Nimesoma uzi wote comment kwa comment, unajaribu kufanya nini kwenye huu uzi wako
brazaj
Umenishangaza zaidi ulivyozungumzia kuwa CDM na kuwa CDM zaidi, lengo la huu mjadala nini? Nafahamu siku zote unaandika unaandika kwa mlengo wa CDM. Sasa hili la uCDM na UCDM zaidi?????
Sote tunafahamu utoaji wa taarifa na nukuu, hakuna aliyepewa written document kati ya hao ambayo ingewaguide chakusema, lengo la msingi: Wote wametoa taarifa ile ile, na bila shaka wote wanakubali ufanyike uchunguzi huru.
Lengo la title ya uzi wako na content yake na vimaswali unavyouliza kwenye comments ni ipi?
Niijibu comment yako hii aya kwa aya kuhakikisha siachi kitu.
Ninafanya hivyo katika moyo ule ule wa kuhakikisha miye kama mtoa mada sitoi nafasi kwa upotoshaji wowote:
Aya yako #1:
Umefanya vyema kuusoma uzi wote kama unavyosema mwenyewe. Hii ikizingatiwa kuwa wengine hatuandiki humu kupoteza muda au kishabiki.
Aya yako #2:
Originally mada ilikuwa chini ya title:
"Nukuu tata kutoka kwenye tukio la kutekwa marehemu mzee Kibao."
Sina hakika uliposoma wewe ilikuwa katika title ipi maana zimekuwapo 3 tofauti.
Moderator pia waliongeza reference ya kusoma ambayo haikuwamo originally.
Siku zote ninaamini maboresho yoyote ya
Moderator ni ya nia njema.
Sielewi ni kipi kimekushangaza wewe kwenye mada hii niliyoiandika mimi kwa nia njema katika kumwomboleza tu, mzee huyu ambaye ni dhahiri kuwa amedhulumiwa.
Zingatia mada hii haina neno CDM wala uCDM popote. Sielewi wapi umeyaokota hayo.
Ieleweke miye siku zote ninaandika kwa mlengo wa haki.
Kwamba kwa kuona kwako nimekuwa nikiandika kwa mlengo wa CDM, labda ni kwa sababu miwili hiyo imekuwa ikikutana pamoja.
Hapa ni mfano wake:
Makamu wa Rais wa zamani, Cheney (Republican) kumpigia kura Kamala Harris
Aya yako #3:
Unakubaliana nami kuhusu lugha gongana ambayo ndicho pekee nilicho orodhesha. Laiti ungekuwa umesoma pote ungekuwa umeona maangalizo kama haya:
"Panapotokea jambo lenye kugusa jamii kila mtu husema lake."
Wapi umeona kuna kesi au hata kulaumiwa kwa mtu kusema lolote?
Kwamba nawe unakubaliana nami lugha hugongana sasa msingi wa kushangazwa kwako na hoja yangu kumbe ni upi ndugu?
Kwamba unasema wao wametaka uchunguzi huru? Uliona au kuelewa maana ya "which is which" kwenye hitimisho?
Kumbe wewe, mimi na yule kuongezea sauti kwenye hilo wewe inakukera?
Aya yako #3:
Title yangu inasomeka wazi. Contents zote ni nukuu. Indeed, hakuna swali hata moja.
Kumbe basi hivi unavyoviita "vimaswali vyako" ndiyo vidude gani au unaviona wapi ewe
binti kiziwi?