji wa mitaji ni hadi Bunge likae,ujue kama lilianzia wizarani au kwa mtu binafsi umalizie na vifungu vya Sheria

Unauliza Mambo mengi ilimradi tu wewe uonekane wa tofauti sana, uonekane una Akili sana kuliko wanaoweka pesa zao, uonekane Mjanja sana, uonekane unajua sana sheria

Vile Unahoji kuhusu Bank kuu ya Tanzania as if ni Saccos/vikoba/Vikundi vya kina Mama mtaani kwenu, ushasema hutaki we acha wafanye wenye uhitaji usilete ujuaji mwingi ilhali hauna maana yoyote

Au uliwahi kuskia mtu katapeliwa huko kwenye UTT ili utujuze ilikuwaje mkuu?
 
Ahaaa. Sasa mkuu hapa umeweka mpira makwapani kiana. Mimi nataka kujua ili niondoa wasiwasi wangu. People change their minds, don't they?"
 
Ahaaa. Sasa mkuu hapa umeweka mpira makwapani kiana. Mimi nataka kujua ili niondoa wasiwasi wangu. People change their minds, don't they?"
UTT ni mutual fund (tumia Google kujua maana ya mutual fund) ambayo imeanzishwa maalum kwa ajili ya watanzania baada ya serikali (Mkapa) kuona watanzania hawana access na mifuk o mikubwa ya mitaji/uwekezaji.
Ipo chini ya Wizara ya fedha, imesajiliwa B.O.T na Mamlaka ya soko la mitaji C.M.S.A.

Wanabodi wake wengi ni wataalam wa fedha,uchumi na sheria.
Huku hakuna janja janja kwani ndipo moja ya taasisi kubwa inayoikopesha fedha serikali. Uendeshaji wake ni wa umakini coz inaisaidia serikali kupata credit rating nzuri kimataifa na ambayo huipa serikali unafuu wa kupata mikopo nje na uwekezaji.
 
Asante mkuu. Mutual fund najua maana yake. Angalau wewe umekuja na maelezo. Unajua watanzania wengi tuna utamaduni wa ''kutii bila shuruti'' na ukionekana kama unahoji basi wewe ni kibaraka na mpingaji. Mimi ni mtanzania na nimekulia Tanzania ambayo ''project'' nyingi zinazoanzishwa huwa zinakuwa hazina mwisho mzuri hivyo nina haki kabisa ya kuhoji.
 
SI kama hivi... Au we huoni kama ni promo hii
Bro,sio kupigiwa debe. Just tunawaeleza watu juu ya namna tofauti za low risk investment.
Ndiyo mana katika moja ya maoni yangu ,nimeshauri watu wajisomee juu ya financial markets.
Hata nawe unaweza ukafanya hivyo,mana Kuna course za online za bure nyingi tu Coursera, YouTube.,pitia platform kubwa kama Bloomberg ujifunze.
Ila yote ya yote ni hiyari ya mtu, ila jifunze uongeze maarifa siyo kubaki hivyo.
 
Nakuelewa mkuu,kwangu ilichukua zaidi ya miezi 6 kufuatilia juu ya Masuala ya Uchumi.
Fursa ni nyingi ila bado serikali haijaweza kuweka haya mambo vyuoni. Mwisho wa siku wahindi ndiyo wanaomiliki Uchumi wetu.
 
Nakuelewa mkuu,kwangu ilichukua zaidi ya miezi 6 kufuatilia juu ya Masuala ya Uchumi.
Fursa ni nyingi ila bado serikali haijaweza kuweka haya mambo vyuoni. Mwisho wa siku wahindi ndiyo wanaomiliki Uchumi wetu.
Ni fursa nzuri,ila nashangaa serikali haijaweka wazi kama ulivyo sema kwa kutoa elimu..mwisho wa siku wanafaidi wachache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…